Wanaume kutooa wapenzi wao wa muda mrefu

Wanaume kutooa wapenzi wao wa muda mrefu

Ivi ni kweli kwamba wanaume wengi hawawaoi wapenzi wao wa mda mrefu?

Na matokeo yake kuwaacha na kuoa msichana mwingine

Na sababu huwa ni nini?
Kwa sababu kuwa muda mrefu kunamfanya mtu kumfahamu mpenzi wake kwa undani hivyo ni rahisi kugundua yale madhaifu na mema ya mpenzi wake. Haina maana kuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu kunamfanya mtu aoe au kuolewa. Mahusiano ya muda mrefu yanasaidia kufahamiana zaidi ila haitoi uhakika wa ndoa ya kudumu. Japo inategemea mahusiano yapo vipi maana watu wanaweza kuwa na uhusiano wa muda mrefu lakini hawana mpango thabiti na mikakati ya baadaye. Kwa mfano; mipango ya kutambulishana, idadi ya watoto, imani ya dini, taratibu za kitamaduni na kadhalika. Mambo kama usaliti na hasira yanaweza kupelekea mahusiano yakafutika hata kama yalikuwa na mpango au yamedumu. Cha msingi ni kuomba Mungu na kuridhiana kwa uthabiti kabisa na kumjengea mazingira mpenzi wako kwamba upamoja wenu ni wa kudumu si wa muda bila kusahau kutumia gharama ya muda, mali na hali.Hakuna mahusiano yasiyo na gharama. Vinginevyo utalalamika kuachwa au kuacha kumbe weye huvumiliki.
 
Mkuu tatizo watoto watakua katika wakati mgumu tutawaleaje?na katika misingi gani ya kiimani

Je msipopata watoto?

Mkibahatika kuwapata si mnaamua tu wawe dini gani. Stop complicating this issue.
Nimeshaona wengi tu wameoana and they are the best parents to their kids. Wazazi wangapi wameshindwa kuwahudumia watoto, watoto wanaishi kwenye mazingira magumu, je ni dini ndio inayotoa basic needs? Je ni dini itawapeleka shule na kuwapatia maisha bora? Je ni dini itakayowafanya wawe watoto wazuri kwa jamii nzima inayowazunguka? Heshima?

Jibu ni malezi mema ya wazazi wao. Na malezi mema yanachangiwa sana na mapenzi kati ya wazazi, maelewano, utu, tabia za wazazi. Sio dini

Wazazi wangapi wameoana dini moja na ni walevi? Wazinzi? Wana michepuko? Hawahudumii watoto wao ipasavyo?

Come on! Open up your mind
 
MKE wangu nilikaa naye kwenye uchumba kwa miaka 6, tangu nikiwa form six, chuo 4 years + mwaka mmoja kazini na leo tumeoana na tunaishi vizuri kabisa.
Ila siku niliyomwambia nataka kumuoa alicheka akidhani masihara na akaniambia kuwa ilikuwa imebaki miezi michache ili aniache na atafute mwanamume muoaji, alinivumulia kwa mengi na alikuwa akinipa huduma stahiki hivyo niliamua kulipa fadhila kwa kumuoa maana ndugu wote wa upande wangu walikuwa wanamjua.

Swala ni kujipanga tu na kuwa na malengo.

Kumbe inawezekana. Ukasubiri na matokeo yakawa mazuri.
 
mitano mbna michache sana wa2 wanakaa zaidi y hpo.......shida ni nyie kina dada ohhhh nataka mume mwenye hiki n kile......pia ndoa inakuja rohoni automatically sio kwa kuilazmisha.....angalia ndoa nyingi kuanzia 2009 upto 2014 nyingi chali cz mlikurupushana tu au m2 kapata mimba ndio mnasogezana.

ila rohoni kwako hukutaka ndoa mapema yani unakua kma baba swalehe
Mmh binamu miaka 5 mingi bana hata kama huwezi kumforce mtu akuoe. Afu sisi hatuwaforce ila tunataka kama mnaona hatuwafai, mtuache mapema tu. Tusipotezeane muda
 
Mi naona kikubwa ni kuvumiliana na kumkubali mwenzako kwa hali yoyote ile mi Nina MTU wangu nimeanza naye form two na mpaka nikamaliza chuo na Mungu ametujalia tuna mtoto mmoja ila kila ninapo mwambia tufunge ndoa anajibu hajajipanga je Nina anaweza kua mvumilivu na hapo tumepita milima na mabonde mazito ila na muomba Mungu azid kunipa uvumilivu
 
Kumbe inawezekana. Ukasubiri na matokeo yakawa mazuri.

Inawezekana kabisa ila wadada papara zimezidi akiona mtaani kwao na aliosoma nao wanaolewa anahisi anachelewa. Wangejifunza kujipangia mambo yao bila ya ''influence''ya watu wengine maisha yangekuwa mazuri.
 
Inawezekana kabisa ila wadada papara zimezidi akiona mtaani kwao na aliosoma nao wanaolewa anahisi anachelewa. Wangejifunza kujipangia mambo yao bila ya ''influence''ya watu wengine maisha yangekuwa mazuri.

Ni kweli.
 
Ivi ni kweli kwamba wanaume wengi hawawaoi wapenzi wao wa mda mrefu?

Na matokeo yake kuwaacha na kuoa msichana mwingine

Na sababu huwa ni nini?
Ni somo refu sana, njoo PM.

rubylove
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom