Wanaume hebu njooni hapa kuna kitu ya bure

Mahondaw

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
67,252
168,551
Mambo! niaje walau! Kuna hii kitu nimeisoma mahala ikanibariki mnooooooooo hivo akili yangu ikaniwazisha sio Mbaya nikishea nanyi kwani yaliyomo yamo iwe kwenye mahusiano ya aina yoyote ile kwa namna moja ama nyingine hii kitu inahuu! Kwakweli sometimes mnajisahau kupitiliza.

1. Usijisahau katika mahusiano ukawa comfortable kiasi kwamba zile mbwembwe zote za kipindi unamtongoza mwanamke wako ukazipotezea.

Mwanaume smart haachi kumfanya mwanamke wake ampende zaidi. Mwanaume anaemfanya mwanamke wake ampende zaidi mahusiano yao hudumu mpaka uchweo.

2. Usisahau kufanya tabasamu kuwa kipaumbele cha mwanamke wako. Ole wao wanaume wanaowanyima tabasamu wapenzi wao wakaacha wanaume wengine ndio wawape tabasamu wanawake zao.

3. Yatunze maneno yako kwa uaminifu mkubwa. Uaminifu ni msingi imara wa mahusiano yenye afya. Mwanaume wa kweli hakimbii majukumu.

4. Usiwe mkoloni katika mahusiano. Kuna haki ya kusikiliza na kusikilizwa (natural justice). Kuwa mwanaume, admit kama umekosea. Kuwa na ujasiri wa kurekebisha pale ulipokosea

5. Usimfanye mwanamke wako aone kama anashindana na muda wako, mfanye ajisikie na yeye anathamani katika muda wako. Sio sababu ya kuwa na muda au laa bali ni jitihada ya wewe kutengeneza muda wa pamoja.

6. Usiwe mvivu. Kuna mtu mwingine pembeni ambaye anatamani kuwa na huyo mwanamke. Linda tunu yako kwa upendo, furaha na amani nae. Usiwe mvivu kumfurahisha, kumlinda, kumridhisha na kumsifia. Pombe na nyama choma zisije zikakuponza.

7. Usihukumu. Kila mmoja anafanya makosa na anajifunza kwayo. Usihukumu makosa yake wala past yake. Na kitu cha muhimu usimhukumu kwa vile unafikiri tofauti na yeye. Binadamu tunatofautiana sana. Enjoy kuwa nae kwa jinsi alivyo. Usilazimishe awe kama wewe.

8. Usi assume kwamba anajua kama unamjali, mwonyeshe kweli unajali. Mpe support katika shughuli zake i.e masomo, biashara, kilimo, etc. Mtumie sms, msikilize, msifie, muonyeshe mapenzi kwa maneno na vitendo na uwe mbunifu.

9. Usiwe mwanaume jina, acha tabia ya kuzila na kususa ,onyesha kuwa wewe ni mtu wa majukumu na ni kichwa katika mahusiano, jenga mahusiano kwa busara zaidi na sio kwa ki imla (dictatorship). Maumuzi yako ya kijinga kijinga yatakutokea puani.

10 Usikate tamaa kirahisi, najua maisha ni magumu ila mwanaume wa kweli anapotaka kitu, atafanya kila awezalo kukipata, unasubiri nini? fanya hivyo sasa.

Mwanangu, Kamwe usichoke kutenda mema maana utalipwa kwa wakati wako usipozimia moyo!

Ninajali.

Mahondaw
 
Hivi unaweza kutabasamu wakati ukidungwa sindano?

Fanyeni utafiti mjue kwa nini Nyani hajengi hali ya kuwa anastahili kuwa na mjengo,

Isije kuwa anakwepa kutozwa kodi.
 
Hivi unaweza kutabasamu wakati ukidungwa sindano?

Fanyeni utafiti mjue kwa nini Nyani hajengi hali ya kuwa anastahili kuwa na mjengo,

Isije kuwa anakwepa kutozwa kodi.

Mhmhmhmhmmmmhhhhmmhhhm atakua ana yake sasa
 
Back
Top Bottom