Wanaume tusiwe hivi

kwetumasoko

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2016
Posts
866
Reaction score
518
Wakuu,

Habarini!

Leo katika mtaa fulani, nimeshuhudia mwanamke mmoja akipigwa kwa ngumi na mateke na mwanaume mmoja. Baada ya kusogea karibu nijue tatizo nini kumbe walikuwa ni wana ndoa, vijana waliokuwepo maeneo yale ikabidi wamkamate yule mwanaume na kumpa kisago kama mwizi.

Yule jamaa baada ya kupewa kisago kitakatifu, akaanza kujitetea kwamba ni mke wake, vijana wakamwambia kama ni mkeo kwa nini uje kumdhalilisha huku mtaani badala ya kumalizana nyumbani, hivi ninavyoongea huyo kijana kapakizwa kwenye toroli anapelekwa kituo cha Polisi, maana hawezi kutembea kabisa na waliompa kisago wamesepa, pia na mkewe nae katokomea kusikojulikana.

Wanaume, kama tuna mifarakano katika ndoa ni bora kuzikontroo hasira zetu, na ikiwezekana tuyamalize nyumbani na sio kuwapa faida wengine mitaani.
 
Kwa jinsi wanawake walivyo na kero nyingi ni nadra kumpata mwanaume anayeweza 'kujikontroli'. Umemwonya kitu mara mbili yeye anarudia tu kukifanya, kisago lazima akipate popote pale.

Kuna wanawake wana maudhi aisee we acha tu!Am talking from personal experience.
 
Nimefurahi sana sana, wangemvuta na "ndeke" zake hahahahaha
 
HUyo jamaa watakuwa walimuolea.Hivi ukimpga ndo solution la tatzo?
 
Awamu ya tano hii minyukano itakua mingi
pesa imekimbia wanasema
 

Umenikumbusha mwaka 2010 mtaa wa ohio dar es salaam..mida ya 11 jioni Nikamuona mwanaume mmoja almost kama 42 yrs akiwa anampiga makofi na mateke mwanamke mbele za watu mpaka akawa anavuja damu hakuna mtu aliyetokea kuwaamua, yule mwanaume alionekana amejazia Bausa. Baadae akachukua taksi na na kumwingiza yule mwanamke ndani kwa nguvu. Taksi ikaondoka mwendo kasi kupitia alihasani Mwinyi road

Kile kitendo kiliniumiza sana, katika maisha yangu nachukia uonevu na udhalilishaji. Kijana nikajitosa kichwa kichwa nami nikachukua taksi nikawa nyuma yao kama gari 3 hivi. Tulivyofika palm beach hotel kukawa na foleni kubwa nikashuka nikakimbia kwa miguu mpaka salenda police station nikaripoti tukio. nikapewa askari polisi 2 wenye silaha, ikawekwa road block pale salender, ile gari ilipofika ikaelekezwa iingie polisi station.

Wote wakachukuliwa nikiwepo na mimi, kumbe walikuwa mtu na mkewe! polisi wakaajitolea kumpeleka yule dada hospital akafungwa majeraha. Wakati huo yule bwana na mie tuko chini ya ulinzi..Yule dada amerudi almost saa 2 usiku, bwana akafunguliwa file la udhalilishaji, kupigana hadharani na kusababisha majeraha

Mashtaka yule mume anamshutumu mkewe ni malaya, kesi ikanigeukia mimi mume ananishutumu mie ni bwana wa yule mkewe, ukweli sikuwa nawafahamu hata kidogo. Huwezi amini niliwekwa lockup mpaka saa 8 usk, wakaja kudhaminiwa na ndugu zao wakaachiwa wote mie nikabaki lockup kumbe yule dada hakuondoka pale kituoni akarudi akanidhamini nikaachawa,dada akanikodishia taksi akanisindikiza mpaka getho kwangu ilala..

Kesho yake nikaripoti polisi baadae wakadrop ile kesi nikawa huru. Yule dada akawa ananipigia simu kunishukuru mwishowe it become happy ending........(dhambi ya happy ending nimeshatubu na kuacha.)

Ila Wanaume tutambue kabisa pshychological kumpiga mwamke unajidhihrisha wazi kwamba uwezo wako wa kufikiria ni mdogo kupita kiasi mpaka unaamua kutumia nguvu.. Lets be a real MAN
 
wanaume wengine bure kabisa ambayo hayawahusu nyie ndo marefarii sasa hayo hayawapi hela, chakula, kodi za nyumba, matibabu, ada za shule, luku na mengineyo embu yaacheni ya watu msipende umbeya haunaga mshahara. Unataka utoe msaada baada ya siku watu wamerudiana achaneni na ya watu
 
alimnyia jamaa papuchi mwezi mzima na mchizi kastukia wife wake ana mchepuko unamgegeda daily
 
Lakini mkuu ni bora ukavumilia kuliko kulianzisha mtaani, kwanza unajidhalilisha wewe na mkeo, vile vile ni unyanyasaji wa kijinsia
 
ndo maana nasema kumpga mwanamke siyo solution hatakama anachepuka unatakiwa kujua chazo maana naye ana akili na maamuzi hategemei akili za mwanaume.
nikweli kabisa... halaf pia amna mtu ambae hakosei na kwa mtu timamu akirekebishwa anaelewa....sio kwenda kudhalilishana mtaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…