Wanaume: Kwanini hampendi ndugu wa wake zenu?

Wanaume: Kwanini hampendi ndugu wa wake zenu?

Na vp wanawake wanaojenga kwa siri asilimia kubwa wanaenda jenga makwao huo si ubinafsi.
 
kwa hili umewasingizia wanaume....tena xn labda ingekuwa ni kinyume chake ningekusapot
 
Haaa haaaa mleta mada kaangalia upande wake hajafanya utafiti wa kutosha.Mimi ninashiriki kila tukio upande wa mke wangu liwe la shida kwa maana ya kifo au raha kwa maana ya harusi,ubarikio...........

Hongera....
 
Hivi inakuaje mwanaume umeoa alafu hautaki ndugu wa mke waje kukutembelea?

Kunatokea na harusi ukweni huendi sherehe huendi unajifanya upo busy au unajifanya haupendi sherehe.

Wakati zikitokea za kwenu mnakua vimbelembele na kuforce mke ashughulike mwanzo mwisho.

Mnajitahidi kufanya watoto wawe kwenu tu upande wa mke hapana, aisee kuishi na mume wa hivi unahitajika uvumilivu wa hali ya juu.

Wanaume acheni ubinafsi.
Hilo halina ubishi ndugu, mwanaume anapooa anampeleka mke wake kwa ukoo wa kwao na nyumba yake, na mwanamke anapoolewa anaoondoka na kufanyiwa send off na ndugu zake wakijua ndio bye bye hivyooo!!! ila kama mwanamke mwenye hekima atatumia busara kuomba ruhusa ili awe karibu na familia yake ila mara nyingi familia za hawa wake zetu hazikawii kuingilia mambo ya ndoa zetu, kuchunguza chunguza na umbea umbeaaa mwiiiingi hadi kufikia kutengeneza ugomvi! na ukiona mume wako hapendi kuwa karibu na ndugu zako ujue walimpa misukosuko mingi na hata madharau punde ulipomtambulisha kwenu! sasa amesha kupata ameamua kukaa mbali na matatizo! na penda usipende ukishaolewa wewe sio wa kuleee ulikotoka ni wa familia ya mume wako, finish!
 
Simple....
Kama hataki ndugu zako na wake wasije....

Asiposhuriki kwako na kwake usiende......

Kuna viunbe bila kuvifundisha njia ngumu watakusumbua...

Una mume unayemfanyia ubabe huo na bado mkawa na amani ndani ya nyumba!?
 
Una mume unayemfanyia ubabe huo na bado mkawa na amani ndani ya nyumba!?

Wakati mwingine tough love inabidi ihusike mpaka atakapo tambua kuoa ni kuungabisha familia mbili tofauti.

Kuna binadamu usipofanya hivyo haelewi ....kwa hiyo sio ubabe ni kufunza mtu somo tu....
 
Wakati mwingine tough love inabidi ihusike mpaka atakapo tambua kuoa ni kuungabisha familia mbili tofauti.

Kuna binadamu usipofanya hivyo haelewi ....kwa hiyo sio ubabe ni kufunza mtu somo tu....

Hahaha nadhani kwa njia hiyo hilo somo halitaingia bali litavuruga sana mambo.

Unajua bana mwanaume kwa mwanamke ni kama Chai na mkate au mfupa na fisi , kuna vitu na namna ya kipekee Mungu amewapa ya kumlainisha mwanaume ni basi tu mmeshindwa kujua your potential methods.
 
Labda kwenu mijini ndo mnakatazana.. Sie vijijini utakatazaje watu?? Maana uko bize shamba na kuchunga ng'ombe.. kaja nani sijui.... utasimuliwa jioni..
Maana sidhani kama ndugu wa mke watakaa kwetu miezi...kwao shuguli hamna? Automatically watakaa siku kadhaa....wenyewe wataondoka- kama vipi nao wanaingia shamba... ndugu yao anaenda shamba, wao wasiende kwanini? Wakapige umbea shambani..
 
Hii ishu nahisi kama ni vice versa, maana nyumba nyingi utakuta ndugu wa mke ndo wamelundikana hapo, wa Mme ni wa kuja na kuondoka
 
waje kufanya nini bana,, kwanza nikiwataka utamlaumu nani.....wakae huko huko tuuuu....
 
Tatizo lao wanageuza wenzao wazazi, wakae tu kwao hamna namna sasa.
 
mtu hana cha kufanya kwako anakuja kufanya nini?
kama ni salamu si hata simu zipo?
mi wife nilishamwambia ndugu atakayekaa kwangu ni mgonjwa kaja kutibiwa, wazazi na wanaosoma.
hao hata mwaka watakaa.
mtu na nguvu zake anaacha kazi huko eti anakuja kupumzika kwangu!!!
ni kurudisha nyuma maendeleo ya taifa usipotaka kufanya kazi.
 
1:Tabia ya ubinafsi
2: kuhepuka gharama make hamkawii kuamishia ndg wote bila kujari athari upande wa pili.
3: kukosekana kwa upendo na maelewano a kifamilia kwa wote wawili.
 
Back
Top Bottom