Watu tumekuwa tukijinasibu 'ulokole' kwenye kadamnasi kwa ajili ya unafiki wetu.
Muanzisha mada, umekuwa kimaadili kwa kiwango gani cha kujitosheleza mwenyewe, hadi uanze kuhubiri na kuiona kavukavu kwako ni chukizo, uione ni ovyo, yaani kwako na nafsi yako ikiri kuwa ni mbaya?
Watu mmekuwa mkitengeneza pesa kwa ajili ya kujenga hofu kwenye saikolojia za watu na kuukwaa ukwasi na kuishi maisha ya kifahari!
Kwanini usielekeze mada yako kuishauri jamii kujiepusha na uchafu na kuishi katika mazingira ya usafi ili kuepuka magonjwa ya milipuko yanayoua zaidi kuliko ukimwi?
Bali unaendeleza yale yale ya kujikinga na maambukizi ambayo tayari kuna watu wa kada hiyo ya kuhamasisha.
Hayo mambo sijui ya kavukavu, sijui condom nk nk ni kuhofisha na kuchanganya watu tu!
Hivi ukimwi unavyofahamika kuliko hata wimbo wa taifa, kuna haja ya kukumbushana kuimba verse zake, kama siyo kuhadaa akili za watu kutaka chochote kitu?
Kavu kavu ndiyo kila kitu, tukiendekeza kuvaliana maputo kama unavyotaka kuogopesha watu, kuzaliana itakuwa ni hadithi na ni kwenda kinyume na maagizo ya mh. Rais ya kuzaliana bila mpango ili kuongeza idadi ya raia, ili mradi mtu uwe na uwezo wa kulisha.
Wacha kupotosha!