DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo, amesema kuwa hoja za kisiasa kuhusu bei ya pamba nchini zinapotosha umma, kwa kuwa tatizo halisi si bei bali ni uzalishaji mdogo wa zao hilo miongoni mwa wakulima wa Tanzania.
Akizungumza Jumanne, Juni 24, 2025, bungeni jijini Dodoma, Nyongo amesema kuwa bei ya pamba ni matokeo ya soko la kimataifa, lakini kiwango kidogo cha uzalishaji ndicho kinachowafanya wakulima wengi kutopata faida kubwa.
“Ukienda India, wakulima huzalisha hadi kilo 2,500 kwa hekta moja, tofauti na Tanzania ambako uzalishaji bado uko chini. Hilo ndilo tatizo la msingi tunalopaswa kulitatua,” amesema Naibu Waziri Nyongo.
Amesema kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha tija ya uzalishaji kupitia tafiti bora za kilimo, usambazaji wa mbegu zenye ubora, pamoja na kuwawezesha wakulima kupata pembejeo kwa wakati.
Aidha, amewataka viongozi wa kisiasa kutotumia changamoto ya bei kama njia ya kuchuma mtaji wa kisiasa, bali washirikiane na serikali kuwaelimisha wakulima juu ya teknolojia za kisasa za kilimo chenye tija, ili pamba iwe na manufaa makubwa kwa wakulima na taifa kwa ujumla.