Wanaume na wanawake wanapolalamika....

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082






Ngoja niyadadavue malalamiko ya wanawake kwanza hapa chini:


1. Wanawake wanalalamika kwamba wanaume sio waelewa wazuri, yaani huwa wanatafsiri mambo tofauti na isivyo.


2. Wanalalamika kwamba wanaume huwa hawajali hisia za wapenzi wao wala hawajali pia kuhusu mahitaji yao.


3. Wanalalamika kwamba wanaume huwa hawajui kuonesha upendo , yaani hata wanapopenda inakuwa kama vile wanajisumbua tu, kiasi kwamba mwanamke anaweza kuhisi kwamba hapendwi.


4. Wanalalamika kwamba wanaume huwa hawana muda wa kucheza na wapenzi wao kabla hawajafanya nao mapenzi yaani hawawaandai kabla ya tendo, wao huwarukia tu na kumaliza haja zao haraka na kugeuka ukutani kabla ya wao (wanawake) hawajaridhika.


5. Wanalalamika kwamba wanaume hawana mawasiliano, huwa hawajui kueleza hisia zao na mawazo yao, bali ni watu wa kunyamaza na kujifungia kwenye dunia yao wenyewe. Wanahisi kama kuelezea hisia zao na mawazo yao ni kuwa dhaifu.


6. Wanawake hulalamika kwamba, wanaume hawana muda wa kukaa nyumbani na familia zao, kwa sehemu kubwa ni watu wa nje tu.


7. Wanawake pia wanawalaumu wanaume kwamba, hawajali mustakabali wa usafi au kupendeza kwa nyumba.


8. Wanawake wanawalalamika kwamba, wanaume huwa wanafanya maamuzi yao bila kujali kuwa wanawake wapo na wanaweza kuwa na michango mizuri sana kwa hicho wanachotaka kukifanya. Huamua kama kwamba wanawake siyo sehemu ya familia.


9. Wanalaumu kwamba, wanaume ndiyo wanaoanzisha au kuendekeza kutoka nje ya ndoa ukilinganisha na wao wanawake.






Malalamiko ya wanaume nayo nayadadavua kama ifuatavyo…..


1. Wanaume wanalalamika kwamba wanawake ni watu wa kulalamika, kukosoa na wenye vijineno vya hapa na pale visivyo na maana na vyenye kukera.


2. Wanaume wanalalamika kwamba wanawake wanajaribu sana kuwadhibiti na kuwakandamiza pale wanapoachiwa nafasi kidogo.


3. Wanaume wanadai kwamba wanawake huwa hawana furaha, mara nyingi wanaonekana kama vile wako kwenye simanzi fulani na wanapenda sana kununanuna hasa pale wanaume wanaposhindwa kuwatekelezea kile walichotaka hata kama hakina umuhimu kwa wakati ule.


4. Wanaume wanalalamika sana kwamba wanawake wanawanyima unyumba kama adhabu ya kuwakomoa. Siyo kuwakomoa tu, bali huwa wanafanya hivyo kwa lengo la kuwashurutisha wakubaliane na utashi wao fulani.


5. Lalamiko lingine la wanaume kuhusu wanawake ni lile la kwamba, huwa hawafikirii kwa mantiki, bali mara nyingi kufikiri kwao huwa kunakumbwa na mhemko. Kwa hiyo, uamuzi wao mwingi hauangalii mantiki bali hujali zaidi hisia zao.


6. Wanawake wanalalamikiwa na wanaume kwamba, hali zao za kihisia huwa hazitabiriki. Yaani huwa zinabadilika kufuatana na mabadiliko ya miili yao ya kihomoni miilini mwao nyakati kama zile za siku zao(hedhi), nyakati za ujauzito na hata wanapokoma kuziona siku zao(menopause) .


7. Wanaume wanawalalamikia wanawake kwa tabia yao ya umbea, kwamba midomo yao huwasha sana hadi waseme kile walichokiona au kukisikia hata kama si lazima na pengine ni hatari.


8. Wanawake wanalalamikiwa pia na wanaume kwamba, huwa wanatoka nje ya ndoa, hasa wanapohisi kukosewa upendo ndani, jambo ambalo haliwezi kuleta suluhu kwa tatizo hilo.


Kama wewe ni mwanaume na umegundua kwamba moja au baadhi ya malalamiko ya wanawake yanakugusa inabidi ubadilike na kufanya kinyume chake. Kama wewe ni mwanamke pia hali ni kama hiyo. Kama kweli una mdomo mwingi kwa mfano, ujue wanaume hawapendi tabia hiyo, hivyo huna budi kubadilika.
utambuzi na kujitambua
 
Kaka hiyo ngoma nzito sema inafundisha kitu kimoja kuwa binadamu awe ke au me wote wana mapungufu na ndiyo maana hawaishi kulalamika. Ndiyo maana watu wengi tunaona ajabu jinsi wanyama wanavyoishi kwa amani hata zaidi ya binadamu. Wanayama hawana ufisadi wala ulaghai bali kuonyesha ukweli wao. Sijawahi kuona simba akimla simba mwenzake. Hata fisi mwenye uchu hajawahi kumla fisi mwenzie. Lakini binadamu je? Wanachunana ngozi, wanauzana kwa wawekezaji, wanabaguana kwa rangi dini hata makabila. Hivyo kwa ufupi somo hapa ni kubwa na ukitaka kujua nisemacho mwangalie binadamu anapozaliwa-huzaliwa akilalamika. Na huwa haishi kulalamika hadi yamkute mauti. Who knows huenda hata huko roho ziendako hulalamika.
 
Hiyo no 4 ktk malalamiko ya wanaume tunaomba ifanyiwe kazi kwenye kitchen party, hizo nyingine tunaweza kuvumilia
 
Kweli umeleta funzo zuri sana na haya ndio malala miko ya pande mbili kila hiitwapo leo.

Naami wanandoa wakiishi kwa kujua hakuna malaika baini yao wawili bali ina hitajika kufunzana na kukosoana au kurekebishana nadhani inaweza ikawa suluhu ya malala miko!
Mfano lalamiko la kutoridhishana lina weza lika tatuliwa kama wote wawili wakivunja ukimya na kila mtu akamfundisha au kumuelekeza mwenzie jinsi anavyo weza kulizika na tendo au ni sehemu gani nikishikwa au vitu gani nikifanyiwa vina saidia kunifanya nilizike na tendo.

Nikunye na hapo pande zote mbili zimekuwa zikiongea pembeni tena kwa kuwaadithia watu wapembeni kuwa mwenza wangu haniridhishi mwisho wa siku ni kutoka nje ya ndoa!
 
Back
Top Bottom