Wanaume: Mnapenda wapole au Wanafiki?

Wanaume: Mnapenda wapole au Wanafiki?

Da Pretty

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
3,059
Reaction score
1,153
Habari wanajamvi.

Nimekuwa najiuliza hili swali, Wanaume mnapenda Mwanamke yipi haswa? Nina marafiki wa kiume na hata kaka zangu ambao huwa naongea nao kuhusu mahusiano.

Utakuta yupo na mwanamke muda mrefu halafu Mara tu unasikia ameoa mwanamke mwingine, baadae anataka kumrudia wa zamani awe mchepuko. Nikiuliza kulikoni ndio nachoka, unapewa kasoro za mke aliyeolewa, sasa najiuliza ilikuaje?

Kuna aliyeoa mke halafu anadai mke kapoa sana, hajui kuomba wala kuanzisha gemu, hana maajabu. Nikiuliza kwanini sasa alimuacha ex? Anasema alichangamka sana na anaonekana mjanja mjanja.

Mwingine hata sijui wala hajanambia kama ana mchepuko ila story zake ni hizohizo mke hajiongezi, mke mstaarabu sana hadi kitandani, ukimuuliza alitaka mke aweje na unamuuliza hakuwaona hao watundu? Anasema aliwaona na atakupa scenario mbili tatu. Uliza mbona hukuoa huyo?

Jibu ni kuwa aliogopa yale mautundu dada anavyojiachia. Mkioa wapole mnayamiss tena.

Kwani mnatakaje? Mwanzo aigize kama mzembe halafu baadae aanze mautundu?

Siwaelewi tu na mkae mkijua hata hao mnaowaona wapole. Kuna mahali wanafunguka kama wewe unavyowafungukia wa nje.
 
Mwanamke awe mpole ila kitandani awe ni mtundu mauno feni hapo sio awe mpole mpaka kitandani.
 
Mwanamke ni kiumbe kinachoeleweka umbo tu mengine ni mchanganyikeni..

Mengin katafute kwa mkuu wa mkoa wa kilimanjaro' utaelewa.
 
Kila mmoja na uchaguzi wake.. binafsi napenda mpole,kichwani timamu haswa,asiwe mropokaji tu ama mmbea Kama tarumbeta.. upande wa mahaba sasa lzm tuvunje chaga!.. sitaki kutawaliwa na ke! Kila mmoja ahudumu Kama nafasi yake inavyomtaka.. akitaka kunitawala ajiandae kuwa mapengo au akamuangalie shilole sasa zile ngeo ajumlishe na alama za kung'atwa..😂
 
Yeyote yule (me au ke) aliyezoea radha tofauti, akimaliza muda mrefu lazima na radha moja atakumbuka ya kale... Kizazi chetu ndo kimefika kituo hichi
 
Mkuu wa mkoa alishasema wanaume wanapenda vipande vipande, huwezi kuwa navyo vyote
 
Wanaume atupendi tunatamani, nampenda mama angu tu, huo ndo ukweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom