Mkuu kama procedure uliyoyaeleza ni ya kweli. Hicho kiwanja ni cha kwako. Kama muuzaji aligaiwa kama urithi and at the time of sale ni hakuwa "minor", yaani below 18 years, tukianzia na law of contract ni kwamba document mliyosaini ni kielelezo tosha cha muuzaji kuwa na uwezo wa kuingia katika mkataba wa kukuuzia kiwanja kwa bei mliyokubaliana "fair price". From the moment ulipomkabidhi pesa na wewe kukukabidhi title deed ni kwamba mmeshamaliza mkataba.
Contract ingekuwa ni void ab initio kama muuzaji angekuwa ni minor, au angekuwa si mmiliki halali wa mali hiyo. Huyo kaka yao anayetaka kukurudishia hela uliyotoa mwaka 2007 ni mpuuzi. Kama mtakubaliana ni lazima ajue kuwa a shilling today is not a shilling tommorow (time value of money) na kwa kuwa wewe ni mwenye mali una haki ya kumtajia hela yoyote unayotaka kuuzia kiwanja chako kama utakuwa willing kuuza hata mara 100 ya bei uliyonunulia.
Hapo hakuna jipya na ukienda huko kwenye kikao cha usuluhishi waambie kuwa, huhitaji usuluhishi katika mali yako kama wanaona wameonewa waende mahakamani na nina kuhakikishia kuwa utashinda kwa kishindo. Suala lilipo hapo si nani atasema nini bali ni documents zinasema nini. kwa kujiandaa zaidi pitia sheria hizi kwanza
1. Law of contract ordinance, section ya who can enter into contract
2. Law of sale of goods, concentrate on when the goods are deemed to be sold
unaweza pitia na sheria ya ardhi lakini kwa hapa application yake si kubwa sana kwani ardhi is an asset na ndiyo maana hata bank unaweza kuiweka kama dhamana ya mkopo. wasikutishe hao mkuu, mchezo uliisha long time.