Wanataaluma vyuo Vikuu waikoromea Serikali

Wanataaluma vyuo Vikuu waikoromea Serikali

Yaani mnatania kweli. Mnashuhudia dhuluma za wazi kabisa kwa taifa zikifanywa na serikali ya CCM kupitia bunge, mahakama, wizara mbalimbali, mnakaa kinywa. Leo mwaibuka kudai haki? Hiyo haki itapatikana katika mwundo upi? CCM ni ileile. Wabunge ni walewale. Katiba ni ileile tena imelainishwa vizuri zaidi kutetea maslahi mazima ya CCM. Wauza madawa ya kulevya ni walewale. Ni familia za viongozi wakuu wa nchi sasa ni nani atawakemea. Shilingi ni ileile. Imeshuka mpaka udongoni. Wabunge waliosimama kidetea kulitetea taifa wamesukumiwa mbali na wale ambao CCM haiukufanikiwa itatumia mahakama yao kuwahujumu. Nyinyi mnadai haki kutoka wapi? Haki itapatikana tu kama tutabadilisha mfumo wote. Wote kabisa. Magufuli amepita nchi nzima akijisifia kwa barabara uchwara ambazo zimemaliza kabisa nguvu kazi, yaani vijana na kuwaacha maelfu na vilema vya kudumu. Hakuna anaeuliza wala kuhoji. Tunasifikia na kushabikia ujinga ambao umatufikisha hapa tulipo. Ni kiasi kuwa watu wanalipa mamilioni ya pesa kuja Tanzania kujionea ujinga uliodumu miaka nenda geuza chini ya mfumo wa CCM. Unawezaje kumfundisha mwanafunzi ambae mfumo mzima wa taifa haujawahi kumtambua na kumpa mahitaji yake tangu akiwa mdogo? Ni nchi gani duniani ambayo haiwajali wazee, wagonjwa, watoto, maskini, vilema kama albinos, yatima, wajane, miundombinu, waalimu, madaktari, watumishi wa umma n.k? Ni nchi gani duniani ambayo inagawa bure madini, gasi, mbuga za wanyama, mazao ya misitu, ardhi, eti ipate neti za mbu, vitabu, zahanati, nk? Ni kwa nini CCM inatupa matokeo ya uwongo kabisa na kuwagandamiza wapizani mchana kweupe na sisi tunanyamaza na kushabikia tu? Amani inadumu mahali ambapo watawala wanagawana madaraka pasipo haki na watoto wao, ndugu zao, rafiki zao pasipo kujali madhara ya maamuzi yao? Wanafunzi wanaweza kusoma na kufaulu bila msingi wa elimu toka shule ya awali? Mwalimu aliyefeli kidato cha nne anaweza kugeuzwa kuwa chombo bora cha kuwaandaa watoto wa primary kuelekea sekondari? Mwalimu anaweza kufundisha bila vifaa, darasa, umeme wa uhakika, madawati, maabara, mabweni, na mazingira bora kwa ujumla? Tunajidanganya sana. Tumegeuzwa dampo la madawa ya kulevya na uasherati. Tunashabikia ujinga ambao hauna kifani na kushuhudia taifa letu likipitwa na majirani zetu huku tukijidai eti kuwakomboa na kuwashauri. Mawejifunza kutokana na makosa yao na wanasonga mbele haraka kutupita. Sisi tutajitambua lini na kuondokana na huu ujinga wa CCM na makandokando yake?
 
Back
Top Bottom