Wanaume ndo tulivyo??

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2007
Posts
2,257
Reaction score
373
For the last few weeks nimekua nikiangalia documentary programs za wanyama kwenye channel ya Animal Planet na pia nimekua ni mpenzi mkubwa sana wa program ya 'Africa' inayoonyeshwa sasa hivi BBC kuhusu wanyama pia. Nimeona kuna similarities nyingi kati yetu na wanyama wengi jinsi ambavyo wanaume tuna behave kwenye society.

Wanyama kama simba au twiga kwa mfano, utakuta dume moja linaishi na majike wengi na lina himaya yake ambayo kama dume jingine likiingia tu kwenye hiyo himaya ni lazima pachimbike kwa jinsi ambavyo watapigana. Cha kufurahisha ni kwamba majike mengi yako happy kumilikiwa na dume moja while its almost impossible kwa madume mawili au zaidi kukubali kushare jike moja. Nime relate hali hiyo na hali halisi ya maisha yetu wanadamu, kuna wanawake wengi wanaokubali kuolewa kwenye ndoa ya mke zaidi ya mmoja na wengine huishi katika nyumba moja au same compound wakiwa na furaha kabisa! Wote tunajua wanaume hata siku moja tusingeweza kukubali kushare mwanamke hata kama ingekua inaruhusiwa! Ni rahisi sana kwa mwanamke kumsamehe mwenzie hata kama amemfumania live akila mzigo, mwanaume akifumania- 9 out 10 ujue uhusiano umekwisha! Kwanini wanaume hatuwezi kucope na 'sharing' kwenye mapenzi?

Its common kwa wanaume wengi kuwa na mademu zaidi ya mmoja na kutotaka 'kusaidiwa' kabisa na wanaume wengine. Sasa kina dada mnaotulaumu kuwa sisi wanaume hatujatulia, sijui malaya, etc how do you explain these behaviours za wanyama? Mkumbuke pia kuwa binadamu tu wanyama.
 
I'd say yes.

Yes because we are wired that way.

We like to conquer. Most of us have enormous egos.

It's the testosterone in us that makes us more aggressive and more territorial.

Simply put, that's just the way we are and that's why we are men and they are women.
 
Mkuu Kana-Ka-Nsungu to some extent uyasemayo yana ukweli. Wanyama ndivyo wanavyoishi in their societies na mwanamke haswa Simba anapenda kuzaa na dume lenye nguvu ili ku protect familia. Kwetu binadamu demu anaona fahari kutoka na mume wa mtu mwenye pesa ili akidhi mahitaji yake. Societies za viumbe vya mwenyezi Mungu ndivyo tulivyo, mwanamme ndiyo mmiliki na mwamuzi wa karibia vitu vingi. Kwa hali ya kawaida, hakuna mwanamke anayependa kuwa nyumba ndogo, kila mmoja anataka kuwa na mji wake. Kina mama wengi wanaokubali hii hali ni kwa sababu hawana jinsi na ufukara ni chanzo kikubwa. Mkuu, ngoja nikuulize wewe. Japo wewe mwenyewe si Simba au mnyama wa porini, mara ngapi unawaza kuchapa mademu zaidi ya ulie naye hivi sasa?
 
Last edited by a moderator:
First of all nakataa.. Not all of men wana demu zaidi ya mmoja ama mke zaidi ya mmoja.. Mimi kama mimi binafsi sina demu..... Huwa najiuliza demu wa nini??
1.Demu atanipotezea tu muda wangu..
2. Gharama za matumizi zitakuwa kubwa(out, kufannya uzinifu,kumsaidia yeye anapohitaji msaada).
3.Kuumizana nafc mwisho wa siku.mambo ya demu na bwana huwa mara nyingi hayadumu, Moja ya kitu kimoja wapo kwa gal cha thamani ni ile sehemu ya kati! Sasa kama ukishanipa kuna umuhimu gani tena wa kukuoa??? Ndo maana wanawake wengi siku hz wanaishia kuwa malaya(japokuwa siyo wa kuuza) but wakutumika na kuachwa!!!!
Girls out there amkeni.. Tambueni thamani yenu.. Think b4 u act.. Not just anyone can come and touch

4.Dini kama dini hairuhusu uzinifu.. So muamini mungu wako ili ufanikiwe.. Duniani hapa tunapita

5.Magonjwa kibao yanayosambazwa na kujamiana.. Google and see the hiv rate in Tz..

Uzungu unatuharibu saikolojia.. Watu siku hz wanaona uzinifu ni kawaida..
 
Uzungu unatuharibu saikolojia.. Watu siku hz wanaona uzinifu ni kawaida..

Hold on right there....uzinifu na uzungu vinahusianaje?

Manake kwa kadri nijuavyo mimi uzinifu upo tokea enzi na enzi na upo kwenye jamii zote.

Sasa ina maana unataka kulaumu uzungu kwa kuleta uzinifu?:confused2:
 
Nyani, unataka sema jamii haijaharibika kupitia hawa watu?
1. Je zamani watu walikuwa wakivaa nguo fupi?
2.Je zamani watu walikuwa wakipigana picha za uchi?...
3. Television siku hz zinazingatia maadili wakati zinarusha vipindi kama vile zamani? Lets say wakionyesha movie kuficha sehemu za vitendo vya ngono!!

Sasa huoni kama hizi ni sababu mojawapo zinazochochea zinaa? Na kuondoka ni taabu kwa sababu visababishi vya zinaa vina achwa!!!
 

Umegusia suala lla uchumi hapo juu kuhalalisha wanawake kukubali kujiingiza kwenye ndoa za wake wengi pia kuna wanaume ambao hali zao sio nzuri kiuchumi na hata siku moja hawatakubali kuwekwa nyumba moja na mwanamke mwenye pesa! hata kama hawaishi nyumba moja au karibu, siku wakijuana- wanazipiga au wanaacha mzigo.

Matamanio ninayo sio siri and i guess wanaume wengi wanayo coz kila demu unayemuona ni mzuri kuliko mwingine! Nawaonea sana wivu wanyama wenzetu wa mwituni kwa freedom waliyo nayo, dume moja majike kumi afu jamaa anakula mzigo mbele ya wengine wote, hamna noma wala nini!
 

NN kwa lugha yako nyepesi unamaanisha " mianaume ndivyo tulivyo!."
 
Nyani, unataka sema jamii haijaharibika kupitia hawa watu?

Hapana. Tusitake kutupia lawama wengine bana.

1. Je zamani watu walikuwa wakivaa nguo fupi?

Zamani ipi? Manake kuna kipindi watu hata walikuwa hawavai nguo. Ilikuwa ni mwendo mdundo tu ndani ya birthday suit. Sasa kipi bora - mtu kutupia nguo fupi au kutupia suti ya kuzaliwa?

2.Je zamani watu walikuwa wakipigana picha za uchi?...

Kulikuwa hakuna haja. Vitu vyote vilikuwa laivu bila chenga wala ukungu.

3. Television siku hz zinazingatia maadili wakati zinarusha vipindi kama vile zamani? Lets say wakionyesha movie kuficha sehemu za vitendo vya ngono!!

Kwani kuna wakati zilikuwa zikionyesha explicit sex scenes?

Sasa huoni kama hizi ni sababu mojawapo zinazochochea zinaa? Na kuondoka ni taabu kwa sababu visababishi vya zinaa vina achwa!!!

Zinaa ilikuwepo, ipo, na itakuwepo na haiwezi kuondoka unless bailojia zetu zibadilike.
 
Ndio maana binadamu tumekuwa tofauti na wanyama kwa kupewa utashi na kufikiri . Usifananishe maamuzi ya wanyama na ya binadamu kwa kuhalalisha umalaya. Wanyama hawaoi, wanajamiiana kwa kuendeleza kizazi.

Malaya=kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu zaidi ya mmoja.
 
Ndio maana binadamu tumekuwa tofauti na wanyama

Hata binadamu ni wanyama pia. Soma bailojia.

kwa kupewa utashi na kufikiri.

Una uhakika wanyama wasio binadamu hawana utashi na uwezo wa kufikiri?

Usifananishe maamuzi ya wanyama na ya binadamu kwa kuhalalisha umalaya. Wanyama hawaoi, wanajamiiana kwa kuendeleza kizazi.

Umejuaje kwamba wanyama wasio binadamu hawaoi? Umewahi kuwa mnyama asiye binadamu?
 
Hata binadamu ni wanyama pia. Soma bailojia.

Hilo lipo wazi, maisha ya binadamu na wanyama wengine nitofauti, niambie kama wanyama najisitiri kwa mavazi, wanaenda shule, n.k kama huwezi tofautisha maisha ya binadamu na wanyama wengine ni afadhali yangu nisiyejua biology.



Una uhakika wanyama wasio binadamu hawana utashi na uwezo wa kufikiri?

Kiwango cha kufikiri/utashi wa wanyama uko tofauti kwa kiwango kikubwa sana, ndio maana ukiwa unafanya mambo yasiyo ya kawaida watu wanakwambia mbona unakuwa kama mnyama?



Umejuaje kwamba wanyama wasio binadamu hawaoi? Umewahi kuwa mnyama asiye binadamu?

Mimi ni binadamu, kama wanaoa sijafanya utafiti, nnachojua na nnachokiona kwa wanyama hakuna suala la dume moja kukaa na jike moja kama binadamu wanavyoishi mme na mke.

Kwa hiyo hii yote ni kuhalalisha wanaume kuwa na wanawake wengi kama wanyama wengine au ni nini?
 
Hata binadamu ni wanyama pia. Soma bailojia.



Una uhakika wanyama wasio binadamu hawana utashi na uwezo wa kufikiri?



Umejuaje kwamba wanyama wasio binadamu hawaoi? Umewahi kuwa mnyama asiye binadamu?
Hebu kaangalie Pro-Bowl kijana, maswali yako ni magumu sana!.
 

Wanyama nao wana akili ya kufikiri ndo maana huoni simba dume akimpanda simba dume mwenzie na akiona dume lingine limeingia kwenye empire yake anaswitch kwenye attack mode. Another very interesting thing, simba dume akimkuta jike na watoto anawaua na kuzaa wake! Ubongo wa dume unachemka hapo..

Unaposema 'wanyama hawaoi, wanajamiiana kwa kuendeleza kizazi.." Mbona hata kwa binadamu hii imekua ni kawaida siku hizi? Watu wangapi unaowafahamu wewe wameamua kuzaa tu na hawajaoana? Kwani binadamu ukitaka kuzaa lazima uwe kwenye ndoa?

Hiyo definition yako ya umalaya ni very offensive kwa ndugu zangu waislamu, usishangae kukiwa na maanndano makubwa sana siku ya ijumaa baada ya swala!!
 
Kwa kiasi tunafanana ila utofauti ni kwenye UTASHI, wanyama hawana ufahamu wa kung'amua kama ambao mwanadamu kajaaliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…