Wanaume tupo bei juu? Au maisha yametupiga au wanawake mapepe?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,680
8,867
Naomba kujua maana nimekuwa nikiona mwanaume ukiwa katika mahusiano basi uliyenaye anataka kuolewa ukiingia social media watu wanatafuta waume tuu saa chakuni shangazi, je ni sisi tumekuwa wa gharama au maisha yamekaba watu hawaoi au wanaume wamekosa imani kwa wadada hivyo kuwatelekeza?

Naomba kujua hilo.
 
kuna kipindi nilikuwa naona maisha yangu hayajakamilika kwa vile tu sina mume.
hata huku nilishaanzisha uzi kutafuta mume..
ila nikaja kufikiria maisha vizuri nikaona huu ni upuuzi kwanini nitafute mume? kwanini nikapotezea mbali hata wale jamaa walionitafuta nikawaomba radhi..nimekuja kujifunza maisha ni wewe mwenyewe tu uolewe usiolewe maisha yapo tu tena yaliyokamilika.
ni upuuzi mtupu mdada kutafuta mwanaume wa kukuoa mitandaoni au popote wewe ishi maisha yako tu kawaida
kama utaolewa itokee tu naturally isipotokea sawa tu .maisha yenyewe ya kupita haya na vyote tutaviacha
 
Back
Top Bottom