JEKI
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 4,845
- 2,968
Jana nilikuwa najibu swali nililotupiwa na mpenzi wangu, alisema kama mwanaume akiamua kuchepuka basi anakuwa hamthamini mkewe, nikamwambia siyo,
Mwanaume anaweza akawa anampenda sana mkewe lakini akatoka nje, mwanaume kuchepuka si kuwa hamthamini mkewe, la hasha!.
Ili kumwelewesha ilibidi nimtolee mfano wa paka, maana tabia hiyo ya wanaume inafanana sana na tabia ya paka, ni hivi, paka hata awe ameshiba kiasi gani hawezi kumwacha panya anayekatisha mbele yake, lazima atamkimbiza tena kwa bidii utadhani ana njaa kweli, akimkamata basi atamchezea weee hadi afe na akifa asilani hawezi kuacha kumla kichwa, unakuta panya kaliwa kichwa tu unajiuliza kulikoni?
Hapo jua paka alikuwa kashiba ila kichwa hawezi kukiacha hata wawe panya kumi.
Hivyo ndo ilivyo kwa wanaume pia, hata kama anamthamini vipi mkewe bado havumilii kuona mwanamke anapita mbele yake.
Hivyo basi nitumie fursa hii kuwapa matumaini wanawake, kwamba mwanaume kuchepuka si kwamba hakupendi, la hasha bali ni haka ka tabia kama ka paka.