Wanaume katika mapenzi ni kama masokwe...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume katika mapenzi ni kama masokwe...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Aug 28, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]  Katika utafiti uliofanywa na akina Kruger na wenzake kwa wanyama jamii ya Sokwe, ilibainika kwamba kulikuwa na vifo vingi vya Sokwe madume wenye umri wa miaka 13. Hali hii ilitokana na sababu kwamba, kwa kawaida katika umri huo, Sokwe madume huwa wamefikia umri wa kupanda na kufanya mapenzi na hivyo huanza kushindana wenyewe kwa wenyewe wakigombea majike na hata kwa lengo la kudumisha hadhi yao miongoni mwa Sokwe wengine.  Katika hatua hii Sokwe hao hufikia mahali pa kupigana na hata kuuana kwa lengo la kujipatia wapenzi na kudumisha hadhi zao. Hali hii haiko kwa sokwe peke yao, bali hata kwa wanyama wengine pamoja na ndege wa aina mbalimbali.  Hata hivyo, pamoja na ukweli huo binadamu naye hajanusurika hata kidogo na purukushani za aina hiyo. Labda kinachomtofautisha binadamu na wanyama hao ni namna wanavyokabiliana na mashindano hayo. Lakini ukweli unabaki palepale kwamba, hata akichagua njia ya aina gani ili kushindana na binadamu wenzake, bado matokeo ya mwisho yatafanana na yale ya wanyama, yaani kifo.  Imeonekana wazi kwamba binadamu wa kiume ndiye mwenye mwelekeo mkubwa wa kupenda purukushani na kuhatarisha maisha yake. Ingawa binadamu huyu wa kiume au mwanaume hahitaji kupigana mweleka na mwanaume mwenzake ili kumpata mwanamke, lakini harakati zake ni zaidi ya kupigana mweleka.  Hata hivyo katika mazingira mengine, mieleka hupiganwa sana katika sura ya mieleka halisi au katika sura nyingine za ushindani wa kutafuta ushindi katika kumpata mwanamke. Wengi tunajua kuhusu habari za kuuawa kwa wanaume kutokana na vurugu za kugombea wanawake.  Tabia hii ya wanaume ya kuhatarisha maisha si ya leo, bali ni ya tangu kale. Huenda huko nyuma baadhi ya wanaume walitumia silaha kwa lengo la kuwadhulumu ama kuwauwa wanaume wenzao ili hatimaye waweze kuwamiliki wanawake wanaowapenda.
  Kwa kawaida, wanaume hushindana wao kwa wao kwa lengo la kumiliki rasilimali na kuhifadhi au kudumisha hadhi na heshima yao ndani ya jamii wanamoishi.  Huu ndio ukweli wenyewe ambao hautofautiani hata chembe na ule wa Sokwe. Ukweli ni kwamba mwanaume anapokuwa na uwezo wa kumiliki rasilimali adimu kama vile fedha na anapoweza kusimika kwa uhakika heshima na hadhi yake, ndani ya jamii iliyomzunguka, mambo hayo humpatia thamani kubwa na kumrahisishia kazi ya kumpata mwanamke anayemtaka.utambuzi na kujitambua
   
 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kazi kweli kweli hapo kati ya mwili sijui kuna nini????? yaani ni balaa mtu yuko radhi hata kutoa gari, nyumba, etc. ili mradi akamilishe haja zake haangalii nikitampata baada ya tendo
   
Loading...