Wanaume acheni kupiga wake zenu watoto wanaona

Wanaume acheni kupiga wake zenu watoto wanaona

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,014
Reaction score
6,834
Deus Mkombozi KiraFollow
December 9 at 10:45 PM
HABARI YA KUSIKITISHA NA LENYE FUNZO KUBWA NDANI YAKE!!!
Juzi nilihudhuria msiba wa rafiki yangu mmoja na mkewe. Yeye na mkewe walifariki kwa ajali ya gari, wameacha watoto wawili mmoja wa miaka kumi na mwingine wa miaka minne wakike, mkubwa ni wakiume.
Sasa tukiwa kwenye ule msiba, mimi kama rafiki nilikuwa karibu sana na wale watoto kwani wananifahamu kama Baba mdogo, kusema kweli nilichokishuhuduia kilinifanya nije nimpende mke wangu mara mia zaidi.
Kweli nampenda sana mke wangu lakini kuna wakati namchukuliaga poa nikiwa na mambo yangu najifanya kidume na namuudhi. Kwasiku tatu zote nilikuwa karibu na ile familia tukimalizia msiba, katika kipindi chote hicho watoto walikuwa wakimlilia Mama yao.
Yaani wakilala wakiamka ni kuniuliza, wananiita anko, Mama yuko wapi? Wanamuuliza Bibi yao Mama yuko wapi? Sasa kilichonifanya nilie nipale ambapo mtoto mkubwa wa miaka kumi ambaye anaelewa kitu kidogo alikua anampembeleza mdogo wake alikuwa anamuambia.
“Usilie Mama kaenda sehemu nzuri, kaenda kupumzika kwa Mungu na Malaika…” Mdogo wake ndipo alipouliza Baba nayeye, akasema “Amemsindikiza Mama watakaa huko na mimi ndiyo nitakulinda, usiogope nipo hapa. Unakumbuka siku ile Mama alivyotuambia twende kwa Bibi kukaa wenyewe…”
Alimuuliza… “Mimi si nilikulinda…nitakulinda na sasa…Mama ametuangalia lakini sisi hatumuoni….” Kama hapo umelia basi subiri majibu ya yule mdogo wake. Huku akijaribu kujizuia kulia alimuuliza Kaka yake. “Sasa kama Baba ameenda na Mama si atampiga tena, mimi sitaki Mama apigwe, kwanini asingeenda peke yake…
.” Nilianza kuwaza namna ambavyo rafiki yangu yule alikuwa akimnyanyasa mkewe, namna alivyokua akimpiga na kumsimanga, nilishaongea naye mara nyingi lakini hakujali.
Lakini alikuwa anawapenda watoto wake na kila siku aliwadekeza ila hawakumkumbuka. Jibu la kijana wake ndiyo lilinifanya niamini kuwa wanadamu si chochote. “Huko hawezi kumpiga, Mama ameenda kwa Mungu, huyo ana nguvu zaidi kuliko Baba. Akimsogelea tu Mama atamchanachana kama karatasi! Mungu ana upendo hapigi watu wema kama Mama!”
Hapo yule mtoto alikuwa akiongea kwa uchungu lakini kwa hasira na kwa imani kabisa. Sikuweza kuendelea kuvumilia kuwasikiliza, niliwaacha na kwenda kumuangalia mke wangu, nilimkumbatia na kumuuliza “Mke wangu hivi na mimi nakunyanyasa?”
Aliniangalia kwa mshangao, aliniulzia kwanini unasema hivyo, nilimuambia hapana niambie tu. Niambie kama kuna kitu nakifanya kinakukwaza ambacho watoto wangu watakiona. Nilimuambia “Nataka wanangu waniulizie nikifa, sitaki wanangu wafurahie kifo changu.
” Mke wangu alinikumbatia huku akitokwa na machozi aliniambia “Hakuna mume wangu, wewe ni mume bora, sema uache tu kuweka soksi kwenye makochi na kuacha sahani Kitandani.”
Nilijikuta natabasmau kidogo, kwani mke wangu alikuwa na furaha. Sasa hivi najifunza nisiache soksi kwenye makochi wala sahani kitandani. Najua alikua anatania ila kama kinamkera nitaacha, maisha hapa duniani ni mafupi, watoto ndiyo kitu tunaacha kwaajili ya kututambulisha, sitaki wanangu wanaitambue kama Baba mkatili. Hupati faida yoyote kwa kumnyanyasa mke wako na wala haikufanyi kuwa mwanaume zaidi!
****MWISHO
Lengo kuwakumbusha wanaume wenye tabia za kuwanyanyasa wake zao kuwa hawana nguvu kuliko MUNGU na ipo siku watafika huko.
Deus Mkombozi Kira.
 
Kweli man!hilo kosa huwa tunafanya!!!Nilisikitika jujuzi mwanangu dina alimwambia mama ake "usifanye hivyo baba atakupiga!"nilisikitika sana!kumbe kile kibao siku ile dogo aliona hadi leo anakumbuka!!!najuuta sana!!!never do again!!!japo huwa wanaudhi sana hawa wenzetu!!!
 
Kweli man!hilo kosa huwa tunafanya!!!Nilisikitika jujuzi mwanangu dina alimwambia mama ake "usifanye hivyo baba atakupiga!"nilisikitika sana!kumbe kile kibao siku ile dogo aliona hadi leo anakumbuka!!!najuuta sana!!!never do again!!!japo huwa wanaudhi sana hawa wenzetu!!!
Wewe ukimuudhi huwa anakupiga pia ama wewe umekamilika??
 
Kweli man!hilo kosa huwa tunafanya!!!Nilisikitika jujuzi mwanangu dina alimwambia mama ake "usifanye hivyo baba atakupiga!"nilisikitika sana!kumbe kile kibao siku ile dogo aliona hadi leo anakumbuka!!!najuuta sana!!!never do again!!!japo huwa wanaudhi sana hawa wenzetu!!!

Nyoko zako unajiona wewe upo perfect umekamilika as if ww huudhi wenzio. Nyani haoni kundule
 
Mwanamke anapigwa kwa psychologically au kwa kanga.

Ila akivuka mipaka, mpige tena kipigo kweli ila watoto na majirani wasione.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyoko zako unajiona wewe upo perfect umekamilika as if ww huudhi wenzio. Nyani haoni kundule
Min 92, matusi, lugha ya kuudhi ohh Mungu anakuona shauri yako
 
Back
Top Bottom