Wanaume mnaonyanyaswa na wanawake msifiche uovu huo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
WANAUME WATAKIWA KUTOFICHA UKATILI WANAOTENDEWA.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ACP Ramadhani kingai amewashauri wanaume kuacha kuficha vitendo viovu wanavyotendewa na wanawake kwa kutoa taarifa katika mamlaka husika ili watuhumiwa washughulikiwe kisheria.

Ushauri huo aliutoa leo Jijini Dar es salaam katika hafla ya utoaji misaada na kuwaona wagonjwa hospitali ya Polisi Kilwa road Dsm ambapo Askari polisi wanawake wa Mtandao wa kijinsia kutoka Mkoa wa kipolisi Kinondoni ikiwa ni muendelezo wa kipindi cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na watoto.
 
Mwanaume huwa hanyanyaswi ila ana nyanyasika na ni watu wa kukomaa unaweza kukuta hata kamanda mwenyewe ana nyanyasika lakini anakomaa na kutoa wito kwa wenzake. Mambo yetu wanaume si ya kupiga piga kelele kama kasuku kwa kuwa tunajua tumeumbwa kupata tabu na mateso. Jiulize kwanini mitume na manabii wote walikuwa ni wanaume. Jiulize kwanini "walimtundika" Yesu na si Maria Magdalena? Kikubwa mwanaume unacho takiwa ni kuwa na maamuzi basi hata macho yakiwa mekundu vipi!
 
Aisee labda ukute hao Askari ni wanawake...ila kama ni wanaume ukienda kuripoti kesi ya kunyanyaswa na mkeo asilimia kubwa utaambulia matusi na dhihaka tu.
 
Back
Top Bottom