Hapana hapa unalea tatizo kwa makusudi au bila kujua, tafuta njia nyingine ya kuwasiliana na mwanao
Nimelisha anzisha jaribu kuwa nawatuma wadogo zangu kwenda kumuona mtoto na hata kumchukua, akawa analalamika kwa watu mimi siendi kumuona mtoto wala sipigi sim, pia walikua wanawatreat vibaya sana wadogo zangu wakienda pale, yaani kuna wakati nilibadili line hadi nikahisi kuchanganyikiwa.
Nawaza pia hilo, japo sioni njia rahisi kwa kweli
Muachie huyo mtoto endelea na maisha yako, mtoto akikua atakutafuta tu.
Kumfuatilia ndio kunampa kichwa cha kukutukana.
Ukikaa kimya atarudi kwenye sense zake.
Unajua hua sipendi hata kumpigia hata hivyo hua simpigii hadi niwe namuhita mtoto, kwa hiyo inaweza kupita hata wiki 3 mimi sijui mwanangu anaendeleaje, Lakini pia inanilazimu kumfuatilia maana ni mtoto wa kike n kuna mambo nikiyafikiria huwa nakosa amani kabisa.
mfano, kunasiku nilimuuliza mtoto nani anakusafisha ukienda chooni?? mtoto akanijibu anasafishwa na kaka wa ng'ombe(mfanyakazi wa ng'ombe) nikampigia nikamwambia kwanini mtoto anasafishwa na kaka wa ng'ombe?? hakuonyesha kujali hata kidogo, aliona ni kawaida tu, lakini mimi nilishamfundisha mwanangu kujitegemea kwa kila kitu, sasa sijui ilikuwaje hadi kumruhusu kaka wa ng'ombe kumsafisha mtoto wa kike.
Zaidi wakati mwingine wanaruhusu mtoto wa kike eti alale na baba ake mdogo mwenye umri wa miaka kama 23 au 24 jamani hebu niambieni kweli hawa watu wanaakili kweli???????
Kwakweli moyo wangu una maumivu sana nikifikiria hayo na nipo kwenye mkakati wakuomba nimchukue na niondoke nae mbali kabisa.