Wanasiasa wenye damu ya uongozi

Wanasiasa wenye damu ya uongozi

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,208
Siasa nchini imejaa ulaghai na ubabaishaji mwingi. Watu wengi wanaingia siasa kwa bahati mbaya tu kwani hawana mvuto wala karama zozote za uongozi.

Wengine wamefuata huko maslahi na si kuwaongoza au kuwawakilisha wananchi bungeni. Kwa wengine, siasa ni njia nzuri ya kuzifanya biashara zao hatamu zisitawi.

Watu wachache ambao walikuwa na mvuto na damu ya uongozi ni pamoja na Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE. Huyu alikuwa na damu ya uongozi kweli kweli.
Alikuwa akiongea watu wanamsikiliza kwa dhati ya mioyo yao. Hata alipotaka kufikisha ujumbe kwa jamii hata uwe wa kukera kiasi gani, alitumia lugha ya staha na badala ya kununa, watu walikuwa wanacheka. Nasema NYERERE alikuwa kiongozi zaidi kuliko mtawala.

Baadhi ya watawala ( sio viongozi) wa sasa, wakianza kuongea ndio kwanza watu wanatoka kwenda kuvuta sigara!! Na wengine huzima redio!

Mzee Mwinyi nae alikuwa na karama ya uongozi kwani alitawala kwa busara. Kwamba ana damu ya uongozi, sina hakika.

Viongozi wengine wenye damu ya uongozi ni JK, Samuel Sitta _Rip, William Lukuvi, Dk Mahiga, Cheyo Mapesa, Nape Nnauye na Dk Slaa.
Wengine ni mama Sitta, Mahiza, Mkuchika, Halima Mdee, Mbatia, Hassan Zungu nk...

Wasio na mvuto kabisa wala damu ya uongozi ni Pinda, Ndugai, Makinda, Makonda, Dk Bilal, Mkapa, Dk Shein, Seif Idd, Sumaye, Polepole, Mpogolo, Anthony Mavunde, Mbarawa na Jafo.

Wengine ni Juliana Shonza, Ajela Kairuki, Freeman Mbowe, Maalim Seif, Joyce Ndalichako, Stella Manyanya, Ole Nasha, Jenister, Kangi, Hapi, Kubenea nk.

Kama taifa kuna kazi ya ku groom viongozi wenye karama. Utitiri wa wasiasa wababaishaji unawabania vijana wenye karama na mvuto wa uongozi. Rushwa na au kukomoana imeharibu kila kitu.
 
Umetumia critelio zip kuwacategoriz

Yohana mbatizaji, abatizaye kwa moto kama hujamtaja kwa makusudi , hujamtendea haki.
 
Napenda sana Mwanasiasa halafu ni Mwanaharakati, mfano Tundu Lissu.

Hawa ndio wanaohitajika kwa Africa, Mimi sinaga za kusema kuna watu wamezaliwa kuwa Viongozi.

Ila kuna watu wamezaliwa kuwa Wanaharakati.
 
Jiwe limeangukia pale kwa bahati mbaya. Nafasi ilikuwa ya Joka la mdimu. Ona sasa mambo ya kishamba yanayoendelea. Mchunga ngo'mbe sio presidential material kabisa.....
 
Suleman Jaffo ni smart sana yule anafit sehemu yoyote, Jaffo ni Lukuvi ajaye

Mavunde hamna kitu pale anatumia nguvu nyingi sana.
 
Tumekusikia mkuu na wenyewe wamekufahamu pia je unashauri nn kitendeke ili wajirekebishe kwani tumewazoea pamoja ya kwamba huwakubali,kumbuka wanadamu wana mapungufu kila watakapo simama na kusimamia,alafu pia wamechaguliwa sidhani kama walio wachagua wamefanya makosa au wamejichagua ,tuanze apo kwa changuzi zinazo waeka hapo walipo
 
Back
Top Bottom