Wanaume, kitanda hakizai haramu bwana!

mr pipa

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2021
Posts
3,609
Reaction score
7,699
Kuna mwamba mmoja yeye kila mkewe akijifungua anachukua vioo viwili, kisha anajitazama yeye na mtoto, ataangalia chogo chake na cha mtoto, akiona kasoro ataanza, mke wangu huyu sio wangu na mambo kibao, sasa tabu yote ya nini? Wanaume mnapima pima ma DNA ili mgundue nini?

Zaidi mtajisababishia mamisongo ya mawazo, ndio mana tunakufa mapema kisa kuendekeza mambo ya kipuuzi.

Wahenga walisema kitanda hakizai haramu, mtoto ni mtoto ma vipimo haya muda mwingine yanadanganya utakuja kataa damu yako kisa kipimo, shauri zenu!
 
Umesikia jana tuu ya Geremi Njitap mchezaji wa zamani wa Cameron na Real Madrid, Chelsea, Newcastle?
Kalea mapacha wasio wake kwa miaka 16,

Hio sio shida kama asingejua, shida imekuja Mama anamletea dharau mbele ya watoto,

Shida inakuja siku atakuja kukufungukia kwa dharau mbele ya watoto kama hivyo...

Mtu kama huyu angejua mapema si angeshaanzisha maisha mapya?

Kaamua kumlipua sasabu ashaona hana cha kupoteza ashamkomba vya kutosha, na jamaa hana options kama zamani.
 
Dharau inaleta uwalakini
 
Akili hizo za kijinga ndio zimewagharimu Wanaume wengi.
Unajifanya mjinga wanawake wanakupasua kikamilifu kukuweka sawa.

Kama alivyoongea reyzzap unaweza kunyamaza na kupuuza Mwanamke akakuletea dharau.

Alafu wanawake wapo very smart kwenye timing. Hawezi kukuletea dharau ukiwa kwenye pick yako. Anakuletea mauzauza ukiwa unamhitaji na akiwa hana chakupoteza.
 
Mm mke wangu akijifungua tu hua nawasikiliza ma sister .Wao hua wanajua kabisa kama umepigwa ama la tukae na dada zetu vizuri wananwake wanajuana yaan kama wifi yao kakupiga wale fasta wanakusanua ww kaka kwenye famila yetu hatuna pigo hizi huyu umepewa.
 
Wanawake wana siri kubwa sana kuhusu mtoto, nawapa mauwa yenu. Jamani akina baba tuwalee watoto bila ubaguzi, mtoto keshezaliwa ni wa wote.
 
Mtoa mada ume sound kama wakike...

Kitanda hakizai haramu inahusika vipi na kulea mtoto asiye wako?

Kwanza kitanda kipi? Na kwanini kitanda, unajua?
 
We jamaa kweli ni Mr. Pipa. Unaendana na jina lako
 
Inaonekana bado unakaa kwa shemeji yako. Toka ingia duniani ujifunze maisha
 
Sometimes we deal with the problems that doesn't exist
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…