mkada
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 1,200
- 908
Hii imetokea leo mlimani city eneo ilipo bank ya nmb, ambapo jamaa mmoja mtanashati alipogongana uso kwa uso na njemba moja iliyokuwa imeongozana na mke wake sijui yule. Yule mdada alikuwa amemwacha jamaa yake kama pace chache nyuma, na baada ya kupishana na jamaa huyu mtanashati,jamaa aligeuka nyumba kumwangalia yule dada ndipo alipogongana na jamaa,ambapo njemba ilimaind sana coz ilijua sababu ni yule jamaa kugeuka na kumwangalia demu wake.Usuluhishi wa chapchap ulifanyika ambapo yule jamaa mtanashati alitokea kwenye vyoo vya mlimani city huku demu akirudi na kujaribu kumkanda na leso njemba wake ambaye alionekana kuumia usoni.........Jamani wanaume tubadilike ,hii tabia ni mbaya sana,mi mwenyewe nilikuwaga nayo ila nimeacha....ukishindwa kabsa kuvumilia basi kabla ya kupishana na mwanamke,simama kwa pozi,tafuta kasababu halafu geukia uelekeao anaoenda mwanadada then piga picha haraka haraka na zisave kwenye memory yako zikakusaidie kama huwa zinawasaidia.