Wanaume fungeni uzazi!

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Tumekuwa tukiwashuhudia akina mama wakihangaika huku na huku wakitafuta njia mbalimbali za uzazi wa mpango au kufunga kizazi.

Ni nadra kuwakuta akina baba wakijishughulisha na mambo hayo hata kama wanafikiri hawahitaji kuongeza watoto wengine. Ni muda mwafaka sasa wanaume kuchukua hatua na kufunga uzazi.

Mwanaume anaweza kufunga uzazi na mambo mengine ya ndoa yakaendelea kama kawaida. Wana JF mpo?
 
Tumekuwa tukiwashuhudia akina mama wakihangaika huku na huku wakitafuta njia mbalimbali za uzazi wa mpango au kufunga kizazi. Ni nadra kuwakuta akina baba wakijishughulisha na mambo hayo hata kama wanafikiri hawahitaji kuongeza watoto wengine. Ni muda mwafaka sasa wanaume kuchukua hatua na kufunga uzazi. Mwanaume anaweza kufunga uzazi na mambo mengine ya ndoa yakaendelea kama kawaida. Wana JF mpo?

Mwanaume afunge nini????
Aisee . . . .
Bila shaka wewe ni mwanamke, ingetamkwa na mwanaume ninge . . . . .
 
kwanini tufunge uzazi? kuna njia za asili za kuzuia mimba kama kufuata siku nk weee maandiko gani yanasema tufunge uzazi????

kwa kina mama pia kama mkiwa na mahusiano mema na waume zenu hakuna haja ya kutumia madawa kupanga uzazi mnajitafutia kansa bure,ndio maana tumepewa akili tofauti na wanyama.

Ukichunguza vema hakuna daktari hata mmoja anaetumia madawa kupanga uzazi au vitanzi nk wao wanahubiri lakini hawatumii wanajua madhara yake.

siku hizi binti hana hata mtoto anatumia madawa akiolewa hakuna mtoto jamani amkeni............kama mkishindwa kabisa bora condom lakini sishauri madawa,vitanzi sijui aftersex nk mabinti kuweni macho.:disapointed:
 
Binafsi sishauri!Ila ulivyowakatalia wanaume ni kama vile ni sawa kwa wanawake kufanya hivyo!

Mi nazungumza kama mwanaume na nimeshajaribu kuwauliza wenzangu kuhusu hilo.

Ni asilimia 2 tu ya niliowahi kuwauliza ndio waliona ni vyema lakin sio wafanye wao bali wanaume wengine. Yaani kwa kifupi karibu wanaume wote hawakubaliani na hilo.

Kwa wanawake ishu ipo tofauti, wao tayari wapo wanaotumia madawa na hata wale wanaofanya operesheni ya kugeuza kizazi kabisa. Na utakuta wanafanya hivyo kuzuia wasishike mimba tena (kama ameshazaa watoto idadi anayotaka) na hivyo haoni sababu ya kuendelea kuzaa tena.

Kwa mwanaume hata awe ameshazalisha watoto mia, na akaona wanatosha bado hawezi hata kuikiria kufunga risasi za bunduki yake.

Inagwaje hata wanawake wapo ambao hawtaki kufunga uzazi hata akimaliza kuzaa.
 
Binafsi sishauri!Ila ulivyowakatalia wanaume ni kama vile ni sawa kwa wanawake kufanya hivyo!

Yaani hata ungeshauri bado ungepata wakati mgumu wanaume wengi kukuelewa.
Ni ngumu sana kumshawishi mwanaume rijali afunge uzazi wake
 
Mi nazungumza kama mwanaume na nimeshajaribu kuwauliza wenzangu kuhusu hilo. Ni asilimia 2 tu ya niliowahi kuwauliza ndio waliona ni vyema lakin sio wafanye wao bali wanaume wengine. Yaani kwa kifupi karibu wanaume wote hawakubaliani na hilo.
Kwa wanawake ishu ipo tofauti, wao tayari wapo wanaotumia madawa na hata wale wanaofanya operesheni ya kugeuza kizazi kabisa. Na utakuta wanafanya hivyo kuzuia wasishike mimba tena (kama ameshazaa watoto idadi anayotaka) na hivyo haoni sababu ya kuendelea kuzaa tena. Kwa mwanaume hata awe ameshazalisha watoto mia, na akaona wanatosha bado hawezi hata kuikiria kufunga risasi za bunduki yake.
Inagwaje hata wanawake wapo ambao hawtaki kufunga uzazi hata akimaliza kuzaa.
ivi mkuu unatoka kijasho kujibu hii sredi?
 
kama ni mdada basi nazani wimbo wa "mapepe" wa kingwendu unamfaa zaidi

Eti CPU asimamishe fank-shenalite ya prosesa yake ???????:nimekataa:nimekataa:nimekataa
Halafu libaki li-CPU lenyewe kama pambo la maua yale ya plastic sebuleni????!!!!

Labda nizaliwe na akili za kunguni
 
Eti CPU asimamishe fank-shenalite ya prosesa yake ???????:nimekataa:nimekataa:nimekataa
Halafu libaki li-CPU lenyewe kama pambo la maua yale ya plastic sebuleni????!!!!

Labda nizaliwe na akili za kunguni

Kwahiyo hapo ndipo uanaume ulipo?
 
Back
Top Bottom