Wanasiasa waenguliwa Tume ya Katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa waenguliwa Tume ya Katiba Mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by abdulahsaf, Mar 30, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tuesday, 29 March 2011

  [​IMG]
  Mwandishi Wetu

  MUSWADA maalumu wa kuunda Tume ya kukusanya maoni na kupendekeza muundo wa Katiba mpya ya Tanzania, unatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la Aprili, mwaka huu.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa muundo wa tume hiyo hautawashirikisha wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Madiwani wala kiongozi yeyote wa kisiasa.

  Tume hiyo inayotarajiwa kuwa na wajumbe 30, itaundwa na Rais Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein na wajumbe wake watakuwa ni wanataaluma, hususan wanasheria na kwamba suala la jinsia litazingatiwa.

  Taarifa hizo zinaeleza pia kuwa Tume itaundwa na idadi sawa ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na Visiwani na inatarajiwa kuwa na majukumu mbalimbali ikiwamo kuwahamasisha watu kujua maana na muundo wa Katiba.

  Majukumu mengine ya tume hiyo yaliyotajwa kwenye muswada huo ni kukusanya maoni kutoka kwa wananchi, kuchunguza na kuainisha muundo wa Katiba kulingana na mifumo ya kisiasa, kidemokrasia, uongozi, sheria za kiutawala na Serikali.

  Mara baada ya Bunge kupitisha muswada huo, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuusaini na kuiunda haraka iwezekanavyo tume hiyo ili ifikapo Juni mwaka huu ianze kazi yake.

  Kamati hiyo itatoa rasimu ya katiba hiyo mpya ikipendekeza pia muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano utakavyokuwa.

  Mchakato wa kuunda tume hiyo unakuja baada ya Rais Kikwete kuwataka wananchi kuwa watulivu akisema suala hilo litaratibiwa kwa umakini ili kuwa na katiba bora ambayo itawasaidia Watanzania kwa muda mrefu.

  Tamko la Rais Kikwete la kuunda tume hiyo ndilo lililozima wimbi la madai ya Katiba mpya lililoshika kasi miongoni mwa watu wa kada mbalimbali ikiwamo wanasiasa, wasomi na wananchi wa kawaida.

  Katika mijadala hiyo, Katiba iliyopo imeelezewa kuwa imepitwa na wakati na haiendani na mahitaji ya mazingira ya sasa ya nchi.

  Vuguvugu hilo lilianza mara baada ya Uchaguzi Mkuu, Novemba mwaka jana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kudai kuwa Katiba ya sasa haitoi haki ya kidemokrasia kwenye uchaguzi.
   
 2. Muro

  Muro Senior Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haitoshi kuunda tume,iwe na wanasiasa au la, kinachotakiwa na wananchi ni katiba mpya kabla ya 2013 na siyo 2015,hivyo time frame ni muhimu sana,na smart objectives kuwa nini kifanyike lini na kwisha ni lini siyo maneno maneno tu.
   
 3. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ya idadi sawa ya wajumbe kutoka Bara na Visiwani mimi sikubaliane nayo. Rule of majority lazima ipewe nafasi kwenye hii process. Of course lazima wananchi kwa ujumla wao wapate nafasi ya kupiga kura ya kukubali katiba mpya. Sasa bara kuna watu wengi zaidi ya Visiwani na ikitokea watu wa bara wakapiga kura ya maamuzi tofauti na wale wa Visiwani ni nini kitatokea?
   
 4. T

  Taso JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  "Wanasiasa waenguliwa Tume..." kwani walikuwemo kwenye Tume?

  Madai ya uongo na kweli yasiyoenda shule.
   
 5. s

  smz JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa maana hiyo Tume itawajibika kwa raisi, au?
   
 6. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Mi naona hiyo tume itakuwa na watu wengi kupita kiasi. Labda kwa sababu sijui hadidu za rejea za tume hiyo, lakini pamoja na hayo, watu 30 ni wengi sana, hasa ukifikiria hali ya nchi kiuchumi ambapo wafadhili hawajatoa pesa walizoahidi katika bajeti.
   
 7. G

  Gurti JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani hoja ya katiba mpya ilianzishwa na wanasheria? Wanasiasa lazima wawepo. Hatutaki changa la macho.
   
 8. m

  mob JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  kama idadi sawa zanzibar in wakazi wangapi na bara in wakazi wangapi?
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,519
  Likes Received: 5,655
  Trophy Points: 280
  Hili la wanasiasa kutokuwepo limekaa kisiasa zaidi hata zitolewe sababu zipi.nguzo za maendeleo kwa mujibu wa azimio la arusha(kama sikosei) ni watu,ardhi na siasa safi.kuna mambo ya kisiasa lazima kundi lao lihusike direct maana wapo wanasiasa wanasheria n.k.fatilia uteuzi wa hao wataalam kama hujakuta wote wanakadi za ccm!
   
 10. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280

  Cha maana iwe inakidhi mahitaji yetu kwa sasa!! Kama wataleta sarakasi, hatukubali!!
   
 11. De Javu

  De Javu JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kinachojadiliwa hapa ni Katiba ya MUUNGANO, Muungano ni wa sehemu mbili baina ya Tanganyika na Zanzibar ili kutenda haki ni lazima iwe hivyo. Katiba iliyopo ndio inayopigiwa kelele kua haitendei haki upande mmoja,pia hao wajumbe wataangalia pande wanazotoka kuona mahitaji/maslahi/mapungufu ya kila upande. Kumaliza matatizo ni lazima pande mbili zilizoungana zikae upya kujadili aina ya muungano/katiba utakaonufaisha pande zote.
   
 12. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Bila shaka yoyote. Hii ndiyo hali halisi maana mwenye kisu ndiye anayekula nyama. Shida ya tume yetu ni kule kuundwa na rais kwa vyovyote vile tumeitawajibika kwake. Hapo ndipo siasa inapokuwa na nguvu hata kama ndani ya tume hakuna wanasiasa. Tuombe heri
   
 13. H

  Haika JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Wanasiasa ni watu wapi hao?
  mfano mtu kama Lamwai anaweza kuwamo?
   
 14. R

  Rangi 2 Senior Member

  #14
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Eeh Bwanae! Bunge ndio liainishe sifa za watanzania wanaopaswa kushiriki katika Tume ya katiba mpya.
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu hivi na wewe kama great thinker kweli umeingia kwenye huu mkenge na mchezo wa kunguni kutoka juu ya shuka kujificha chini ya shuka?. Huu ni mchezo wa kitoto ambao CCM wanataka kuucheza ili kulinda masilahi yao. Huwezi kusema wanasiasa wasiwemo wakati wateuzi wa tume hiyo ni wanasiasa tena wote wa kutoka CCM. Hakuna jipya hapa kama mteuzi ni Mwanasiasa tume hiyo itakuwa answerable kwa mwanasiasa na hakuna mtu atakayekuwa tayari kuteua watu ambao hana imani kuwa watamlindia masilahi yake. Kinachotakiwa kufanyika hapa zaidi ya hili changa la macho ni.

  Ilitakiwa Muswada upelekwe bungeni wa kutaka tume hiyo iundwe na
  1. Mwakilishi wa kila chama chenye mbunge mmoja au zaidi bungeni
  2. Kila taasisi ya dini yaani waislam na wakristo watoe wawakilishi wawili wawili
  3. TANGO, au umoja wa NGO utoe mwakilishi mmoja
  4. Taasisi za elimu ya juu za serikali zitoe wawakilishi wawili
  5. Taasisi za elimu ya juu za binafsi zitoe mwakilishi mmoja
  6. Serikali ya Jamhuri itoe wawakilishi wawili na ya Zanzibar wawili

  Kazi za hii tume ambayo katika muswada huo na budget yake iwekwe kabisa itakuwa ni

  1. Kumchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na katibu wa tume miongoni mwao ambao kazi zao hazitakuwa beyond organising public hearings na kukusanya maoni ambapo baada ya kila mkutano kila mjumbe anapewa kopi yake na kazi ya katibu ni kuwa na maoni yote kwa muda wowote na wakati wowote electronically, I mean kwenye video na muhtasari kwenye hard copy.

  2. Tume hii iwe huru kuajiri wanasheria na wataalam waliobobea katika fani mbalimbali katika kuhakikisha kuwa kazi yao inaenda vizuri wakiwemo wa kisheria, IT, fedha etc.

  3. Kuyaunganisha mawazo ya wananchi wote na kuyafanyia tathmini ili kuondoa yanayopingana na kisha kuchapisha rasimu yake kama katiba na kuirudisha tena kwa wananchi kuijadili kwa totality na kuongeza ama kufanyia marekebisho baadhi. Na baada ya hapo inapigiwa kura na wajumbe wa tume hiyo kwa kigezo kuwa kilichomo ndani ya rasimu ni maoni solely ya wananchi na hakuna kipengele chochote kilichopachikwa either na wanatume au nje. Ili Rasimu ipite ni lazima wajumbe wote waikubali si kwa kuwa yaliyomo yamewafurahisha la bali kwa kuonesha kuwa kumbukumbu zao za maoni ya wananchi na kilichomo havitofautiani.

  4. Baada ya hapo rasimu hiyo inaanza kunadiwa kwa wananchi kwa ajili ya kuipitishwa kwa referendum na tume ya kusimamia referendum hiyo inachaguliwa na kuundwa na Tume hiyo kwa wajumbe wote kuwakubali watendaji wa tume kwa sauti moja.

  Wakati wa referendum sasa hapo watu wanaweza kuchukua upande na kazi ya tume inakuwa imefikia kikomo pale tu rasimu hiyo inapokuwa imepitishwa na asilimia si chini ya 60% wananchi ya wapiga kura wote walioandikishwa na tume ya uchaguzi ya referendum ambayo itapata maagizo yote kutoka kwenye tume ya katiba, Mchakato huu utatakiwa uwe umekamilika mwishoni mwa 2012 ili kutoa nafasi kwa vyama na serikali kujiandaa na uchaguzi wa 2015 kwa kutumia katiba mpya.

  HUU MCHAKATO UKIFANYIKA NDIYO UTAKUWA UMEWAENGUA WANASIASA KATIKA KUINFLUENCE OUTCOME YA TUME HII NA SI KWA KUCHAGULIWA NA SHEIN AU KIKWETE.
   
 16. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2011
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Nakubaliana na wewe mkuu kwa silimia 100%, hiyo tume ikichaguliwa kwa mfumo uliopendekeza ndiypo itaitwa TUME HURU, vinginevyo kama mswada unavyotaka itakuwa Tume ya Kikwete, na itakwenda kuwakilisha mawazo ya Kikwete hata siku mmoja haitapeleka wazo la mwananchi la kumpunguzia madaraka Kikwete!! hiyo ni ndoto. Ikichaguliwa na Kikwete na Sheni italinda masilihi ya watawala waliopo sasa ambayo ndiyo inalalamikiwa.
   
 17. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hili linaelekea kuwa jambo zuri kabisa kwa mustabali wa Taifa letu na natumaini wenye nia hjema kwa taifa wataunga mkono mia kwa mia. Wasi wasi wangu ni pale serikali itakapotofautiana, kama inavyoelekea, na wazo hili tufanyeje kwa mbinu za amani hadi kufanikiwa? Tuna tatizo kubwa mikononi mwetu na elimu ya uraia inahitajika sana watu waelewe haki zao na wawe huru kushiriki kuamua watakavyo na si kuburuzwa tu.
   
 18. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuhusu uwakilishi sawa wa wajumbe kutoka bara na visiwani ni kichekesho mbali na kutilia mkazo haja ya kuwa na serikali. Ni ukweli kwamba hatuwezi kuwa na katiba moja ikatosha maeneo mbali mbali ya nchi yo yote hapa duniani na ndiyo maana kila nchi ina Katiba yake kukidhi mahitaji kwa mustakabali wa nchi yao. Kama tutarithia serikali tatu ni hapo tu uwakilishi sawa wa wajumbe kutoka bara na visiwani una maana kwa maswala ya muungano tu. Vinginevyo, kama visiwani wenyewe wanavyosema kuwa Zanzibar si sehemu ya Tanzania bali ni nchi yenye mipaka waliotaja; yaani Tanzania bara pia nu nchi yenye mipaka iliyobaki chini ya Muungano jambo ambalo hadi sasa lina baraka za serikali ya Muungano na ya Zanzibar. Yaani hatima ya katiba mpya 50% yake iwekwe chini ya reheni ya watu wachahe hivyo yenye % ndogo sana ya uwiano kieneo na wingi wa watu kati ya bara na visiwani. Hapa akili ipo? Kama nakosea munielemishe. Vinginevyo kama mvutano huu ni mkubwa na ajili ya amani ya nchi zetu bara na visiwani basi uwakilishi wa wajumbe sawa iwe pale tu inapohusu mambo ya muungano - wazungu wanasema in the unlikely event that worst goes to worst. Niko tayari kukosolewa kwa hoja tu.
   
Loading...