Wanasiasa waenguliwa Tume ya Katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa waenguliwa Tume ya Katiba Mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by nickname, Mar 30, 2011.

 1. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Tuesday, 29 March 2011 21:20
  Mwandishi Wetu
  MUSWADA maalumu wa kuunda Tume ya kukusanya maoni na kupendekeza muundo wa Katiba mpya ya Tanzania, unatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la Aprili, mwaka huu.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa muundo wa tume hiyo hautawashirikisha wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Madiwani wala kiongozi yeyote wa kisiasa.

  Tume hiyo inayotarajiwa kuwa na wajumbe 30, itaundwa na Rais Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein na wajumbe wake watakuwa ni wanataaluma, hususan wanasheria na kwamba suala la jinsia litazingatiwa.

  Taarifa hizo zinaeleza pia kuwa Tume itaundwa na idadi sawa ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na Visiwani na inatarajiwa kuwa na majukumu mbalimbali ikiwamo kuwahamasisha watu kujua maana na muundo wa Katiba.

  Majukumu mengine ya tume hiyo yaliyotajwa kwenye muswada huo ni kukusanya maoni kutoka kwa wananchi, kuchunguza na kuainisha muundo wa Katiba kulingana na mifumo ya kisiasa, kidemokrasia, uongozi, sheria za kiutawala na Serikali.

  Mara baada ya Bunge kupitisha muswada huo, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuusaini na kuiunda haraka iwezekanavyo tume hiyo ili ifikapo Juni mwaka huu ianze kazi yake.Kamati hiyo itatoa rasimu ya katiba hiyo mpya ikipendekeza pia muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano utakavyokuwa.

  Mchakato wa kuunda tume hiyo unakuja baada ya Rais Kikwete kuwataka wananchi kuwa watulivu akisema suala hilo litaratibiwa kwa umakini ili kuwa na katiba bora ambayo itawasaidia Watanzania kwa muda mrefu.

  Tamko la Rais Kikwete la kuunda tume hiyo ndilo lililozima wimbi la madai ya Katiba mpya lililoshika kasi miongoni mwa watu wa kada mbalimbali ikiwamo wanasiasa, wasomi na wananchi wa kawaida.Katika mijadala hiyo, Katiba iliyopo imeelezewa kuwa imepitwa na wakati na haiendani na mahitaji ya mazingira ya sasa ya nchi.

  Vuguvugu hilo lilianza mara baada ya Uchaguzi Mkuu, Novemba mwaka jana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kudai kuwa Katiba ya sasa haitoi haki ya kidemokrasia kwenye uchaguzi.

  My Take: Nionavyo mimi ni kweli wanasiasa wanatakiwa wakae pembeni wasiingilie mchakato wa katiba mpya.Wanasiasa wanatakiwa washiriki mchakato wa katiba mpya kwa kutoa maoni na pia uwahamasisha wananchi watoe maoni kwa Tume ya Katiba.Hii itasaidia mchakato wa Katiba mpya uende haraka na Katiba mpya ipatikane kabla ya 2015.
   
 2. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu hivi na wewe kama great thinker kweli umeingia kwenye huu mkenge na mchezo wa kunguni kutoka juu ya shuka kujificha chini ya shuka?. Huu ni mchezo wa kitoto ambao CCM wanataka kuucheza ili kulinda masilahi yao. Huwezi kusema wanasiasa wasiwemo wakati wateuzi wa tume hiyo ni wanasiasa tena wote wa kutoka CCM. Hakuna jipya hapa kama mteuzi ni Mwanasiasa tume hiyo itakuwa answerable kwa mwanasiasa na hakuna mtu atakayekuwa tayari kuteua watu ambao hana imani kuwa watamlindia masilahi yake. Kinachotakiwa kufanyika hapa zaidi ya hili changa la macho ni.

  Ilitakiwa Muswada upelekwe bungeni wa kutaka tume hiyo iundwe na
  1. Mwakilishi wa kila chama chenye mbunge mmoja au zaidi bungeni
  2. Kila taasisi ya dini yaani waislam na wakristo watoe wawakilishi wawili wawili
  3. TANGO, au umoja wa NGO utoe mwakilishi mmoja
  4. Taasisi za elimu ya juu za serikali zitoe wawakilishi wawili
  5. Taasisi za elimu ya juu za binafsi zitoe mwakilishi mmoja
  6. Serikali ya Jamhuri itoe wawakilishi wawili na ya Zanzibar wawili

  Kazi za hii tume ambayo katika muswada huo na budget yake iwekwe kabisa itakuwa ni

  1. Kumchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na katibu wa tume miongoni mwao ambao kazi zao hazitakuwa beyond organising public hearings na kukusanya maoni ambapo baada ya kila mkutano kila mjumbe anapewa kopi yake na kazi ya katibu ni kuwa na maoni yote kwa muda wowote na wakati wowote electronically, I mean kwenye video na muhtasari kwenye hard copy.

  2. Tume hii iwe huru kuajiri wanasheria na wataalam waliobobea katika fani mbalimbali katika kuhakikisha kuwa kazi yao inaenda vizuri wakiwemo wa kisheria, IT, fedha etc.

  3. Kuyaunganisha mawazo ya wananchi wote na kuyafanyia tathmini ili kuondoa yanayopingana na kisha kuchapisha rasimu yake kama katiba na kuirudisha tena kwa wananchi kuijadili kwa totality na kuongeza ama kufanyia marekebisho baadhi. Na baada ya hapo inapigiwa kura na wajumbe wa tume hiyo kwa kigezo kuwa kilichomo ndani ya rasimu ni maoni solely ya wananchi na hakuna kipengele chochote kilichopachikwa either na wanatume au nje. Ili Rasimu ipite ni lazima wajumbe wote waikubali si kwa kuwa yaliyomo yamewafurahisha la bali kwa kuonesha kuwa kumbukumbu zao za maoni ya wananchi na kilichomo havitofautiani.

  4. Baada ya hapo rasimu hiyo inaanza kunadiwa kwa wananchi kwa ajili ya kuipitishwa kwa referendum na tume ya kusimamia referendum hiyo inachaguliwa na kuundwa na Tume hiyo kwa wajumbe wote kuwakubali watendaji wa tume kwa sauti moja.

  Wakati wa referendum sasa hapo watu wanaweza kuchukua upande na kazi ya tume inakuwa imefikia kikomo pale tu rasimu hiyo inapokuwa imepitishwa na asilimia si chini ya 60% wananchi ya wapiga kura wote walioandikishwa na tume ya uchaguzi ya referendum ambayo itapata maagizo yote kutoka kwenye tume ya katiba, Mchakato huu utatakiwa uwe umekamilika mwishoni mwa 2012 ili kutoa nafasi kwa vyama na serikali kujiandaa na uchaguzi wa 2015 kwa kutumia katiba mpya.

  HUU MCHAKATO UKIFANYIKA NDIYO UTAKUWA UMEWAENGUA WANASIASA KATIKA KUINFLUENCE OUTCOME YA TUME HII NA SI KWA KUCHAGULIWA NA SHEIN AU KIKWETE.
   
 3. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Asante,nimeukubali uxhambuzi wako,hakika ni mzuri na umenibadili mawazo.Big up
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  TUNAPENDA KUONA UCHACHE ZAIDI WA SERIKALI (EXECUTIVE) KWENYE MCHAKATO
  WA KATIBA MPYA NA TUME HURU ZA UCHAGUZI BARA NA VISIWANI


  Wa-Tanzania mtakubaliana na mimi kwamba tumekwepo na uwepo wa serikali kila mahali katika maisha yetu kiasi kwamba kwenye suala la katiba sasa ni sharti watupishe tuwe mstari wa mbele na wao wabakie tu kama wawezeshaji tu.

  We have had just TOO MUCH OF GOVERNMENT IN OUR LIVES and so let them stay away from intruding into defining of our destiny as a people and how we want to be governed. This is an area that donor countries need to intervene in assisting us in seeing lesser and lesser of government executives in constitutional making and more and more of ordinary citizenry taking active part not only in giving views but more so in managing every other stage and decision-making apparatus appended to to the processes in the area.

  Hakika, wakati tunasema kuwa ni habari njema 'Mtoto wa Mkulima' kuni-prove wrong kw kutokupigisha zaidi danadana endapo kweli muswada utafikishwa bungeni mwezi Kama ambavyo alivyotuahidi kama taifa, bado kuna mambo ambayo ni sharti yarekebishwe hata kabla ya muswada wenyewe kutinga bungeni, kama vile:

  1. TUME HURU YA BUNGE KUUNDWA KATIBA MPYA


  Tunaposema kwamba hatutaki tume ya Rais kuhusu mambo ya katiba na kwamba badala yake tunasema tunahitaji Tume Huru ya Bunge kushughulikia maswala ya Kuratibu maswala ya kuundwa kwa Katiba Mpya na Tume Huru za Uchaguzi Bara na Visiwani maana yetu kama taifa ni kwamba TUNANATAKA MASUALA YOTE YA KATIBA KUSIMAMIWA NA WANANCHI WENYEWE kama washika dau muhimu zaidi kupitia vikundi mbali mbali.

  Ni kwamba tunahitaji people-centred constitutionalisation process kwa namna ambapo wananchi hatushiriki tu kwa kutoa maoni bali pia kwa kusimamia na kutole maamuzi sisi wenyewe na wala si rais, waziri wala wabunge tena; hatupendi kabisa kuingiliwa kwa namna yoyote ile na executive kwenye appointments of the officers, Kusimamiwa na wao wala Kuwajibika kwa Watawala. Hili tunaomba lieleweke wazi mapema na kuzingatiwa.

  Muswada huo uongeze zaidi na zaidi uwepo wa washikadau wote kwenye ngazi zote za maamuzi na utendaji wa Tume Huru ya Bunge ya Katiba Mpya na katika mchakato mzima na kuteuliwa, kugharamiwa na kuwajibika kwa bunge tu.

  2. RATIBA YA MCHAKATO NA HADIDU ZA REJEA KWA TUME YA KUUNDWA KATIBA MPYA

  Masuala hayo mawili yafanyike na mkutano mkuu wa taifa kuhusu katiba mpya kisha kupelekwa bungeni kurasmishwa kuwa ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa huo muswada wa bunge kuundwa kwa katiba mpya.

  Hapo maana yake ni kwamba tunasema si rais, waziri, chama cha siasa wala bunge IS COMPETENT ENOUGH TO ARRIVE AT those two primary guiding aspects kama kweli tunakusudia katiba mpya kupata senses of OWNERSHIP and LEGITIMACY by ordinary Tanzanians and not project of the executive Dr Ali Mohamed Shein ninayo imani kubwa sana kwamba hutochelea kuona mantiki na nguvu ya hoja hii.

  Let's NOT feel that you are intent to ABDUCT and ULTIMATELY IMPOSE on us the once people-intitiated constitutional reform agenda to be undertaken YOUR WAY and not the one that we all need.

  3. SOURCES OF FUNDING FOR THE ENTIRE CONSTITUTIONAL REFORM PROCESS

  Tunawaomba nchi wahisani wajitokeze kugharamia mchakato mzima ili kesho na kesho kutwa kusiwepo mambo ya kukwamishana katika hatua zozote zile kwamba hakuna fedha.

  4. UJUMBE KATIKA TUME HURU YA BUNGE KUUNDWA KWA KATIBA MPYA

  Dhana potofu kwamba wajumbe sharti wawe wanasheria itupiliwe mbali maana kinachatafutwa hapa SI KWENDA KU-ARGUE A CASE bali ni kwenda kupokea maoni ya wenye nchi hivyo sioni ni kwa msingi upi mlango wa katiba ufungwe kwa watu wa taaluma moja tu wakati hata taaluma tu ya ukocha wa kandanda nayo itaguswa na sheria mpya na ni wadau muhimu mle ndani pia. Hili lifikiriwe vema na kwa haraka.

  Isitoshe, hata kama condition ingalibakia kama ambavyo tayari tunakataa hapa juu ya nani awe mjumbe wa tume, nadhani hao wanasheria ambao si wanasiasa vile vile watahitajika kupendekezwa na washikadau na wala si kazi ya rais wa Zanzibar na wa Muungano kufanya hiyo kazi kwa maana kwamba watakapoliachiwa basi chama tawala CCM ambacho ndicho kimewafadhili katika nyadhifab hizo kitakua kimepata undeserved advantage over other stakeholders na hivyo kushinda dhamira ya mfumo mpya wa siasa za vyama vingi kwa mtindo wa ushindani wakati wote.

  In fact, by all intents and purposes the two presidents are the leading face of the country's most divergent PARTISAN politics that MUST NEVER assume in entirety and single-handedly the roles in putting the country's blueprint to guide future political competition spectrums with a mark of utmost good faith and impertiality.

  NB: THE TOTAL SUM BOTTOMLINE OF EVERYTHING ON CONSTITUTIONAL REFORM AGENDA MUST AT ALL TIMES REMAIN THAT EVERYTHING BE DONE TO THE FINEST MEANING COME 2014 SO THAT THE 2015 GENERAL ELECTIONS ARE CONDUCTED WITHOUT A COMPROMISE UNDER THE NEW CONSTITUTION!!
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Wakati hayati Mwalimu Nyerere alituambia kuwa JK hafai kiutu uzima sisi hatukusikia na wa kulaumiwa ni Ben Nkapa.
   
Loading...