WirelessBrain swali lako ni zuri japo mie sio mwana uchumi ila ntajaribu kuongezea kama wachangiaji waliotangulia walivyoanza kujibu.
Kwanza kabisa, Benk Kuu ya Tanzania ndio msimamizi mkuu wa mwenendo wa kiuchumi na shughuli zote zinazohusu pesa.
Wao ndio hutangaza tenda na kusimamia mchakato mzima kutokana na vigezo walivyojiwekea. Makampuni mengi ni ya nje.
Tukirudi kwenye wazo la kuzitengeneza nyingi, kwa ufupi kiwango cha noti wanazoprint kiba mahesabu yanayoendana na hali halisi ya uchumi wa nchi. Ina maana thamani ya tshs 10,000/= iendane na huduma au kazi ya kiwango hicho. Sasa ukizitengeneza nyingi inamaana zinapatikana kirahisi bila kuzifanyia kazi stahiki, watu wengi watakua na hizo noti bila kuzalisha au kujituma. Mwisho wa siku thamani yake itashuka. Kwakuwa zipo nyingi na wengi wanazo, huduma amvayo ungeipata kwa 3,000/= unaweza kuipata kwa 10,000/= au zaidi.