Hakuna sera madhubuti mpaka sasa. Unakuta hawa watoto wa namna hii wanalelewa na mzazi mmoja mwingine hasa baba amesepa na hakuna sheria ya kumbana. Kutokana na ongezeko kubwa la watoto wa mitaani natoa maoni yangu katika mjadala huu wa katiba "Kuanzia sasa jukumu la kuwatunza watoto katika familia ni la baba na mama" kama huwezi kutunza watoto basi sio lazima kutiana mimba na kuzaa watoto halafu kuwaacha mabarabarani wakiishi katika taabu na hatimaye kukosa muelekeo yaani kuwa wezi,malaya na wauza unga.Kuwe na sheria na dhabu ,tumechoshwa kuwasikitikia watoto wa mitaani