Wanataaluma vyuo Vikuu waikoromea Serikali

Wanataaluma vyuo Vikuu waikoromea Serikali

Joined
Jul 31, 2015
Posts
41
Reaction score
21
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA WANATAALUMA KUKOSA IMANI NA WATENDAJI WA SERIKALI

UTANGULIZI
Ndugu wana habari, Ni miaka miwili sasa tangu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) atoe maagizo ya kutafutia ufumbuzi hoja zilizoibuliwa na wanataaluma kupitia Umoja wa wanataaluma ASAs. Mnamo tarehe 21/08/2013 Rais wa JMT alifanya kikao na viongozi wa wanataaluma ili kusikia matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi. Katika kikao hicho maazimio mbalimbali yalifikiwa na kuwekewa mikakati ya utekelezaji jambo ambalo lilileta faraja sana kwa wanataaluma kwamba matatizo yao ya muda mrefu yangepata ufumbuzi. Kwa kuzingatia dhamira na utashi wa Mh. Rais katika kushugulikia matatizo ya wanataaluma, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ilitoa taarifa kwa umma tarehe 22/08/2013 yaani siku moja baada ya kikao hicho juu ya yaliyojiri. Katika taarifa hiyo kwa umma, Mh. Rais alielekeza maeneo nane ya kufanyiwa kazi kwa kushirikiana na viongozi wa wanataaluma na wadau wengine kupitia uratibu wa katibu Mkuu wa wizara ya Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma. Maagizo hayo kwa mujibu wa Kurugenzi ya habari ikulu yalikuwa kama ifutavyo
(1)-- Serikali, kupitia Wizara ya Fedha, ihakikishe kuwa Bajeti ya Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki vya Umma ambayo imekuwa inapungua mwaka hadi mwaka inarejeshwa kwenye viwango vya zamani mapema iwezekanavyo, na kwamba bajeti hiyo isiwe inapungua mwaka hadi mwaka kama ilivyo sasa.
-
(2)-- Nyongeza ya fedha hizo itumike kuboresha mazingira na miundombinu ya kufundishia katika Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki vya Umma.- Shughuli hiyo ianze kwa kufanyika tathmini ya kujua vipaumbele, na kuandaa mpango mahsusi wa utekelezaji.
-
(3)-- Madai ya wanataaluma yatokanayo na stahili zao, na ambayo yamehakikiwa yalipwe kwa awamu na kazi ya uhakiki wa madeni mengine iendelee.
-
(4)-- Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ishirikiane na Viongozi wa Vyuo hivyo kupitia upya Muundo wa Utumishi (Scheme of Service) wa wanataaluma kwa lengo la kuuboresha kwa kuzingatia mahitaji maalum ya wanataaluma.
-
(5)-- Vyuo Vikuu vya Umma virejeshewe uhuru wa kuajiri wanataaluma moja kwa moja -kama ilivyokuwamwanzo badala ya kufanywa na Sekretarieti ya Ajira Serikalini.
-
(6)-- Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ikutane na Viongozi wa Muungano wa Wanataaluma haraka iwezekanavyo ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya upandishaji vyeo wanataaluma na nyongeza -ya mishahara ya kila mwaka.
-
(7)-- Utaratibu wa Mikopo ya Ujenzi wa Nyumba kwa ajili ya watumishi wa Serikali ulioanzishwa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa JMT, uhusishe pia Wanataaluma wa Vyuo Vikuu. Aidha, Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki vyenye ardhi ya kujenga nyumba za kuishi wanataaluma vijadiliane na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii yenye wanachama kwenye vyuo hivyo ili kuona uwezekano wa Mifuko hiyo kujenga nyumba za kuishi za wanataaluma kwenye maeneo hayo.
-
(8)-------------- Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Mdhibiti wa Mifuko hiyo washirikiane haraka na Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki vya Umma pamoja na Serikali ili kulipatia ufumbuzi tatizo la uwasilishaji wa michango ya pensheni ya wanataaluma.
-
UTEKELEZAJI WA MAAGIZO
Ndugu wanahabari, katika maagizo hayo nane jambo ambalo limetekelezwa kikamilifu ni moja tu yaani agizo namba tano (5)la Vyuo Vikuu vya Umma kurejeshewa uhuru wa kuajiri wanataaluma moja kwa moja bila ya kazi hiyo kufanywa na Sekretarieti ya Ajira Serikalini.
Katika maagizo yote ya Mh. Rais, moja kubwa linalowagusa wanataaluma na ambalo lingeondoa matatizo mengi ni suala la Muundo wa Pamoja wa Utumishi wa Wanataaluma (harmonized Scheme of Service).- Utekelezaji wa agizo hili ulikuwa na sehemu au hatua kubwa mbili ambazo ni uundwaji na utekelezaji wa muundo husika.
Kuwa na muundo wa pamoja wa utumishi wa wanataaluma kulitokana na sababu kadhaa kubwa ikiwa ni pamoja na kuzingatia mahitaji maalumu ya wanataaluma na upekee wao (Uniqueness) ambao una utaratibu tofauti na watumishi wengine wa umma wa kutathminiwa kwa ajili ya upandishaji vyeo hasa matumizi ya machapisho (publications). Pili ni kuondoa tofauti kubwa zilizopo miongoni mwa miundo ya utumishi ya vyuo husika kuhusu kuajiri, kutathmini na ulipaji mishahara. -Katika hatua hii ya uundaji wa muundo wa pamoja wa wanataaluma, wanataaluma wa Chuo kikuu kishiriki cha Elimu Mkwawa tunakiri kushiriki kikamilifu kuandaa muundo huo kwa kadiri ya maagizo ya Rais. Hata hivyo mchakato wa kuunda Muundo husika ulikamilika tangu tarehe 17/03/2014 katika kikao cha wadau wote waliohusika kuuandaa.- Viongozi wa wanataaluma tulishiriki katika kuujadili, kuupitisha kwa wadau wetu na kuutolea mapendekezo mbalimbali ya uboreshaji katika hatua zote muhimu za utekelezaji wa maagizo ya Mh. Rais.

Utekelezaji wa Muundo wa Pamoja
Ndugu wanahabari, kama ilivyoelezwa hapo juu, mchakato wa kuunda muundo huu ulikamilika Machi, 2014 na mategemeo yalikuwa ni kutekelezwa kuanzia Julai 2014 katika bajeti ya 2014/2015.- Msajili wa Hazina alitoa waraka na 2 wa 2014 kuelekeza menejimenti za- vyuo namna ya utekelezaji wa Muundo huo wa pamoja. Hata hivyo, Msajili huyo huyo wa hazina alitoa waraka mwingine Septemba, 2014 kusitisha kutekelezwa kwa Muundo husika kwa madai ya kuwepo malalamiko kutoka kwa baadhi ya wadau. Wanataaluma- kukubaliana na maamuzi yaliyofanyika na mamlaka husika kwa matarajio kwamba muundo mpya ungeanza kutekelezwa mwaka mpya wa fedha 2015/16. Kwa matumaini hayo Julai 2015 Msajili wa hazina alitoa waraka wa mishahara ambao ulionekana kuzingatia muundo huu wa pamoja, lakini cha ajabu kumekuwa na visingizio vingi vinavoonyesha kutupiana mpira baina ya msajili wa hazina na utumishi. Hali hii inapelekea tujiulize maswali mengi sana hasa ya inakuwaje maagizo ya Rais yanapuuzwa kwa kiasi hiki?
-
Ndugu wanahabari, katika kikao chake cha dharula kilichofanyika septemba 7, 2015, wanataaluma wa Chuo kikuu kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na mambo mengine -walitafakari kwa kina jambo hili na kuazimia yafuatayo;
Wanataaluma wamekosa imani na watendaji wa serikali katika kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Rais tarehe 21 Agosti 2013 na kwa hiyo wamechoka kula maneno ya watendaji wa serikali bali wanataka kuona maelekezo ya Rais yanatekelezwa haraka.
Wanataaluma wanaamini wanaidai serikali madai mengi sana na ya muda mrefu sana ikiwa ni pamoja na posho za nyumba, pesa za likizo, nyongeza ya mishahara ya -mwaka, kupandishwa vyeo, posho za madaraka na za kujikimu kwa waajiriwa wapya, lakini wamekuwa wavumilivu na wazalendo vya kutosha na hivyo wameaazimia kwa pamoja kwamba; kama wasipopata uhakika kutoka utumishi au hazina juu muundo wa pamoja uliowianishwa wa utumishi wa wanataaluma kufikia tarehe 5/10/ waatasitisha shughuli zote za kitaaluma kwa muda ili kupata nafasi ya kuanza vikao (Extended meetings) kujadili mustakabali wao.
Tunaiomba serikali kupitia Utumishi na Ofisi ya msajili wa hazina ituwekee bayana majibu sahihi juu ya nini kinakwamisha muundo huu mpya wa utumishi kuanza kutumika. Ni bora tuishi tukijua utekelezaji wa muundo huu hauwezekani kuliko kuishi tukisubiri kitu ambacho serikali haiko tayari kukitekeleza.
Kutokana na ufuatiliaji wa karibu tuliofanya bila mafanikio kwa takribani miaka miwili sasa tumepata wasiwasi wa kuwepo kwa dalili za hujuma na ucheleweshwaji wa makusudi. Hali ambayo inatukosesha uvumilivu kwani tunaamini serikali ingeweza kufanya vizuri na kwa kasi zaidi kama kweli ina dhamira ya dhati ya kutekeleza muundo huu. Kwa kuzingatia haya yote tuliyoyaeleza, tunamwomba Mhe. Rais, kama mamlaka ya juu iliyohusika kuagiza kuanzishwa na utekelezwaji wa Muundo huu wa Utumishi kuingilia kati ili kunusuru mchakato huu.

Hitimisho
Ndugu wanahabari, Wanataaluma wa Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Mkwawa wametafakari kwa kina sana jambo hili kwa kuzingatia masilahi mapana ya nchi yetu na wanaamini kuwa Muundo huu wa Utumishi uliowianishwa wa wanataaluma ndio muundo bora ukilinganishwa na muundo unaotumika sasa. Utekelezwaji wa Muundo huu utaondoa kero nyingi ambazo zilibainishwa na kufanya Mhe. Rais aagize uanzishwaji na utekelezwaji wa Muundo huu. Tutaendelea kupigania kuwepo kwa muundo huu wa utumishi wa wanataaluma wa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki vya umma ili kuweka mazingira bora ya kazi yaliyo sawa miongoni mwa wanataaluma katika ngazi zote katika vyuo vikuu vya umma.

Tunatahadharisha pia kuwa, wanataaluma hatutakuwa tayari kuanza mwaka mpya wa masomo 2015/2016 kabla ya muundo huu wa utumishi kuanza kutekelezwa. Tunafahamu na tunaamini kuwa hii ni HAKI ya wanataaluma wa vyuo vikuu vya umma kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutoa mchango wao wa kulijenga Taifa letu.

-Mwenyekiti- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - ------------------------ Katibu Mkuu

Samson John Mgaiwa- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -Philpo John Gwevu
 
Yaani Wasomi pamoja na Watu wote wanaojitambua KWELI WAMEICHOKA CCM,sasa kwanini Serikali isiwasikilize Wanataaluma na Wasomi? Ndio maana msimamo wao pamoja na CWT ni Kumchagua Lowassa na kuipigia kura UKAWA.
 
Hili ni andiko la wanataaluma/wasomi?

nini tofauti kati ya mwanataaluma na msomi? Acha kuwa na narrow mind. Think like a great thinker ndio uulize swali lako. Otherwise go lumumba st. to beg your posho!
 
Dunian pote, Hakuna yeyote Wasomi Waite wanataalum walishiriki ktk vuguvugu la Mabadiriko.

Waomi wanaeaza Projects Poket/briefcase. Hatuwategemei sana Kwenye vita Hii dhidi ya CCM.

Tuwaachr watoe press Release ambozo kimsingi, Hawapo serious.
 
Tupo serious mkuu. Azma yetu ni moja tu, kuliondoa nduli fisiem. Hii press release inalenga kuwatia hamasa wadau wa taaluma ili wafanye kweli panapo tarehe 25 mwezi huu..

Haya mafisiem hakuna popote yalishawezafanikisha.. yamekalia wizi, fitna na hujuma tu.. tena yanafanya hayo yote dhidi ya nchi yao wenyewe.. huu ni usaliti wa hali ya juu na yafaa yanyongelewe mbali..

Changamoto za wanataaluma ni nyingi mno.. fikiria unaingia ukumbi wa mihadhara, umeme hakuna (ni giza) vipaza zauti vimeharibika au vimezimika kwa ajili ya mgao wa umeme (hakuna usikivu) wanafunzi wengi hawana mkopo na hawana uhakika wa shule maana wengi wameshindwa kusajili kozi husika (mawazo tele), wengi hawajakula chakula kizuri na uwezo wa kufuatilia lecture unashuka.. zaidi, darasa/program ina wanafunzi 350, mhadhiri uwafundishe wote hao, utoe tests zisizopungua mbili, assignments zisizopungua mbili, lab reports zisizopungua mbili, lab tests zisizopungua mbili, final exam ya masaa yasiyopungua tatu, usahihishe vyote hivyo, utoe majibu.. duh.. lazima uwe chizi.

Tukidai malipo yanayolingana na kazi, dana dana kibaoo..

Sasa tunasema hivi... fisiem mtaisoma namba mwaka huu.. panga pangua lazima muipate full wrath ya wanataaluma..

Ombi ni kwenyu ndugu zetu msiofanya kazi vyuo vikuu, tuhamasishane, kitanda kwa kitanda mtu na mtu.. tuioneshe fisiem hasira zetu zote.. TUMECHOOOOOOKKAAAAA
 
Yaani Wasomi pamoja na Watu wote wanaojitambua KWELI WAMEICHOKA CCM,sasa kwanini Serikali isiwasikilize Wanataaluma na Wasomi? Ndio maana msimamo wao pamoja na CWT ni Kumchagua Lowassa na kuipigia kura UKAWA.

Ukitaka kujua wameichoka CCM ,tazama hii

[h=2][/h]
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye viwanja vya mikutano vya Peoples kuhutubia wakazi wa Singida mjini.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi Singida mjini kwenye uwanja wa mikutano wa Peoples ambapo aliwaambia wakazi hao kuwa ataibadilisha Singida na kuufanya kuwa mji wa Biashara, pia aliwaambia vijana wanafunzi wa vyuo kuwa atahakikisha wanapata mikopo kwa wakati, mikopo kwa vijana na wakina mama .
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wakazi wa Singida mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Mgombea wa Urais kwa kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akitoa salaam za shukrani kwa Mbunge wa Singida mjini anayemaliza muda wake Ndugu Mohamed Dewji (kushoto) na Mkuu wa mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea wa ubunge wa jimbo la Singida kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Peoples.
Mbunge wa Viti Maalum mtarajiwa Aysha-Rose Matembe akiwasalimu wakazi wa Singida mjini waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Kutoka kulia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Mwigulu Nchemba akipiga push ups pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Singida mjini Ndugu Mussa Sima (katikati) na Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu.
Wakazi wa Singida mjini wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida Diana Chilolo akihutubia wakazi wa Singida mjini waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Iramba Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa Singida mjini waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea ubunge wa jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba akihutubia wakazi wa Singida mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ndugu Lazaro Nyalandu akihutubia wakazi wa Singida mjini kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mbunge wa Jimbo la Singida mjini anayemaliza muda wake Ndugu Mohamed Dewji akihutubia wakazi wa Singida mjini kwenye mkutano wa kampeni za Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Umati wa wakazi wa Singida mjini waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
Msafara wa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili kata ya Sepuka .
Mwigulu Nchemba akimkaribisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipowasili Sepuka.
Wakazi wa Sepuka wakishangilia ujio wa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kabla ya kuhutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya shule ya msingi Kiomboi Bomani.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Mhe. Mwigulu Nchemba akihutubia kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Kiomboi Bomani.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa shule ya msingi Kiomboi Bomani.
Wakazi wa Kiomboi wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiondoka eneo la Mto Ndulumo baada ya kukagua daraja ambalo kwa sasa halitumiki baada ya kuathirika na mafuriko ambapo aliwaahidi wananchi wa kijiji cha Msingi Kidi kuwa daraja hilo litatengenezwa mapema
 
Jamani wanataaluma kichinjio mnacho. Tarehe 25.10.2015 tuwang'oe CCM kupitia sanduku la kura, mwana mkaidi hafaidi mpaka ck ya idi.
 
Safi sana Magufuli, Hapa ni kazi tu.
 
Mafundisho tamko limemzidi akili kaamua kumwagia uzi kijani. Kaza kichwa hicho soma tamko mkuu.
 
Sijamuelewa vizuri mleta mada, wanataaluma anaozungumzia ni wepi hasa? Si wale wale waliomtunuku Kikwete uprofesa ndani ya miaka hiyo hiyo miwili wanayotaja.

Wanataaluma gani ambao tangu mwanzo hamkujua kuwa mnadanganywa, kana kwamba hamjui udanganyifu wa serikali ya Kikwete wakati miaka yote wanafunzi wenu wanagoma kwa madai yanayofanana na hayo hayo yenu.

Naishauri serikali mkianza tu hivyo vikao vyenu muitiwe polisi iwakung'ute mpaka mnyooke maana inaonekana mlimpa Rais uprofesa ili awatekelezee hayo madai yenu, na baada ya kuwashtukia mnataka kuanza vikao, mnazidiwa hata na walimu wa shule za msingi za Kenya?
 
nini tofauti kati ya mwanataaluma na msomi? Acha kuwa na narrow mind. Think like a great thinker ndio uulize swali lako. Otherwise go lumumba st. to beg your posho!
Hakuna tofauti ndiyo maan nimeweka "mkato" kati ya maneno hayo mawili.
 
Dunian pote, Hakuna yeyote Wasomi Waite wanataalum walishiriki ktk vuguvugu la Mabadiriko.

Waomi wanaeaza Projects Poket/briefcase. Hatuwategemei sana Kwenye vita Hii dhidi ya CCM.

Tuwaachr watoe press Release ambozo kimsingi, Hawapo serious.

Mkuu hawa Oliver Tambo, Stive Biko,walter sesulu,malcom X,Martin Luther king Jr hao ni baadhi ya wasomi walioshiriki mabadiliko bila kumsahau karl max alitembea na taa ya chemli mchana kuwahamasisha watu waamke.usizungumzie dunia mkuu wakati huna data..
 
Nilikuwa sijui kama vyuo vikuu sasa wanaweza kuajiri ma-lecturer na maprofesa wao moja kwa moja bila kupitia serikalini. Ndugu yangu aliapa kamwe asingepeleka maombi yake kupitia kwa huyu Hawa Ghasia. Alisema kufanya hivyo ni kujidhalilisha tu na akaamua kujikita katika kilimo cha Nyanya kule Turiani. Ngoja nimshtue apeleka maombi UDSM.
Huyo ndugu yako hafai kufundisha hata chekechea!Hiyo si sababu muhimu kabisa kuzira kuomba kazi,labda kama ungetwambia kilimo cha nyanya kimemshinda!
 
Nimefurahi rais wetu anapewa ulinzi wa haja ...Hapa kazi tu
 
Back
Top Bottom