Wanaume bwana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume bwana!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 4, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  [h=3]Wanaume bwana![/h]

  [​IMG]
  Kwa nini wanaume wanahitaji sex na wanawake wanahitaji upendo.
  wanaume huwa frustrated na wanawake kwa kuwa hawapendi sex na wanawake huwa frustrated na wanaume kwa kuwa kila mara wao ni sex tu.
  Wanawake wanawalaumu sana wanaume kwa kuwa hawajui kupenda na wanaume wanawalaumu sana wanawake kwa kuongea tu kuhusu upendo lakini hawataki kuonesha vitendo (kufanya mapenzi).

  Sababu inayofanya binadamu kujihusisha na sex ni kutokana na hormone ya testosterone, ambayo kwa kiwango kikubwa ni hormone ya wanaume.
  Mwili wa kawaida wa mwanaume huzalisha mara 20 zaidi ya mwili wa mwanamke.
  Kwa maneno mengine, hamu ya sex kwa mwanaume katika siku moja ni sawa na hamu ya sex kwa mwanamke baada ya kukosa sex kwa siku 20 au hamu ya kuhijitaji sex kwa mwanaume katika siku 20 ni sawa na hamu ya mwanamke kukosa sex kwa mwaka mzima.

  Kwa kufahamu hizo tofauti hadi hapa unaweza kufahamu maumivu ambayo jinsia nyingine inayapata.
  Kumbuka wanaume kuhitaji sex hadi kupitiliza hawajasababisha wao au ni kitu wanajitakia bali ndivyo wameumbwa na hizi ni sababu zinazofanya mwanaume kuwa mwanaume na mwanamke kuwa mwanamke.
  Wanaume na wanawake ni tofauti.
  +++++++++++++++++++++++

  Mwanaume anaweza kuzalisha au kusababisha mimba kwa mwanamke kila anapofanya sex, lakini mwanamke anaweza kuzaa mtoto kila baada ya miaka 2; hii ina maana mwanamke lazima awe makini kuchagua sana (picky) mwanaume wa kuoana naye ili kuzaa naye watoto.
  Lazima achague the best seed.
  Kwa miaka mingi (generations) wanawake wamekuwa wakilipa gharama (price) kutokana na kuchagua wanaume wasiofaa (mbegu dhaifu); kwani wanawake waliochagua wanaume wenye udhaifu wa genes wamesababisha kuwa na watoto (offspring) ambao imekuwa si rahisi kuishi (survive); wanawake waliochagua wanaume wenye genes imara wamezaa watoto imara ambao waliishi, na hawa ndio wanabeba genes za mama zao za kuwa wachaguaji wa kupitiliza (picky) linapokuja suala la kuoana hadi leo, na moja ya hao offspring ni wewe.

  Kwa asili wanaume huhitaji sex mara kwa mara ili kusambaza kizazi wakati wanawake huhangaika kutafuta the best seed ili kuwa na maamuzi bora ya kupata mbegu bora ya kuwa na kizazi bora.

  “Men seek quantity - women seek quality”
  Ndiyo maana wanaume wanahitaji sex na wanawake wanahitaji upendo.

  Upendo ni uhakika ambao wanawake huhitaji kwa mwanaume ili kuhakikisha atashikamana naye kusaidia kulea watoto na kuhakikisha wanakua, na sex kwa mwanamke ni kitu cha ziada anachotoa kwa mwanaume ili awe committed kwake.

  Kwa mwanaume sex ni kitendo cha kimwili ambacho husaidia kupunguza msukumo wa hormone ya testosterone ndani ya mwili wake na baada ya kufanikisha ndipo mwanaume huanza kuhisi upendo kwa mwanamke au hujikuta mwanamke huyo hana thamani tena kama hakuna commitment (ndoa)
  Ndiyo maana wanaume wengi hupotea baada ya kukipata kile walikuwa wanakitafuta kwa mwanamke kwa kuwa issue nzima ilikuwa ni testosterone na si upendo.
  Ndiyo maana mwanamke kumpa mwili mwanaume mapema kabla ya ndoa ni hatari sana kwani wanawaume wengi huwa hawajawa tayari kupenda (huwa anakuwa bado hajampenda mwanamke bali ni msukumo wa testosterone).
  Mwanaume huhitaji muda ili feelings zake ziwe developed na njia sahihi ambayo mwanamke anaweza kufanya ni kukaa mbali na maombi yake ya sex.
  Kama ataweza kujizua kufanya sex maana yake ataweza kujenga upendo wa kweli ambao ndiyo msingi wa mahusiano, kinyume na hapo baada ya sex ataishia na mwanamke atajikuta anakuwa mtumwa.

  sababu ya wewe kuwepo hapa leo ni kwa vile ancestors, wanaume na wanawake walifanya maamuzi sahihi na wakaweza kuvutia partner sahihi (best seed) ambaye leo wewe upo.
  Hivyo haina haja kujisikia uchungu sana kwa mume kuhitaji sex mara kwa mara na mke kuhitaji upendo au kupendwa mara kwa mara.
   
 2. T

  Tall JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Inawezekana unawaelewa wanawake......likini ni vigumu kutuelewa sisi wanaume 100%...kutuelewa inabidi kwanza uwe mwaume.
   
 3. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pdidy umeamkaje??
   
Loading...