Wanaume hawapendi Mwanamke Kulalamika

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,900
21,990
[h=3]Wanaume hawapendi Mwanamke Kulalamika[/h]

Ile unarudi tu home kutoka kazini kila siku jioni kiumbe huyu ndo anakutazama hivi?
Nahisi baada ya siku kadhaa utatamani urudi yeye tayari kalala! Binadamu ni kuimbe anayependa sana kulalamika iwe ofisini, kanisani, hotelini, kazini, sokoni, darasani, mikutanoni, msibani, harusini nk watu ni kulalamika tu.

Na kwa upande wa wanandoa mwanamke ndiye anajulikana sana kwa kuwa mtu wa kulalamika kasi kwamba wanaume wengi huwa wanachoka na kuanza kujiuliza hivi mwanamke anahitaji kitu gani maana kila unachompa bado hakiweze kumfanya asilalamike zaidi au tena.

Je, ni tabia ipi huchukizana wanaume?
Ukiwauliza wanaume wengi kwenye ndoa asilimia kubwa watasema hawapendi kabisa tabia ya mwanamke kulalamika kwa kila kitu na wakati wote.

Kwa nini wanaume hawapendi mwanamke mlalamishi/mnung’unikaji?
Wanaume tangu watoto wao wamefundishwa kuwa tough, kuwa wavumilivu, kuwa unemotional, kuwa wanaume na zaidi kwamba tabia ya kulalamika si ya wanaume.
Matokeo yake wamekuwa watu dhaifu sana linapokuja suala la mtu mlalamikaji na hushindwa kuvumilia kuona mtu analalamika mnuda wote.

Wanaume pia ni watu wa ku-fix matatizo au kutoa solution na si kutafuta solution.
Mwanamke anapolalamika kwa mara ya kwanza humvuta mwanaume kuja kutatua tatizo na akiendelea kulalamika mwanaume hujisikia ameshindwa ku-fix hilo tatizo na hujina failure mkubwa.
Kulalamika si njia njema ya kuuliza au kupata kitu kwa mwanaume bali ni njia bora ya kumfanya ajisikie vibaya.

Mwanamke mlalamishi ndani ya nyuma kwa mumewe muda wote hufanya mwanaume amuone ni takataka zaidi na kwamba hawezi kukufanya uwe happy na mwanamke usipokuwa happy maana yake mwanaume ameshindwa kazi ya msingi kabisa katika mahusiano.
Anajiona ni sawa na mwindaji anayerudi mikono mitupu nyumbani baada ya siku nzima ya kuwinda.

Wanawake wengi hutegemea sana mwanaume kuwa source ya furaha zao, huo ni mzigo mzito sana ambao mwanaume anaweza kuubeba.
Pia mwanamke unawajibika kabisa kujipa furaha mwenyewe kwanza, unapochukua jukumu la wewe mwenyewe kuwa mwanamke mwenye furaha na mumeo hujiona amefanikiwa sana hata kama hakufanya lolote kwa furaha uliyonayo na zaidi unapokuwa na furaha unaruhusu moyo mumeo kufunguka kirahisi kwako kuliko kuwa jimwanamke lenye uso usio na furaha kama vile ulilazimishwa kuolewa naye.

Pia kulalamika kunafanya mwanamke usiwe attractive, mwanamke unapolalamika kwa kila kitu na kila wakati mwanaume hukuona upo ugly na huvutii kabisa ndo maana wanaume wengi wanawatoroka wake zao kisa mwanamke ni mlalamisha na mwanaume anasema nimeshindwa kujua anataka kitu gani na pia nitawezaje kumfurahisha maana ni kulalamika tu kila siku.

Usiwe Chronic complainer maana kuwe na jua unalalamika, kusiwe na jua unalalamika.
kuwe na mvua unalalamika kusiwe na mvua unalalamika.
uwe na kazi unalalamika usiwe na kazi unalalamika.
Ukiwa mnene unalalamika ukiwa mwembamba unalalamika.
Uwe na mtoto unalalamika usipokuwa na mtoto unalalamika
Utaishi na nani?
Nani anataka jitu la aina hii?
Jirekebishe!
 
Bwana we,kuna baadhi bila kulalamika siku haijaisha kwa hiyo mzoee na umvumilie
kwa kifupi huwa wanaitwa wanagubu..........
 
Kweli kabisa mdau! mimi binafsi sipendi kusikia lalamishi hizi za kike na mara nyingi hazina maana kwani wanatumia kama nyia za kutoa shida zao badala ya kusema na kujadili kwa njia ya kawaida.

mara nyingi naona bora niende mbali na mazingira ya lalamishi, kwani yana yanapunguza mapumziko na raha ya maisha, bora niende hata baa kwani ntasahau habari hizo kwa muda
 
Mkuu Tusker Baridi
Niombe radhi bana alikuwa jiran yangu yule ila nafikiri ukitaka kujua Maombi ya mwanamke yanartisha kamuulize masanja uko aliko..alikuwa akirudishwa usiku na gari za wanawke huku akigawa michango yetu aliovuna kwenye vitabu feki ya simba na yanga...mkewe aliingia maombi ndugu ilikuwa ni ama aondoke mkewe ama masanja ..ndio maana akafa kifo cha aibu tena ...mi niliwahi kusema wanwake awajui siri na nguvu walizonazo juu ya wanaume piga goti nakwambia kama utomwona mkemwanzako basi utaenda msiba wake
 
aisee, nilidhani ni mimi tu nasumbuka. Mke wangu mlalamishi mpaka najuta kumwoa. Inaboa ajabu!
 
asante tumekuelewa..lakin msiache kutusikiliza

Tunawasikiliza sana, lakini mhhh, saa nyingine mpaka inaboa. Kwa kweli wanawake walalamishi (na wengi wao wako hivyo) ni kero sana. Jifunzeni kuwa more positive katika communication ndani ya mahusiano.
 
Back
Top Bottom