Wanaume nao hunyanyaswa kingono na Wanawake.

Culture Me

JF-Expert Member
May 24, 2017
10,447
21,160
Tumezoea kesi nyingi za wanawake wananyanyaswa kingono na wanaume, lakini tunafumbia macho upande wa pili wa shilingi, wanaume pia hunyanyaswa kingono na wanawake, cha kusikitisha wanaume hawasemi kwa kuhisi aibu, kuchekwa, kubezwa na hata kutokuaminiwa.

Kuna wengine hushikwa makalio na wanawake kisha wanawacheka,(sio mpenzi wake)

Kuna wengine hukonyezwa na wanawake,(sio mpenzi wake)

Kuna wengine huvutwa sehemu zao nyeti au kutomaswa na kuambiwa una uume mdogo au mkubwa au mfupi au mrefu kisha wanacheka,(sio mpenzi wake)

Kuna wengi wamelazimishwa kuwaingilia wanawake kingono kwa sharti kua wakikataa basi mwanamke atapiga kelele kua alitaka kumbaka,

Kuna wengine hulazimishwa kuwaingilia wanawake kinyume na maumbile na kama wakikataa basi hupigwa au kung'atwa au kuumizwa sehemu mbali mbali,

Kwa walio kwenye mahusiano kama mwanamke akimchoka basi humfanyia visa, humyima chakula, humpiga kwa kumrushia vitu vya kuumiza hata kumng'ata na matusi na kama mwanaume akijaribu kumgusa kidogo basi kesi imerudi kwake,

Share nasi kama umeshawahi kunyanyaswa kingono na Mwanamke au kunyanyaswa kihisia, kimwili na kiakili na Mwanamke.
Usione aibu.
 
wanaume wa dar mnaitwa huku................
Woman Judo Throws Man Knockout
 
Wapo wanawake wana sauti kwa wanaume zao Daaah kuna baba huku namuonea huruma
huyo baba ananyanyaswa kiakili, kihisia na pengine hata kimwili lakini hana pa kukimbilia, ingekua ni mwanamke ndio anafanyiwa hivyo hata majirani wangeshamshtaki.
 
Tumezoea kesi nyingi za wanawake wananyanyaswa kingono na wanaume, lakini tunafumbia macho upande wa pili wa shilingi, wanaume pia hunyanyaswa kingono na wanawake, cha kusikitisha wanaume hawasemi kwa kuhisi aibu, kuchekwa, kubezwa na hata kutokuaminiwa.

Kuna wengine hushikwa makalio na wanawake kisha wanawacheka,(sio mpenzi wake)

Kuna wengine hukonyezwa na wanawake,(sio mpenzi wake)

Kuna wengine huvutwa sehemu zao nyeti au kutomaswa na kuambiwa una uume mdogo au mkubwa au mfupi au mrefu kisha wanacheka,(sio mpenzi wake)

Kuna wengi wamelazimishwa kuwaingilia wanawake kingono kwa sharti kua wakikataa basi mwanamke atapiga kelele kua alitaka kumbaka,

Kuna wengine hulazimishwa kuwaingilia wanawake kinyume na maumbile na kama wakikataa basi hupigwa au kung'atwa au kuumizwa sehemu mbali mbali,

Kwa walio kwenye mahusiano kama mwanamke akimchoka basi humfanyia visa, humyima chakula, humpiga kwa kumrushia vitu vya kuumiza hata kumng'ata na matusi na kama mwanaume akijaribu kumgusa kidogo basi kesi imerudi kwake,

Share nasi kama umeshawahi kunyanyaswa kingono na Mwanamke au kunyanyaswa kihisia, kimwili na kiakili na Mwanamke.
Usione aibu.
hii labda kwa wanaojifanya wanaume walio kwenye kikundi chenu cha LGBTQ
 
Tunanyanyaswa sana, hasa kingono. Tunanyimwa unyumba wakati tunahitaji punani, hilo ni nyanyaso!!!
Ukiona unanyimwa ujue kuna sababu, amechoka, hafurahii au ana mawazo.

Zungumza na mwenzio.
 
Back
Top Bottom