"WANAUME TAFUTENI HELA”

"WANAUME TAFUTENI HELA”

Namshakende

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
884
Reaction score
2,333
Wakuu, habari za muda huu.

Leo asubuhi nimepokea ujumbe kutoka kwa mwanamke mmoja akiniambia hapendi mwanaume bahili kama mimi na kwamba ninapaswa kutafuta pesa. Ujumbe huo umenifanya nitafakari kuhusu kauli maarufu ya “Wanaume tafuteni hela.”
28395.png


Ni kweli mwanaume anapaswa kujituma, kujitegemea na kuwajibika. Lakini je, kila mwanaume ambaye bado hajafanikiwa kiuchumi ni mvivu au hajitumi?

Wapo wanaume wanaobeba zege, magunia, kuchimba mifereji na kufanya kazi ngumu kila siku, lakini bado kipato chao hakitoshelezi. Je, tunapaswa kuhoji juhudi zao au kutambua kuwa fursa na mazingira ya kiuchumi havifanani?

Pia, kuna tofauti kati ya kutokuwa na fedha na kuwa bahili. Mtu anawezaje kutoa kile ambacho hana?

Kwa upande mwingine, mwanamke ana haki ya kutamani mwenza mwenye uwezo wa kifedha. Lakini je, haki hiyo inaambatana na wajibu gani katika kujenga maisha ya pamoja?

Umaskini si ushahidi wa uvivu, kama ambavyo utajiri si ushahidi wa uwajibikaji.

Swali si kama mwanaume anapaswa kutafuta hela; bila shaka anapaswa kujituma. Swali ni je, mahusiano ni ushirikiano wa watu wawili katika kujenga maisha au ni jukumu la mwanaume kumfadhili mwanamke?

Na kama mwanaume mwenye uwezo wa kifedha akipoteza mali zake kesho, je, thamani yake kama mwenza nayo inapotea?

Tunatafuta wenza wa maisha au wadhamini wa maisha yetu?
 
Mchepuko au malaya au msimbe asiwe kipimo chako cha kuonyesha kuwa unatafuta hela au hautafuti...

Mke wako, watoto wako na wazazi wako ndo wanaotakiwa kuwa kipimo cha uwezo wako wa utafutaji pesa...siyo msimbe na malaya ambaye babake mwenyewe hakuwahi kumiliki hata mdenge wa baiskeli.
 
Wakuu, habari za muda huu.

Leo asubuhi nimepokea ujumbe kutoka kwa mwanamke mmoja akiniambia hapendi mwanaume bahili kama mimi na kwamba ninapaswa kutafuta pesa. Ujumbe huo umenifanya nitafakari kuhusu kauli maarufu ya “Wanaume tafuteni hela.”
View attachment 3715135

Ni kweli mwanaume anapaswa kujituma, kujitegemea na kuwajibika. Lakini je, kila mwanaume ambaye bado hajafanikiwa kiuchumi ni mvivu au hajitumi?

Wapo wanaume wanaobeba zege, magunia, kuchimba mifereji na kufanya kazi ngumu kila siku, lakini bado kipato chao hakitoshelezi. Je, tunapaswa kuhoji juhudi zao au kutambua kuwa fursa na mazingira ya kiuchumi havifanani?

Pia, kuna tofauti kati ya kutokuwa na fedha na kuwa bahili. Mtu anawezaje kutoa kile ambacho hana?

Kwa upande mwingine, mwanamke ana haki ya kutamani mwenza mwenye uwezo wa kifedha. Lakini je, haki hiyo inaambatana na wajibu gani katika kujenga maisha ya pamoja?

Umaskini si ushahidi wa uvivu, kama ambavyo utajiri si ushahidi wa uwajibikaji.

Swali si kama mwanaume anapaswa kutafuta hela; bila shaka anapaswa kujituma. Swali ni je, mahusiano ni ushirikiano wa watu wawili katika kujenga maisha au ni jukumu la mwanaume kumfadhili mwanamke?

Na kama mwanaume mwenye uwezo wa kifedha akipoteza mali zake kesho, je, thamani yake kama mwenza nayo inapotea?

Tunatafuta wenza wa maisha au wadhamini wa maisha yetu?
ulaaniwe na kila kitu
 
Utafule hela ili umpe?

Yeye pesa zake anazotafuta anazifanyia nini ? Au yeye hatafuti pesa? Au pesa zake anasubiri azitafutie kwako baada ya wewe kutafuta??
 
Kuwa na hela na ubahili ni vitu viwili tofauti....
Sijazipata nyingi ila hata hiki kidogo tu nakionea ubahili kuhomg hovyo, nakupa pesa kwa sababu ipi? Kiukweli mie sitoi hela kichizi chizi na kwingine sitoi kabisaaaa, ye ana papa na mimi nina ukuni, kama kwenye maisha ya kawaida hatusaidiani usitegemee mie nikupe hela yangu, njoo tutatumia pamoja tutagegedana kila mtu ashike lake, nikikumisi nitakutafuta, ukinimisi karibu.
 
Back
Top Bottom