Wanaume hii imekaaje?

Enny

JF-Expert Member
May 26, 2009
962
130
Kuna kaka mmoja alipendana na mdada. wakati urafiki umekolea akaanza kuhamia kwa mdada huyu kwa kuleta nguo moja, mbili mara kahamisha nguo zote. Mwisho chumba chake kimechukuliwa. Siku moja alimwambia huyu mdada kuwa anataka awalete watoto wake hapo, lakini bibie alikataa na kumwambia kwanza atafute nyumba yake wahamie kwake badala ya yeye kuishi kwa mwanamke. Lakini sasa , huyu mdada jana ananiambia mwanaume kaamua kuagiza watoto waje tu pale hivyo sasa wapo njiani. sasa ameniomba ushauri afanyeje nae hapendezwi na huyu mkaka kuhamia kwake na familia yake? naomba mchango wenu kwa hili.
 
Pole sana dada Enny!

Huyo jamaa unampenda sana? Ukipenda boga penda na ua lake. Mwache awalete watoto kama unampenda.

Tahadhari: Mkigombana utaondoka wewe umwachie nyumba yako kwakuwa baba ni KICHWA cha familia: Stuka!

Kama si wewe yamekukumba mwambie huyo rafiki yako eti babu amemshauri ASTUKE eti!

Mwanaume anayehamia kwa mwanamke SI MME BORA!
 
Mario naleli ee....
 
Last edited by a moderator:
Hivi wakati ameanza kuhamisha nguo moja moja hakumwuliza kulikoni? na je aliwahi kumwambia kuwa ana watoto?
 
Hana haja ya kuanza kujifikiria nini cha kufanya wakati inaonekana yeye toka mwanzo hakuwa na msimamo wa kuishi na mwenza wake,kitendo cha mwanaume kuhamia kwake taratibu bila yeye kuchukua hatua ndio mwendelezo wa haya yanayomkuta sasa.
Pia inaonekana huyo mwanaume mambo yake ni magumu na anamtegemea mwanamke huyo kwa karibia kila kitu,hivyo kama anaweza asubiri watoto wake waje na akae chini na mwenza wake wajue cha kufanya maana wahenga walisema(ukipenda boga,penda na maua yake)
Akishindwa basi abwage manyanga aendelee na maisha yake.
 
HUyo ni mwanaume kweli, hao watoto ni wake kweli maana unaweza sema watoto ni wako kumbe umesaidiwa na wenzio wewe hujui tu, khaaa mwanaume na watoto anahamia kwa mwanamke du kweli , Marioooooooo nalelioooooooooooooooooo
 
mwambie anachunwa shost.
amekuwa ustaw wa jamii bla kujijua
amkimbize hakuna love apo zaid ya kutumika
kadanganyika na muhogo?na maneno lain ya blue band....dah kaz nzto ama kwel mwalimu wetu kaded

SEMESTER IJAYO ATALIPIA YEYE PANGO...ahhh ata ivo aijatulia mwambie akatafute nyumba.

dah kuna watuwanapenda jaman dunian umu mpk akil inahama....:twitch:
 
Mapenzi yao yalikuwa na makubaliano yepi??halafu tujadili vizuri huu usuhano??
 
Anamtaka yeye bila watoto, hapo ni kumweleza ukweli kwamba mimi watoto hapana, vinginevyo nawe ondoka. Hata kama ndo kupenda maua ya boga niletewe watoto bila ridhaa yangu.
 
mme *****,najua imekutokea wewe,acha uvivu bana tafuta vyako,mwanaume anasifiwa kaz sio kula,ebooo:sick:
 
mnh mwache alete watoto wake iwe familia yenu,ila mshirikishe kwenye mambo ya kutoa matumizi -hakikisha na yeye anachangia kama rent,chakula nk....kama hana pesa mtafutie shughuli ya kufanya....
ila kama hujajiandaa kulea napo asikushurutishe,mwambie mtoe suport kwa watoto wake-ila wakae huko huko walipokuwa wanakaa
 
Anamtaka yeye bila watoto, hapo ni kumweleza ukweli kwamba mimi watoto hapana, vinginevyo nawe ondoka. Hata kama ndo kupenda maua ya boga niletewe watoto bila ridhaa yangu.

lakini wadada si mnataka haki sawa? ndiyo hiyo sasa siku hizi raha sana unalelewa na mdada kama jaf kwa shrose unatolewa out rahaaaaaa!
 
huu ni ushauri mzuri sana:first:
Pole sana dada Enny!

Huyo jamaa unampenda sana? Ukipenda boga penda na ua lake. Mwache awalete watoto kama unampenda.

Tahadhari: Mkigombana utaondoka wewe umwachie nyumba yako kwakuwa baba ni KICHWA cha familia: Stuka!

Kama si wewe yamekukumba mwambie huyo rafiki yako eti babu amemshauri ASTUKE eti!

Mwanaume anayehamia kwa mwanamke SI MME BORA!
 
Kuna kaka mmoja alipendana na mdada. wakati urafiki umekolea akaanza kuhamia kwa mdada huyu kwa kuleta nguo moja, mbili mara kahamisha nguo zote. Mwisho chumba chake kimechukuliwa. Siku moja alimwambia huyu mdada kuwa anataka awalete watoto wake hapo, lakini bibie alikataa na kumwambia kwanza atafute nyumba yake wahamie kwake badala ya yeye kuishi kwa mwanamke. Lakini sasa , huyu mdada jana ananiambia mwanaume kaamua kuagiza watoto waje tu pale hivyo sasa wapo njiani. sasa ameniomba ushauri afanyeje nae hapendezwi na huyu mkaka kuhamia kwake na familia yake? naomba mchango wenu kwa hili.

kama ni nyumba ya kupanga aondoke na kumwacha jamaa. Tatizo lake huyo dada litakuwa ni kuwa kimya wakati hakupendezwa na hali tangia jamaa kahamia hapo kimoja. Bora uonekane katili kwa kuwa mkweli kuliko kuumia rohoni kwa kitu usichokipenda.
 
Haki sawa tunazozililia kila siku mbona hatuzipendi sasa?
Ingekuwa huyo mwanamke kaenda kukaa kwa mwanaume na watoto wake angeona sawa eeh? Tena angefurahi eeh?
 
Back
Top Bottom