Wanasiasa Wasijenge Ufa Kati ya Watumishi wa Umma na Wananchi

Ozzanne Issakwisa

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
288
240
Mahusiano mazuri kati ya mtoa huduma na mtumiaji (nitamwita mwananchi), hasa katika suala la kuaminiana ni hatua ya awali katika kutoa huduma bora.

Wanasiasa wanawajibika kwa wananchi, lakini pia wanawajibika kwa kauli au matendo yanayopunguza kuaminiana kati ya mtoa huduma na mwananchi.

Inafahamika kuwa watumishi wachache wa umma, wamepoteza imani waliyokuwa wamejijengea na hivyo hata kazi zote nzuri zinazofanywa na watumishi wengi waadilifu hazithaminiwi wala kutambulika.

Inahuzunisha kuona juzi kumetokea mgomo wa watumishi wa afya, ambao wanadai walivamiwa na wananchi na wakakashifiwa kwa maneno mbalimbali na zaidi wakatishiwa maisha. Sidhani tunahitaji kufikia huko, yaani wananchi tuvamie hospitali na kuanza kupanga taratibu!!!

Binafsi siamini kama utakuwa na amani kukaa kwenye kiti cha kinyozi anayekunyoa kwa wembe, na wakati huo huo mkawa na mikwaruzano mikali. Athari za kutokuaminiana.

Wanasiasa wajenge mahusiano mema kati ya wapiga kura na watumishi wa umma. Vyombo vya sheria vitumike kutoa haki, lakini kikubwa wasisahau kwamba kuna tume za kimaadili zilizopo kisheria kwa baadhi ya kada, zinazoweza kutoa haki. Mfano madaktari wana Medical Council of Tanganyika, ambayo mara ya mwisho niliisikia ikiwafutia leseni madaktari waliogoma (Naamini bado ziko active na kama zimekufa zifufuliwe, maana hizo zinapaswa kusimamia maadili na uwajibikaji, ila sasa ziwezeshwe zifanye maamuzi kwa kasi ya Hapa kazi tu).

Mwananchi, Serikali/Wanasiasa na Mtumishi wa umma kila mmoja asijifanye malaika. Ajitathmini.

Mwananchi ajue ukiendesha chombo cha moto bila kufuata sheria za barabarani utapata ajali, inayoweza kuchukua uhai wako hata kama utapelekwa kwa Dr. Ben Carson. Huo ni wajibu kabla ya kupata haki.

Serikali isikwepe share zake za lawama, na kwamba ilikuwa haipeleki fungu la kutosha linalostahili katika sekta ya afya, na kwamba ilijisahau sana kwa sababu viongozi wengi walikuwa wanatibiwa nje.

Mtumishi wa serikali ajitathmini kama anastahili kulipwa mshahara kila mwezi. Bila shaka anajua wajibu wake ni kumhudumia mwananchi, ili aondoke ofisini kwake akiwa na tabasamu.

Ndugu zangu madaktari na manesi, sote tunajua hamna uwezo wa kutupa uhai, lakini ukiongeza kwa mgonjwa hata sekunde moja ya kuishi, ni furaha kwa kila mtu. Tunajua hatuwezi kuwafanya malaika, lakini mkikutana nasi mtutibu kwa upendo, hata kama sisi wananchi au serikali tumewaghafirisha.

Tusijenge ufa tukaoshindwa kuuziba.
 
Ukitaka haya yaishe,kwanza serikali itimize wajibu wake,na pia wanasiasa waache kujificha nyuma ya watumishi,pale wanaposhndwa kudeliver wawajibike badala ya kuwasingizia watumishi
 
Watumishi wa umma bana shida tupu. Mshahara laki 6 matumizi million, halafu woga wa kutumbuliwa unasabaisha mastrees halafu unaambiwa ukatibiwe muhimbili dokta anakuambia kanunue dawa hapo Msd ambayo ni mali ya serikali.
 
Watumishi wa umma bana shida tupu. Mshahara laki 6 matumizi million, halafu woga wa kutumbuliwa unasabaisha mastrees halafu unaambiwa ukatibiwe muhimbili dokta anakuambia kanunue dawa hapo Msd ambayo ni mali ya serikali.
Mishahara yenyewe inatosha?
 
Siasa isiingilie taaluma, unamlazimisha daktari akutibu akikupa chloroquine wakati unaumwa kifua Nani wa kulaumiwa
 
Nilisema na nasema tena, fani ya utabibu iwe ya kisayansi, tiba mbadala, kienyeji au kiimani ina command respect toka kwa jamii popote pale. Jamii inawaheshimu sana watu hawa kwa sababu rahisi kabisa - wanashughulika na uhai. Nani anayependa kuugua na hatimaye kufa? Hakuna, kimbilio ni matabibu.

Matatizo kati ya serikali/wanasiasa na wahudumu wa afya isiwe ndo kigezo cha wananchi maskini wanyonge kuombwa rushwa, kutolewa
lugha chafu, kunyanyaswa, kupuuzwa na hata kusababishiwa vifo ambavyo vingeweza kuepukwa. Kumbuka hapa wanaopatwa na haya ni wananchi maskini wanyonge. Wenye pesa kwa pesa zao hupata huduma sawasawa na mafunzo walioyapata vyuoni.

Ukiona popote pale wananchi masikini wanyonge wamewainukia watumishi wa afya fahamu tatizo ni watumishi wa afya na si vinginevyo.

Pia kibaya zaidi ni viongozi wa sekta ya afya kukaa kimya pale wahudumu wa afya wanapovunja miiko ya kazi zao. Hawajui? La hasha wanajua sana.

Nawashauri viongozi wa afya wapiganie wanayoyataka bila wahudumu wa afya kuvunja miiko ya kazi zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom