Wanaume: Tumeusiwa

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,440
Reaction score
38,437
C&P
______________________________
Wanaume wenzangu, tufanye kazi kwa bidii tutafute hela ili uzee wetu tuwe na uwezo wa kujitegemea. Hakikisha kwenye uzee wako una pesa zako mwenyewe za kukufanya usurvive.

Sahau kuhusu watoto, na mama yao kwamba watakutunza. Wewe ndiye stranger pekee kwenye hiyo familia unayoiita ya kwako. Hiyo nyumba ni ya huyo mwanamke na watoto wake. Not yours.!

Babu yangu aliniambia kwamba mwanaume aliyeoa ni sawa tingatinga, ambalo linatengeneza barabara, lakini ikishakamilika linabebwa juu juu kwenye lori na kuondolewa, eti likitembea litaharibu barabara. Yani barabara ambayo tingatinga lenyewe limeitengeneza haliruhusiwi kutembea juu yake.

Vivyo hivyo kwa mwanaume aliyeoa. Atajinyima, atajishughulisha, atajizuia kufanya anasa, atakopa, atavaa mitumba ili tu watoto wake waishi vizuri, wale vizuri na kusoma shule nzuri. Siku hizi urithi pekee uliobaki ni elimu bora coz mashamba ziliishaga. Lakini pamoja na yote hayo, bado ukizeeka hao watoto sio wako, ni wa mama yao. Wewe watakuita "kamzee".

Watoto wakiwa na umri wa miaka 10 ndipo mama yao anaanza kuwajaza taarifa zisizovutia kuhusu wewe. Kadri wanavyokuwa ndivyo wanavyoelezwa mambo mengi. Wakifika utu uzima atawaambia "isingekua mimi hamgesoma, yeye alikua ni pombe tu na wanawake" Ukisikia hivyo ujue tingatinga limemaliza kazi yake sasa linakaribia kuondolewa barabarani.

Watoto wanapoanza kazi, mzee anakua amestaafu. Wanapokuja kutembelea wazazi, wakiondoka wanampa baba elfu 5 mbele ya mama. Halafu wanaenda jikoni na mama, wanampa hela kwa siri bila mzee kujua. Wakiondoka mama anamfuata mzee na kumwambia sukari imeisha. So ni suala la mzee kuamua kutoa ile elfu 5 aliyoachiwa na watoto ikanunue sukari, otherwise anywe chai isiyo na sukari. Hii ni moja ya sababu inayowafanya wazee kufa mapema baada ya kustaafu na kuacha wake zao wajane.

Nimeshuhudia wazazi wenye watoto ng'ambo wakimchukua mama yao akaenjoy life majuu, na kumuacha baba yao nyumbani akilisha ng'ombe zao mbili, na kutafuta chakula cha kuku.!

Wanaume work hard and save something for yourself at old age. Tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka dont expect too much from them. Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani. Kama huna hela utaumwa hata na mbwa yako mwenyewe.......!
 
Watoto wasiporubuniwa na mama/baba zao, basi mke/ mume anamteka akili awasahau/asiwape kipa umbele wazazi
 
Ataanza kuwajaza taarifa zisizovutia endapo kweli alikuwa anafanya hivyo.

Ila kwa baba ambaye alikuwa ana mapenzi kwa mke na watoto wake naamini uzeeni hawezi kupata shida.
 
Wanaume mnasahau kuwa vitu mnavyoona ni kazi ya kina mama ndiyo hujenga ukaribu wa mama na mtoto.

Jiulize baba ni lini ulikula chakula na wanao na kuona Victor alivyo mvivu wa kula?
Ni lini mara ya mwisho uliwavalisha pyajama na kugundua pyajama za James zimekuwa ndogo anahitaji mpya
Ni lini ulienda kumuona mwalimu wa Ashura na alikueleza hesabu zinavyomsumbua?

Wakina mama tunapambana na vyote hivi ndiyo maana hata uzeeni watoto wanaamini nikimpa mama hela itanunulia chakula lakini ukimpata baba itaishia bar
 

Hizo pajama mwisho wa siku nani ananunua.
Huko shule mwisho wa siku nani analipa ada..
Nyumbani hiyo lishe bora inayowapa watoto akili inatoka wapi?? Hiyo nyumba mnayoishi ni nguvu za nani.??.. Watoto wanenjoy maisha w'ends kwa fedha ya nani, nyumbani dstv na katuni vinatoka wapi?? Watoto wakiumwa hospital nani anagharamia??

Hayo yoote mwanaume anaonekana nothing..
Duh Dada Mungu anakuona..
 
Mkuu watoto Hawa kumuona wewe una jenga nyumba ila wamemuona mama anasonga ugali
Hawa kukuona wewe unalipa ada lakini walimuona Mama kwenye parent evening.
Hawa kukuona wewe ulivyonunua pyajama ila walimuona mama akirudishia vifungo.
 
Habari hii haina ukweli wowote na mifano ipo mingi tu kwa mfano mzee kingunge, Mwinyi, mkapa, wasirra, JK, n.k. nimetoa mifano ya watu maarufu ili usibishe wapo usiowajua kama mchambawima, mwakivuzi, n.k
 
Hayo ni mawazo ya baba asiejiamini, anajijua kabisa njia zake zilikuwa mbovu na ashaharibu. Kama alikuwa baba na mume kweli asingekuwa na mawazo hayo.
 
Huu uzi nimeongeza ktu, watoto wengi kama sio wote ukimuulza mama na baba, watakuambia mama ata mm mwenyew so mama ananafas kubwa kutake advantage ya kukutesa uzeen kama akiamua
Wababa show love kwa familia at the same time save money on ur own
 
Tena ukute baba alifanya maroroso na watoto walishuhudia alivyowatesa wao na mama yao!!
 
Tena ukute baba alifanya maroroso na watoto walishuhudia alivyowatesa wao na mama yao!!
Kabisa na ile nyumba ndogo wanaifahamu na kwa uchungu walimsikia mama anavyolalamika baada ya nyumba ndogo kutamba alinunuliwa kiwanja
 
Mkuu watoto Hawa kumuona wewe una jenga nyumba ila wamemuona mama anasonga ugali
Hawa kuku Ona wewe unalipa ada lakini walimuona Mama kwenye parent evening.
Hawa kuku Ona wewe ulivyonunua pyajama ila walimuona mama akirudishia vifungo.

Ndio maana mwisho wa siku tunasema huwa mnawajaza chuki watoto, unasonga ugali kwa hela ya unga na mboga aliyoleta baba halafu huwaambii watoto ukweli kwamba baba ndio engineer wa kila kitu..unawavalisha watoto pajama
bila kuwaambia nani kanunua pajama unafikiri kama watoto ni watajifunza nini maana ya uanamume au kuwa baba???

Kwa point yako ina maana wale walioenda Kwa RC Makonda wameenda kufanya nini sasa, if they can sort out and daddy is nothing?

Binafsi wanangu wanajua baba kaenda kazini kutafuta hela ili tule Good time, na nikiwaaga nawaaga hivyo hata kama niko kwenye starehe zangu.. Watoto nyumbani lazima wafundishwe who is baba..mama ukienda tofauti na hapo unatengeneza future mbovu kwa watoto..
 
Mkuu watoto Hawa kumuona wewe una jenga nyumba ila wamemuona mama anasonga ugali
Hawa kukuona wewe unalipa ada lakini walimuona Mama kwenye parent evening.
Hawa kukuona wewe ulivyonunua pyajama ila walimuona mama akirudishia vifungo.
Huo ni ukweli Sky Eclat , ila una wajibu wa kuwajulisha /kuwafahamisha hao watoto ushiriki wa baba yao kwa hayo wanayoona wanapata toka kwako
 
Huo ni ukweli Sky Eclat , ila una wajibu wa kuwajulisha /kuwafahamisha hao watoto ushiriki wa baba yao kwa hayo wanayoona wanapata toka kwako
Ni muhimu wakuone siku mojamoja unawaogesha na kufanya nao homework. Uwafahamishe pia usipokuwepo nyumbani unakuwa kazini.

Zile presentations zinazokufanya usiende kwenye parent day hakuna atakaezikumbuka ukistaafu lakini mtoto atakua na sura yako kwenye parent evening kichwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…