Wanaume huwa tunaambiana ukweli

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Ukiwa na hela hata wanawake waliokukataa kwa
kigezo kwamba 'You are not good looking'
utashangaa wanakutumia meseji za 'Hallo
Handsome how are you'
japo wanajua kabisa una
sura kama Tambi za jiko la mafuta..
My fellow Men, leo nna double portion status kwenu.

-1.Kama Mwanamke anasema Ur not good
looking leo, halafu kesho umepata fuba anaanza
ku-pair Bluetooth, kaa nae mbali..
Heshimu mwanamke anayejua your not good looking
akakupenda as your, akaku-support mka-hustle
mpaka ukafika hapo ulipo angalau kale
ka-uhandsome kalikokuwa hakapo kameanza
kuonekana kwa walio nje...

maana wengi wetu hatuna shukrani kwa wapenzi wetu wanaotupend
kwa misura yetu mibovu na umaskini, tukipata hela
tunataka tubadilishe kila kitu..

Usifanye hilo kosa, kupendwa ukiwa na hela ni rahisi kama mlevi kubanwa na kwikwi... A true Lover utamjua when you are nothing, atakuvumilia from the scratch, Wanaume tunajisahau sana hili!

-2.Mwanaume kuwa na hela ni sawa na Mwanamke
kuwa mzuri, hela kwa Mwanaume ni dalili wewe ni
Fighter, ni hard-worker,ni Success Chaser, ni Paper finder..hizi ndo aina za watu Wanawake wanataka...Sio maneno mengi unanukia Pafyumu
kama muuza urembo wa Buguruni, hela huna, you are
simply useless man, hupati mtu...Fanya kazi kwa
bidii, mafanikio hayaji kwa kushinda Bar na kuuza
Sura Samaki -Samaki, sura. Hela huna na Sura huna,sasa tukusaidieje??
 
Kwanza hata uwe mbaya lakini ukiwa na hela unakua mzuri,pesa hua ina miujiza yake kumfanya Ugly akawa Handsome,sasa sio kosa lao ni kosa la CASH msiwalaumu kabisaaaaaaaaaaa,lakini hata wanaume pia wakimuona mwanamke ana pesa majina yote anamaliza ,baby ,sherry,kimwana,queen of my heart,ur da only fish in my sea,ur da only one,my sweetheart,na kadha wa kadha,wakati alipokua hana hata kumuangalia unaona nuksi....
 
Tangu nipate kazi wale madem waliokuwa wananidharau naona salamu zimemekuwa nyingi Mara utaambiwa Mustapha siku hiz unazid kupendeza mara mambo yako safi Pumbavuu Kaaa Mbali kabisaa
 
Sema wanawake ndo mnasababisha mpaka tunachanganyikiwa, unakuta kidume ana hustle huku hana hata mwanamke wa kumtia moyo ili apate nguvu na moyo wa kuzisaka, na hata akiwa nae basi kutwa maneno na vitimbi kedekede... Inachosha
 
Tangu nipate kazi wale madem waliokuwa wananidharau naona salamu zimemekuwa nyingi Mara utaambiwa Mustapha siku hiz unazid kupendeza mara mambo yako safi Pumbavuu Kaaa Mbali kabisaa
''nilivyokuwa kabwela mlinikwepa kama ukoma/ leo mambo juu ya mstari kunisalimu mnaona noma''- Prof Jay- zali la mentali
 
Sema wanawake ndo mnasababisha mpaka tunachanganyikiwa, unakuta kidume ana hustle huku hana hata mwanamke wa kumtia moyo ili apate nguvu na moyo wa kuzisaka, na hata akiwa nae basi kutwa maneno na vitimbi kedekede... Inachosha
jamani atiwe moyo wa nini na he is a man,kwani kuna moyo wa ziada kwa mwanamke au same kila mtu ana mmoja?lol
 
Back
Top Bottom