Wanataka kuachana kisa jina

Wanataka kuachana kisa jina

iphone 18 promax

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2012
Posts
2,915
Reaction score
2,142
Siku ya leo nmealikwa kwenda kutatua ugomvi wa watu wapendanao sasa kwa kweli naona kama vile shida tu jamaa rafiki yangu anamwanamke ambaye ndio mke mtarajiwa amejifungua mtoto wa kike cha kushangaza hajashirikishwa kuita jina la mtoto kashaangaa anapigiwa na shemeji yake kuwa mtoto tumemuita fulani sasa jamaa anajiuliza mbona mimi sijashirikishwa na mimba tumelea mwanzo mwisho jana kampigia mwanamke na kumwambia tuachane na wakati huo wiki ijao tunaenda kutoa poza kaniambia rafiki yangu nikamwambia apotezee tu jamaa hataki hivi utaratibu wa kuita jina ukoje kwa mtoto.
 
Mwambie awe ngangari, hiyo familia inaonesha ina madharau. Kwa ustaarabu wa kawaida tu ukiacha desturi zetu shemeji yako hawezi kutoa jina la mtoto wako. Asimame kama mwanaume otherwise ataolewa yeye
 
mkuu sasa mimi nashindwa kumwambia jamaa ukweli ila kamwambia mwanamke sikutaki na sikuoi tena sasa analia na kuomba msamaha eti hakujua jina aloitwa ni la msanii kisa mama mkwe kalipenda sasa mimi nataka nisiende kusuruhisha na mimi mwanamke ananisumbua nimumbembeleze jamaa na jamaa hataki kusikia inshu ya kurudiana
 
Wamempa jina la Wema?
 
Me najua kwa mila za kiafrika kama hujatoa mahari na hujaoa unakuwa huna mamlaka juu ya mtoto. Sasa jamaa yako hata posa hajapeleka anataka aanzishe vurugu. Halafu hapo anaoa mke au anaoa mtoto? Kama anaoa mke haina shida jina la mtoto atalibadilisha mbele ya safari!
 
haki ya kutoa jina ni ya baba na mama wa mtoto. huwa nachoshwa sana na wakwe kuwa na kimbelembele cha kuita majina. si wawaite majina watoto wao? kwa nini kung'ang'ania kuita jina mtoto wa mwenzio? hasa upande wa mwanaume ndo huwa wanayo hii tabia chafu
 
Kama alikuwa bado hajamuoa huyo mwanamke, hana haki ya kutoa jina ashirikishwe kutoa jina yeye kama nani?
 
pamoja na kuwa anahaki ya kushirikishwa kwenye itoaji wa jina la mtoto.lakini hiyo sababu haitoshi kumuacha mzazi mwenzie
 
ashirikishwe kama baba wa mtoto. kuoa au kutooa hakuondoi ukweli kuwa yeye ndiye baba wa mtoto

Huo upande wa "mwanaume" ndo hauna wanawake wenye kuzaa?
Kwanza ndo upande gani?
 
Haki hiyo hana kwa mujibu wa desturi na mila zetu.. ila kuna taratibu za kufuata ili aweze kuita jina analopenda mwenyewe.

Nashauri asiache kupeleka posa maana hiyo ndio forum ya kuwasilisha malalamiko yake na nini cha kufanya ili aweze kumuita jina mtoto wake.
 
pamoja na kuwa anahaki ya kushirikishwa kwenye itoaji wa jina la mtoto.lakini hiyo sababu haitoshi kumuacha mzazi mwenzie

Anajuaje kama baba wa ukweli wa mtoto ndo katoa jina hilo kisha anadanganywa ukweli ndo wamempa?
Ni wazazi gani, binti yao anapewa tu mimba from no where- aliyempa humjui kisha unakurupuka kwenda kutoa jina kwa mtoto? Its a shame kwa utaratibu wa kiafrika hadi sasa.
Na mwanaume ambaye mtoto wake kachaguliwa jina kwengine ana haki ya kumkataa!
A name carries with it a lineage (urithi wa kinasaba) heritage, customs and pride. Na kiafrika ni from a fathers lineage.
Kama baba hakuchagua jina la mtoto basi hawezi kuitwa ni wa ubini wake. Na kwa sababu jamaa hajatoa mahari upande wa binti una haki ya kumchukua huyo mtoto kabisa kama wao so jamaa anaweza kusepa zake!

huna haki ya kutoa jina kwa upande wowote ule. haki yako ni kutoa jina kwa mwanao tu na si kwa mtoto wa dada yako wala kaka yako
Upande wa kwetu kuna dada pia ,sasa tukikurupuka kutoa jina kwa mtoto wa dada tunakuwa upande wa "mwanaume" bado?
 
ashirikishwe kama baba wa mtoto. kuoa au kutooa hakuondoi ukweli kuwa yeye ndiye baba wa mtoto
Hii kali kweli, kibongo bongo kitendo tu cha kumpa mimba binti yangu bila kumuoa kwangu mimi ni tusi sembuse kumtafuta ashiriki kutoa jina?
 
Kama alikuwa bado hajamuoa huyo mwanamke, hana haki ya kutoa jina ashirikishwe kutoa jina yeye kama nani?

mkuu mimi mke ninaeishi nae nilitoa poza baada ya kujifungua na wakati yuko mimba nilipata matatizo ya kufariki kwa baba yangu siku kujifungua nilipigiwa simu na mama mtu nkaulizwa njoo uite jina nikaenda kuita jina baada ya wiki nikatoa mahali na kumuhamisha kikazi sababu tulikuwa sehemu tofauti sema inategemea na uelewa wa familia
 
hiyo sio sababu ya kumuacha msichana wa watu aseme tu kama ana lingine huyo rafiki yako
 
Anajuaje kama baba wa ukweli wa mtoto ndo katoa jina hilo kisha anadanganywa ukweli ndo wamempa?
Ni wazazi gani, binti yao anapewa tu mimba from no where- aliyempa humjui kisha unakurupuka kwenda kutoa jina kwa mtoto? Its a shame kwa utaratibu wa kiafrika hadi sasa.
Na mwanaume ambaye mtoto wake kachaguliwa jina kwengine ana haki ya kumkataa!
A name carries with it a lineage (urithi wa kinasaba) heritage, customs and pride. Na kiafrika ni from a fathers lineage.
Kama baba hakuchagua jina la mtoto basi hawezi kuitwa ni wa ubini wake. Na kwa sababu jamaa hajatoa mahari upande wa binti una haki ya kumchukua huyo mtoto kabisa kama wao so jamaa anaweza kusepa zake!

aisee! Chukua tano kabisa. Hata ningekuwa mm hapo nikuachana naye tu....... Wantapaje jina wakat baba wa mtoto yupo?! Kitendo cha kumpa wao jina inamaana wao ndio waliompa mimba mwanao........ Wakwe wengne sijui wakoje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom