Wanaume kuweni wazi kwa wake zenu

Wanaume kuweni wazi kwa wake zenu

Jimaz

Member
Joined
Jan 13, 2014
Posts
35
Reaction score
40
Wanajamvi habari zenu. Mimi ni mke na mama wa watoto 2 , kunakitu sikielewi kuhusu huyu mume na nishaongea naye mara nyingi tu naona bado kinajirudia sasa naomba ushauri wenu great thinkers maana mume nampenda sana na ndoa naipenda na nnaiheshimu tatizo ni kwamba huwa nikifanya kitu ambacho huyu bwana hapendi huwa hawezi kuniambia hapohapo atakaanalo wee sasa siku akitaka kusema ni lazima awe amepiga mbilitatu za kutoa nishai hapo sasa ndio anaweza kunieleza kitu ambocho nimefanya hapendezwi nacho na mara zote huwa labda ni mambo ya malezi ya watoto au kuhusu matumizi ya ndani ya nyumba yani mambo kama hayo .kwangu mimi huwa ninaona ni mambo madogo sana lakini sasa yeye kwa kuwa amekuwa keshakunywa basi huwa ananieleza kwa kufooka kwa ukaali huwa inaniudhi sana na tunaishia kugombana na mwambia haya ni mambo madogo sana mume wangu inatakiwa unieleze kwa upole na upendo sio kunifokea kama mtoto unaniudhi na kuniumiza basii atabwaaata, ila ikifika kesho yeye kashasahau shida inabaki kwangu nakuwakuwa nimechukia nnabonge la donge hii imekaaje nataka aache kuwa anakunywa kwanza ndo aseme tatizo nataka aniambie akiwa sober
 
Huyo anagubu kurekebishika kwasasa sio rahisi......samaki mkunje angali m'bichi
Iyo ni rabia yake ya asili kikubwa mvumilie tú na uwe na subra
Pole bibie!!!!!!!!
 
Hii itakuwa vizuri umpelekee mumeo maana ndio inamuhusu zaidi.
 
Vunja ukimya dada, msubiri akiwa ametulia na hajanywa ongea nae mwambie vitu ambavyo anafanya na hupendezewi navyo, nahisi itasaidia na kama ni mwelewa atabadilika.
Nakutakia maisha mema kwenye ndoa yenu.
 
Wanajamvi habari zenu. Mimi ni mke na mama wa watoto 2 , kunakitu sikielewi kuhusu huyu mume na nishaongea naye mara nyingi tu naona bado kinajirudia sasa naomba ushauri wenu great thinkers maana mume nampenda sana na ndoa naipenda na nnaiheshimu tatizo ni kwamba huwa nikifanya kitu ambacho huyu bwana hapendi huwa hawezi kuniambia hapohapo atakaanalo wee sasa siku akitaka kusema ni lazima awe amepiga mbilitatu za kutoa nishai hapo sasa ndio anaweza kunieleza kitu ambocho nimefanya hapendezwi nacho na mara zote huwa labda ni mambo ya malezi ya watoto au kuhusu matumizi ya ndani ya nyumba yani mambo kama hayo .kwangu mimi huwa ninaona ni mambo madogo sana lakini sasa yeye kwa kuwa amekuwa keshakunywa basi huwa ananieleza kwa kufooka kwa ukaali huwa inaniudhi sana na tunaishia kugombana na mwambia haya ni mambo madogo sana mume wangu inatakiwa unieleze kwa upole na upendo sio kunifokea kama mtoto unaniudhi na kuniumiza basii atabwaaata, ila ikifika kesho yeye kashasahau shida inabaki kwangu nakuwakuwa nimechukia nnabonge la donge hii imekaaje nataka aache kuwa anakunywa kwanza ndo aseme tatizo nataka aniambie akiwa sober

Pole sana mama.

Unajua usipuuzie kuwa ni ulevi. Kinachotokea ni kwamba vitu vidogo vidogo vinavyomuudhi anavimezea na inakuwa kama pressure cooker (kawaida kwa wanaume wengi). Sasa siku na siku akinywa zikipanda basi anaamua kumwaga radhi.

Sasa wewe fanya hivi.
Akianza kubwata akiwa amelewa wewe nawe isipandishe, msikilize na umuitikie tu. Cha muhimu ni kukumbuka kitu alichokufokea nacho. Siku ya pili (usiilaze kiporo) pombe zikiisha kaa nae kwa utulivu (akisha kula na kushiba) na umkumbushe alichokisema jana yake. Kwa upole mueleze kuwa ungependa muwe na mazungumzo kama haya mara kwa mara kwa sababu yatakusaidia wewe kujirekebisha na pia wakati mwengine yatamsaidia yeye kujua shida zako. Usikae kimya tu na kusononeka. Hii haitakusaidia kitu.

Chanzo cha hii tabia:
Nadhani mumeo hua ana soni kukukabili na malalamiko yake ndio maana anasubiri mpaka alewe. Ukimkabili kwa upole ili mzungumze wakati hajalewa baada ya muda itamfanya aone kuwa ni jambo la kawaida kukosoana bila kugombana, na kwamba hahitaji kuunyaka ulanzi ili akueleze mapungufu anayoyaona.

Msumeno:
Ni muhimu hii iwe kwa pande zote mbili. Mumeo anapaswa kujua kuwa kuna wakati ategemee utamueleza mapungufu yake bila ya haja ya kugombana. Hapa uanze na haya mambo yake ya kukufokea akiwa amelewa.
 
Evarm na Kifyatu Mungu awabariki sana kwa ushauri wenu yani nimefarijika sana na nitaufanyia kazi vizuri sana you guys are really great thinkers! be blessed and have a very good day.
 
Mmmh! Eti nilisikiaga mambo ya ndoa kuvumiliana .!!!
 
mwanaume aone aibu kusema mpaka asaidiwe na pombe!!!?
 
katka hali hii una mambo ya kuchagua 1. Ondoa makwazo na pombe ataacha (anaonekana anakunywa kwa ajili yako) na ugomvi hautotokea. 2. Akienda kunywa pombe akirudi wewe kunywa gundi, itika pale tu inapolazmu.
 
Back
Top Bottom