Wanaume tutafakari

ndayilagije

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
7,492
8,295
Naamini mko sawa kimwili, kiakili na kiroho.

Naomba tushirikishane hii tafakari yangu, maana peke yangu siwezi. Hivi karibuni kumeibuka hali isiyopendeza sana ya vifo vya wanaume baada ya kukimbiwa na wenza wao, mfano Ivan na Hanad. Lakini pia wanawake kama Ex Mrs Mbasha, Ex wa boss Ruge kuwakimbia wenza wao.

Ilizoeleka wanaume wakiacha lakini si kuachwa. Maana hawa wanawake wameumbwa kuwa wasaidizi wa wanaume kwa mujibu wa biblia kitabu cha kwanza,sura ya kwanza Mungu akasema :"si vema mwanaume awe peke yake,nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye".

Je wanaume wameshindwa kusimama katika nafasi zao za kuongoza hali wakisaidiwa na wanawake, kiasi cha wanawake kuona hata bila wanaume hao hakuna tatizo? Zingatia single parent wa kike ni wengi na wanalea watoto bila shida kuliko idadi ya wasingle baba wanaolea watoto.

Wababa tumeshindwa?
Karbuni.
 
Wanawake wasome maandiko matakatifu

Mwanamke n mtu anaweze kudanganyika haraka sana
Ndo maana Mapepo huwakumba wao

Mwanawake wanamapungufu kiasi furani.... ila uzuri maisha yanaendelea hakuna shida
 
Pamoja na mapungufu yetu,ww kama mwanaume umechukua hatua gani??halafu si wanawake wenye mapungufu hata nyie mnayo mengiiiii mno hakuna kiumbe kikamilifu chini ya jua iwe me/ke wote ni wakosefu tuu tumejawa na ubatili na kujilisha upepo,..

Muhimu kila kiumbe asimame kwenye mipaka yake na nafasi yake,mwanamke afanye wajibu wake na mwanaume vivo hivyo.
 
Kumbukeni nyie n wasaidizi wetu, mmetoka ubavuni kwetu
 
Zamani swala la Ndoa ilikuwa ni Mchakato ambao unahusisha Majadiliano na viapo mbali mbali hivyo hata Wanandoa matarajio yao hayakuwa tofauti sana na mchakato uliopitiwa..,
Hv ss swala la Ndoa limekuwa ni rahisi kuliko hata rahisi yenyewe na Matarajio ya Wanandoa yamekuwa ni makubwa kuliko uhalisia wenyewe at last divorce ndo imekuwa suluhisho!!!
 
Naamini mko sawa kimwili,kiakili na kiroho.
Naomba tushirikishane hii tafakari yangu,maana peke yangu siwezi. Hivi karibuni kumeibuka hali isiyopendeza sana ya vifo vya wanaume baada ya kukimbiwa na wenza wao,mfano Ivan na Hanad. Lakini pia wanawake kama x Mrs Mbasha,x wa boss Ruge kuwakimbia wenza wao. Ilizoeleka wanaume wakiacha lakini si kuachwa. Maana hawa wanawake wameumbwa kuwa wasaidizi wa wanaume kwa mujibu wa biblia kitabu cha kwanza,sura ya kwanza Mungu akasema :"si vema mwanaume awe peke yake,nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye".
Je wanaume wameshindwa kusimama katika nafasi zao za kuongoza hali wakisaidiwa na wanawake,kiasi cha wanawake kuona hata bila wanaume hao hakuna tatizo?zingatia single parent wa kike ni wengi na wanalea watoto bila shida kuliko idadi ya wasingle baba wanaolea watoto.
Wababa tumeshindwa?
Karbuni.
Mtoto huwa ni mali ya mama yake
 
Pamoja na mapungufu yetu,ww kama mwanaume umechukua hatua gani??halafu si wanawake wenye mapungufu hata nyie mnayo mengiiiii mno hakuna kiumbe kikamilifu chini ya jua iwe me/ke wote ni wakosefu tuu tumejawa na ubatili na kujilisha upepo,..

Muhimu kila kiumbe asimame kwenye mipaka yake na nafasi yake,mwanamke afanye wajibu wake na mwanaume vivo hivyo.
Kwa hiyo gurudumu limezungushwa na mwanamke kachukua fursa?
 
Wanawake wasome maandiko matakatifu

Mwanamke n mtu anaweze kudanganyika haraka sana
Ndo maana Mapepo huwakumba wao

Mwanawake wanamapungufu kiasi furani.... ila uzuri maisha yanaendelea hakuna shida
Hakuna shida vipi mkuu wakati tunakufa? tufanyeje?
 
Ndiooo wanaume baadhi mmeshindwa kusimamia nafasi zenu,mnapenda dezo na uyoriyori mwingi Mungu amewapa mamlaka na nguvu ila mnamuangusha sana....kuweni kama Habakuki 2:1 "SIMAMENI KWENYE ZAMU NA NAFASI ZENU".
Nani kakuita huku, haya ni majadiliano ya wanaume.
Si unaona msivyo jua mipaka yenu
 
Zamani swala la Ndoa ilikuwa ni Mchakato ambao unahusisha Majadiliano na viapo mbali mbali hivyo hata Wanandoa matarajio yao hayakuwa tofauti sana na mchakato uliopitiwa..,
Hv ss swala la Ndoa limekuwa ni rahisi kuliko hata rahisi yenyewe na Matarajio ya Wanandoa yamekuwa ni makubwa kuliko uhalisia wenyewe at last divorce ndo imekuwa suluhisho!!!
Je ni nani amerahisisha?au tumeshindwa kukidhi makusudi ya kuwa kichwa na sasa ni mikia.
 
Mimi tuliachana kwa sababu nilimpa offer siku moja ya yeye kuwa juu wakati wa mechi basi ndiyo akawa kila siku anataka yeye awe juu kama vile yeye ndiye kanioa, basi tukashindwana
 
Hukujua kosa la Esau kwa Yakobo,uliuza nafasi yako.Usimlaumu kwa kumuonjesha utamu wa juu ukitarajia atarudi chini.
 
Tangu kuumbwa kwa dunia tabia ya mwanamke haijawai kubadilika tena now day wamekua na tabia mbaya iliyoboreshwa na usasa!!
Ata yule unaemuita wife material ukijipindua hua tofauti sana.
TUISHI NAO KWA AKILI AMNA NAMNA
 
Haijawahi kubadilika na haikukusudiwa ibadilike. Je sisi tumebadilika?hilo haliwezi kuwa chanzo cha tatizo mkuu?
 
Je ni nani amerahisisha?au tumeshindwa kukidhi makusudi ya kuwa kichwa na sasa ni mikia.
Hakuna alieharamisha, Msingi wa tatizo ni kuacha tamaduni zetu na kuiga tamaduni za nchi zilizoendelea kwa kisingizio cha Utandawazi matokeo yake ndo hayo Dogo bado anasoma anakuja na Kademu home anakatambulisha kwa Wazazi kuwa huyu ni Girlfriend wangu na Watu wanakenua Meno, na ukifuata tamaduni unaonekana ndo Mshamba wa mwisho!
 
Samahani kiongozi,nitauliza tena!hapo nyumbani dogo anapoleta gf wake panaitwa kwa nani?kama ni kwa bwana fulani huo udhaifu ni wa nani. Bado naona wanaume tunahitaji kukaza. Hata huyo dogo anaitwa kwa jina la baba yake.eg lamerk mussa.
 
Back
Top Bottom