Wanaume muache kukashifu (kuponda) Wanawake

Joyboy

JF-Expert Member
Sep 16, 2023
1,360
3,400
Habari.

Nitaanza kwa kusema kwamba Mm sio mgeni humu JF, ni member wa muda mrefu kidogo nina kama miaka 6, sema nimepoteza account yangu, maybe imefutwa kwa sababu kuna kipindi nilikuwa less active, nimejaribu ku-log in imekataa.

Kilichonifanya nianzishe hii thread ni kukereka, sijajua labda nyie mmezoea ila tangu nirudi humu JF nimekuwa naona kuna thread nyingi sana zimeanzishwa na zinaendelea kuanzishwa zenye malengo ya kuponda wanawake na kutunaka wanawake....kwanini?

Hv ni asili yetu kweli sisi wanaume kuwa na mdomo mwingi kiasi hiki, kila siku kuanzisha thread za kulialia kuhusu wanawake, mambo mengine watu wanalalamika ni ya kijinga sana hadi unatafakari aliyeandika hv amewaza nn kichwan mwake.

Kwa siku unaweza kupishana na threads karibia saba za kulalamikia wanawake na ukakutana na threads kama mbili za kulalamikia wanaume, ni kitu cha kustaajabisha sana, yaan wanaume tumewazidi wanawake midomo na kulalamika.

Kama mwanamke unayempenda/mpenzi/mke wako amekutendea ndivyo sivyo deal nae kama mwanaume sio unaona kwamba hii ni fursa ya kaunzisha mada JF.

Kama ni issue nzito bac ilete ila uhakikishe sio jambo ambalo ww mwenyew huwez kulitatua, akili na fikra unatumia kufanyia nn kama hata vitu vidogodogo unavofanyiwa na mke wako unashindwa kuvitatua.

Alaf tukumbuke kitu kimoja, sikuzote mwanamke ni mtu wa majaribio, mkiwa kweny urafiki atakujaribu, mkiwa kweny uchumba atakujaribu, mkiwa kweny ndoa bado ataendelea na majaribio yake, anafanya hivo kwasababu wanataka the perfect male partner, sasa atajuaje kama you're the perfect choice bila kukujaribu??

Ndo maana wanafanya hivo, sometimes atakukera ili aone response yako, ili ajue anaishi na mwanaume wa aina, sometimes ataanzisha ugomvi na wanaume wengine ili aone ujasiri wako kama utaweza kumtetea, kiufupi anachotaka ajue ni kwamba, "Je wewe ni kweli yule unayesema na je ww ni mtu ambaye anaweza akakuamini na kukupa maisha yake" its very simple, sasa unakuta mshkaji mwingine haelewi haya mambo kajaribiwa kidogo tuu anaanza kupagawa anatukana wanawake na kuanzisha thread zenye maudhui ya ajabu, kitu kinachonishangaza sana kwa sababu sisi wanaume asili yetu sio watu wa kulialia, haswa ikiwa chanzo ni mwanamke.

Tujitafakari na turudi kweny hali yetu ya mwanzo, it's not too late.
 
Bado hujasema hayajakukuta bado ....

Mkuu mimi nimeshakaa na mke zaidi ya miaka mitatu tuka divorce sitakwambia sababu sasa wewe je umekaa na mke ndani miaka mingapi kuishi naye kulala nakuamka?
Una uhakika hayajanikuta boss?
nimepitia changamoto nyingi sana kweny mahusiano yangu na sijawahi kuyaleta humu JF, una deal nayo tuu kama mwanaume.
 
Wahenga walisema "Pilipili usiyoila yakuwashia nini"
Najaribu kuanza kuvuta picha kama mada zinakukera au zinakukwaza achana nazo unapobishana au kuelekeza watu wa dizaini hii tunakuchukulia kama timu moja tu ila kwasababu umeshavuka unataka wenzio waache kuyazungumzia haya

Hii inaitwa JAMII FORUM yaani kuna mambo mengi ambayo watu wanakuwa wanayapitia katika jamii leo,kesho n.k mtu anapoanzisha uzi leo anategemea kupata mawazo meeng juu ya tatizo lake KWA muda mfupi (Sharing is caring) kupitia Jamii inayomzunguka,kwako ni kero kwakuwa umeshavuka kipindi hiki(Umepevuka) ila kuna vijana weengi wanateseka kupitia experience za watu wengine wanajifunza na kujirekebisha.Wanaume weengi in nature sio wazungumzaji Sana kama jinsia me hivo njia yao ya kutoa moyoni ni kupitia majukwaa kama haya

Mwisho unapofanya jamboo lolote kuwa mdadisi na sio mhukumu .......mambo haya yanayozungumziwa na wanaume na wanawake ni maisha halisi yanayojenga watu kama yasingekuwa na umuhimu zamani Sana mods wangeshafunga jukwaa kama hili ila kwakuwa watu wanaelimika na kufikia stage nzuri hakuna tatizo la wanaume kutoa ya moyoni
 
Habari.

Nitaanza kwa kusema kwamba Mm sio mgeni humu JF, ni member wa muda mrefu kidogo nina kama miaka 6, sema nimepoteza account yangu, maybe imefutwa kwa sababu kuna kipindi nilikuwa less active, nimejaribu ku-log in imekataa.

Kilichonifanya nianzishe hii thread ni kukereka, sijajua labda nyie mmezoea ila tangu nirudi humu JF nimekuwa naona kuna thread nyingi sana zimeanzishwa na zinaendelea kuanzishwa zenye malengo ya kuponda wanawake na kutunaka wanawake....kwanini?

Hv ni asili yetu kweli sisi wanaume kuwa na mdomo mwingi kiasi hiki, kila siku kuanzisha thread za kulialia kuhusu wanawake, mambo mengine watu wanalalamika ni ya kijinga sana hadi unatafakari aliyeandika hv amewaza nn kichwan mwake.

Kwa siku unaweza kupishana na threads karibia saba za kulalamikia wanawake na ukakutana na threads kama mbili za kulalamikia wanaume, ni kitu cha kustaajabisha sana, yaan wanaume tumewazidi wanawake midomo na kulalamika.

Kama mwanamke unayempenda/mpenzi/mke wako amekutendea ndivyo sivyo deal nae kama mwanaume sio unaona kwamba hii ni fursa ya kaunzisha mada JF.

Kama ni issue nzito bac ilete ila uhakikishe sio jambo ambalo ww mwenyew huwez kulitatua, akili na fikra unatumia kufanyia nn kama hata vitu vidogodogo unavofanyiwa na mke wako unashindwa kuvitatua.

Alaf tukumbuke kitu kimoja, sikuzote mwanamke ni mtu wa majaribio, mkiwa kweny urafiki atakujaribu, mkiwa kweny uchumba atakujaribu, mkiwa kweny ndoa bado ataendelea na majaribio yake, anafanya hivo kwasababu wanataka the perfect male partner, sasa atajuaje kama you're the perfect choice bila kukujaribu??

Ndo maana wanafanya hivo, sometimes atakukera ili aone response yako, ili ajue anaishi na mwanaume wa aina, sometimes ataanzisha ugomvi na wanaume wengine ili aone ujasiri wako kama utaweza kumtetea, kiufupi anachotaka ajue ni kwamba, "Je wewe ni kweli yule unayesema na je ww ni mtu ambaye anaweza akakuamini na kukupa maisha yake" its very simple, sasa unakuta mshkaji mwingine haelewi haya mambo kajaribiwa kidogo tuu anaanza kupagawa anatukana wanawake na kuanzisha thread zenye maudhui ya ajabu, kitu kinachonishangaza sana kwa sababu sisi wanaume asili yetu sio watu wa kulialia, haswa ikiwa chanzo ni mwanamke.

Tujitafakari na turudi kweny hali yetu ya mwanzo, it's not too late.
Mbona naona kama umeandika yasio kweli? Ziko wako thread hizo hapo?
 
Back
Top Bottom