Wanaume tuwe na huruma, tuwe tunaacha hela ya matumizi nyumbani

raia_mwema

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
479
313
Let us be realistic, wanaume tubadilike tuwe na huruma kwa wake na wapenzi wetu, unakuta mwanaume unatoka asubuhi kwenda kazini hauachi hela ya matumizi, unategemea familia itaishi vipi?

Wapo wengine ambapo pamoja na kuwa mwanamke hana kazi hawajali hawaachi hela ya matumizi, mishahara ikitoka mwanaume haonekani nyumbani wiki nzima ukiisha ndio anarudi, mbaya zaidi unakuta nyumbani pana watoto wadogo wanaishia kuteseka.

Wapo wengine wanaorudi nyumbani usiku wa manane wakiwa wamelewa akifika ni kulala kesho alfajiri ameshatoka! Pia wengine huwapiga wake zao kama vile punda, tukumbuke wanawake nao binadamu kama sisi, ingekuwa wewe unafanyiwa hayo ungependa?

Tubadlike
 
Pole sana kwa yaliyokusibu au kugusika kwa namna Fulani. Inashauriwa mke asiwe mtunza goli. Jishughulishe mtu unaamka unashinda home miaka yote ili iwaje? Akipata tatizo la kudumu unategemea nini?
 
Over and Out..

obama-mic-drop.jpg
 
vijana wa sasa hv wanapenda tu kujisifia kuwa na rundo la watoto.. ila malezi ni ziiiroo.. maganda ya ndizi wao kazi kutelezea tu kwa mke.. hichi sasa hv ni kilio cha wanawake wengi sana walioolewa... hapa wanawake tujifunze kitu kwamba hawa viumbe ni wajibu wao kukutunza wewe na watoto zako.. kuanzia malazi mpk mavazi.. tutumie ustawi wa jamii ipasavyo.. watajirekebisha tu taka wasitake
 
Leo umekuwa raia mwema wa ukweli ukweli pongezi zangu 100% zifike kwenye kiti chako cha enzi.mawazo constructive sana.Ni kweli familia zetu zinasota kwa sababu ya viruka njia jamani tuache ama tupunguze ili familia xetu nazo zi enjoy matunda ya mikono yetu kwa kuwa ni baraka hata kwa mwenyezi mungu.
 
Alaf mwanaume akiletewa watoto wa 49 psnt ya mkemia mkuu wanalalamika.
Mfyuuuu
 
vijana wa sasa hv wanapenda tu kujisifia kuwa na rundo la watoto.. ila malezi ni ziiiroo.. maganda ya ndizi wao kazi kutelezea tu kwa mke.. hichi sasa hv ni kilio cha wanawake wengi sana walioolewa... hapa wanawake tujifunze kitu kwamba hawa viumbe ni wajibu wao kukutunza wewe na watoto zako.. kuanzia malazi mpk mavazi.. tutumie ustawi wa jamii ipasavyo.. watajirekebisha tu taka wasitake
Kabisa Mumy ila ni kukosa ubinadamu mana katika hali ya kawaida haiwezekani mume uondoke nyumbani hujaiachia kitu familia na bado roho yako ikawa na amani.

Mbadilike jamani kama mnaona ni majukumu mnaolea nini si mngebaki single ili muhudumie matumbo yenu pekee.
 
Pole sana kwa yaliyokusibu au kugusika kwa namna Fulani. Inashauriwa mke asiwe mtunza goli. Jishughulishe mtu unaamka unashinda home miaka yote ili iwaje? Akipata tatizo la kudumu unategemea nini?
Mkeo anaamka asubuhi...

Anakuandaa wewe na wanao

Anasafisha nyumba

Anaandaa chakula chenu

Anawafulia na kuwapigia pasi

Anahakikisha nyumba safi mazingira masafi

Halafu unamwita mtunza goli?????
 
Mkeo anaamka asubuhi...

Anakuandaa wewe na wanao

Anasafisha nyumba

Anaandaa chakula chenu

Anawafulia na kuwapigia pasi

Anahakikisha nyumba safi mazingira masafi

Halafu unamwita mtunza goli?????

watu hawana heshima kabisa kwa wake zao... kesho ye akiitwa mwanaume suruali anamind anasema kadharauliwa... ukimuona mwanaume hana kauli njema kwa wanawake mtilie shaka mwanaume huyo!!!
 
Nanyie wanawake sazingine mnajitakia wenyewe.

Mtu hakujali kwa mavazi
, wala chakula.
Lakini upotu, why don't you get back home!!.

Kunajamaayangu jirani hapa anaonekana smart lakini anaitesa sana familia yake mwanamke anatia huruma sana.
 
Back
Top Bottom