Wanaume: Huwa mnasahau nini kwa ma-ex zenu?

lady Jay

JF-Expert Member
May 29, 2016
526
646
Habarini. Nina swali kwa wanaume.

Huwa kuna kitu mnakuwa mmekisahau kwa ma ex zenu? Kwa mfano mimi kila ex wangu lazima arudi, oohh nimekumic wakati kipindi tuko kwenye mahusiano most of them walianza kuwa na vituko.

Ukiwa nao labda hapokei simu, hajibu texts, pozi nyingi, kuonana nae kazi mpaka naamua kuwambia ngoja nisikubane tafuta furaha sehemu nyingine kama mimi kwangu unaikosa.

Ila cha kushangaza baada ya muda( pengine kashapata mtu mwingne) anaanza tena ukaribu mara nimekumiss, kila wakati anakupigia simu. Kwanini wakati tupo wote hukufanya haya mpaka tuachane? Na mimi nkishaachana na mtu hisia zinaisha kwake kabisa so hiyo hali inaniboa. Kwanini tukiwa wote vituko halafu baada ya muda unanitaka tena wakati una mtu?

Huwa kuna kitu mnasahau jamani? Ila mimi siwezi mrudia mtu niliyeachana nae asije akawa anataka nichezea bure hata kama yuko serious. Japo kuna wachache ndo wanarudi wanataka urafiki, japo urafiki na mtu uliyempenda ni vigumu labda kama sikumpenda kiivyo urafki sawa tu.

Naomba mnisaidie nijue kwanini mnakuwa hivi? Na hawa watu niwafanyaje?
 
MAPENZI ya siku hizi comedy tupu. Sometym unakuta una act kwa mfano mimi tulikuwa WAPENZI tukaachana kwa sababu ndogo na hatukugombana basi siku tukionana nitaona aibu kukukaushia ntajifanya kama nimekuchangamkia ukiingiia line tunaanza tena tunakumbushiana sex kwa sana.. Kifupi MAPENZI ya sisi waafrica ni kuigiza hivo ex wako akikwambia amekumiss hamna lolote kuna kitu anataka kuwa makini.. Na hata hivo huo umakini Hakuna ngono unafanya very easy nazungumzia kwa vijana Kama mimi. Wachache wanapotezea ma ex wao kweli.. Sio uphilipino huku
 
Wewe una matatizo na usipoangalia utaachwa sana

Wanawake dizaini yako ndo wale wanambana mtu hadi
anashindwa 'kupumua'
mara uko wapi? mara mbona hupokei simu?
mara kapiga,dakika kumi baadae kapiga tena na cha maana hakuna

inaitwa suffocation....wanaume hatupendi suffocation .....

we need 'SPACE'......

Kkukumiss ni kawaida.....anything good huwa tunaki miss
hata msosi wa mama ntilie mzuri uliepita tu mtaa huo kwa bahati mbaya unaweza
kuumiss siku moja...ukarudi mtaa huo huo kutazamatazama kama bado anapika tena
 
Habarini. Nina swali kwa wanaume.

Huwa kuna kitu mnakuwa mmekisahau kwa ma ex zenu? Kwa mfano mimi kila ex wangu lazima arudi, oohh nimekumic wakati kipindi tuko kwenye mahusiano most of them walianza kuwa na vituko.

Ukiwa nao labda hapokei simu, hajibu texts, pozi nyingi, kuonana nae kazi mpaka naamua kuwambia ngoja nisikubane tafuta furaha sehemu nyingine kama mimi kwangu unaikosa.

Ila cha kushangaza baada ya muda( pengine kashapata mtu mwingne) anaanza tena ukaribu mara nimekumiss, kila wakati anakupigia simu. Kwanini wakati tupo wote hukufanya haya mpaka tuachane? Na mimi nkishaachana na mtu hisia zinaisha kwake kabisa so hiyo hali inaniboa. Kwanini tukiwa wote vituko halafu baada ya muda unanitaka tena wakati una mtu?

Huwa kuna kitu mnasahau jamani? Ila mimi siwezi mrudia mtu niliyeachana nae asije akawa anataka nichezea bure hata kama yuko serious. Japo kuna wachache ndo wanarudi wanataka urafiki, japo urafiki na mtu uliyempenda ni vigumu labda kama sikumpenda kiivyo urafki sawa tu.

Naomba mnisaidie nijue kwanini mnakuwa hivi? Na hawa watu niwafanyaje?

Hahahahahaha na waje watusaidie kuelewa walau kiduchu....!!!! Inakera sana wakati mwingine....!!!
 
ukiwa nacho huwez kuona thaman ya kitu ila siku huna ndio unajua thaman.
Weng huwa ni ulimbuken tu. Huwa wanafikiri unachompa anaweza kupata kwa mwingine wanasahau kuwa mapenz sio ngono.
Ngono utapata kwa ke au me lkn upendo hutofautiana.
Kiukweli, mkifikia hatua ya kuachana ujue hakuna mapenz. Wanaopendana wanaoana ila weng ni tamaa tu.
 
Mtalaka hatongozwi,
yani unaweza kutumia nguvu kubwa (muda mwingi, mbinu kali, maneno matamu, kuvumilia usumbufu, uongo, pesa) kumpata mwanamke mpya lakini kwa ex ni kama vile unakumbushia tu.

kwa vile zaman uliishi nae ex wako, unajua ugonjwa wake, matatizo yake, mapungufu yake, zawadi/mambo anayoyapenda, sehemu anazo zipenda, mavazi/vinywaji/vyakula anavyovipenda, utamu wake, siri zake na hata zile aibu zake pia unazijua

Sio ma ex wote unaweza kuwapata wengine wanakuchukia moja kwa moja kutokana na ile hatua ya mwisho mlioachana, mfano umempiga, umemfukuza, umemtukana na kumdhalilisha mbele ya jamii, au umemwambia neno nakuchukia, nitakuua, sikutaki, sikupendi.

Hatua za mwisho ukiachana na ex wako ni muhimu sana kuzingatia ufanye juu chini usimuumize ila ionekane mazingira ndio yamesababisha ila hukupenda itokee hivyo, mfano unabadili namba ya simu (baadae utamuambia simu ilipotea namba zake ulipoteza)
 
Ila na utakayempata baada ya kuachana na wa kwako nae ana ex wake na yuko kama wako tu, hapo kuwa mpole tu na mpe gemu basi maana wako mpya nae anapewa gemu na ex wake.
 
Wewe una matatizo na usipoangalia utaachwa sana

Wanawake dizaini yako ndo wale wanambana mtu hadi
anashindwa 'kupumua'
mara uko wapi? mara mbona hupokei simu?
mara kapiga,dakika kumi baadae kapiga tena na cha maana hakuna

inaitwa suffocation....wanaume hatupendi suffocation .....

we need 'SPACE'......

Kkukumiss ni kawaida.....anything good huwa tunaki miss
hata msosi wa mama ntilie mzuri uliepita tu mtaa huo kwa bahati mbaya unaweza
kuumiss siku moja...ukarudi mtaa huo huo kutazamatazama kama bado anapika tena
Hii kitu ya always calling na text kila dakika ni tatizo saana....binafs inanikera
 
Back
Top Bottom