Wanaume: Vijue visa vya michepuko

Cheps nyingine nuksi tupu. Ukute hata ladha hana unajikaza kiume lakini ndo anataka kumpindua bi mkubwa home
Tatizo unaweka kambi,
Kanuni ukishaona hailipi na ukaribu unautokomeza.
 
Status
'Status' na Majukumu/Uwajibikaji Lakini ujue.
 
Hivi mkuu unakaa pande zipi!!. .. Mana daah una maneno mpaka nashangaa...
Unaonekana wewe ni muongeaji wa kupindukia.
Mchague mmoja kati ya hao ulowamention then atakudadavulia kiroho sayona
 
Hivi mkuu unakaa pande zipi!!. .. Mana daah una maneno mpaka nashangaa...
Unaonekana wewe ni muongeaji wa kupindukia.
Mkuu mimi ni mpole sana... Huwezi amini
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nimecheka eti hata uoge na omo
 
Michepuko inataka PESA, MUDA na UVUMILIVU kupita hata wife home, siku umefulia jiandae kupewa maneno ya shombo.
 
Michepuko sina hamu nayo kabisa, yaani ina bajeti kali kuzidi hata hii ya kuhamia Dodoma, fikiria mchepuko eti unataka hela ya matumizi ya kila siku, mchango wa harusi (ndugu&marafiki). Ghafla unadai hauwezi kupanda bajaj kila siku unataka gari.. Mi ngoja nirejee kwa mke halali wa ndoa. Hizo hips za mchepuko kama dili azile basi.
 
Bora urudi tu kama mwana mpotevu, kuliko kuangamia
 
ila kiukweli wanaume hatuwatendei haki wake/wenza wetu, kuna siku hiyo side chick alikuwa anataka pesa sijui akasuke na kupata pesa ya kununulia nguo eti kuna sherehe ya bethidei ya shoga yake ili atokelezee, akaomba kama laki hivi. Namnukuu "baby naomba laki tuu si unajua kuna party ya fulani nataka nitokelezee" nikamsikilizaaaaa katika hiyo simu alopiga, alipomalipomaliza kuongea sikumjibu, nikakata simu, kisha nikakaa na kuanza kufikiria. Maana juzi kati tuu mama mwenye nyumba alitoka kuniomba pesa ya kufanya shopping na pocket money ya matumizi ya hapa na pale, nikamtoleaga nje kuwa sina pesa.

Aisee baada ya kukata simu ya huu mchepuko simu na kufikiria kwa muda, nikainua simu na kumpigia maza haus na kumwambia, ombi lake limesikilizwa. Nikirudi nitampatia kiasi alichoomba. Aisee niliporudi tuu home, nikakata kilo 2 na kumkabidhi fanya unachotaka kama ulivyoniambia. Aisee alishangaa, maana sijawahigi kumpa pesa kama hiyo kwa mkupuo. kesho yake narudi home nakuta kuna mchele, mafuta, unga maharagwe na mazagazaga mengine ya jikoni. Huku yeye akiwa kanunua gauni moja na mimi kanichukulia shati moja kama suprise. Aiseeee nilijiona nimeokoka katika mdomo wa mamba mchepuko.

washenzi sana hawa michepuko, Ila na sisi wanaume tunayatakaga haya matatizo ya michepuko.
 
Mkuu ulifanya jambo la maana. Nilishawahi kuwa na michepuko kadhaa, nianze na Maureen yeye alikuwa muuza duka la Nguo, kila akikupigia simu yake ujue ni kizinga cha haja. Kuna siku alinipigia eti kapata loss ya laki 3 dukani anaomba nimlipie nikamtumia laki 2, kesho yake akanipigia dear upo wapi? Nikamuambia nipo Arusha kikaz akadai nna hamu ya kukuona nikamkatia tiketi ya fastjet 230,000 (return ticket) sasa siku ya safari nakumbushia awahi airport eeh anadai eti kapata period (tumbo la hedhi) kalala hawezi kusafiri aisee nilipata hasira. Nikamblock na kufuta namba yake. Michepuko ni ugonjwa wa moyo.
 
Hahahahahahah

Wanasema...happy wife happy Life
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…