Wanasiasa wabashiri bajeti ya kiinimacho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa wabashiri bajeti ya kiinimacho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 9, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  SIKU moja kabla ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkullo kusoma bajeti ya serikali ya mwaka 2010/11, wanasiasa wameeleza kuwa bajeti hiyo inaweza kuwa kiini macho.

  Miongoni mwa wanasiasa wanaotegemea hayo ni mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba ambaye alisema hayo baada ya kufanya tathmini katika taarifa za awali zilizotolewa na waziri huyo kwa wabunge kuhusu bajeti hiyo itakayokuwa ya Sh11.1 trilioni katika mijadala kwenye kamati.

  “Kwa kweli mara nyingi tunakuwa na bajeti mbovu nchini lakini mwaka huu ni bajeti ya kiini macho,” alisema Profesa Lipumba, ambaye ni mchumi.

  Alisema awamu ya kwanza ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (Mkukuta) haukufanyiwa makadirio tangu mwanzo na ulipokuja kufanyiwa makadirio ya bajeti ikagundulika kuwa serikali haikuwa na fedha za kuutekeleza.

  “Kwa hiyo Mkukuta huu haukufanikiwa na huu wa awamu ya pili haujafanyiwa makadirio, jambo ambalo litasababisha ugumu katika utekelezaji wake,” alisema Profesa Lipumba.

  Alifafanua kuwa ugumu huo utaongezeka zaidi kutokana na mapato ya serikali kupungua na uamuzi wa wahisani kuzuia theluthi moja ya mchango wao kwenye bajeti kuu. Hata hivyo wahisani wamesema kuwa wataendelea kusaidia Mkukuta.

  “Sisi tulitegemea kwamba sekta ya madini hasa dhahabu itatoa mchango mkubwa katika kukuza pato la taifa, lakini kutokana na taarifa za awali za Waziri Mkullo hakuna mabadiliko yoyote,” alisema Profesa Lipumba.

  “Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa pato la taifa kuzidi kuanguka mwakani kwa sababu huu ni mwaka wa uchaguzi. Ukitoa mishahara ya wafanyakazi fedha nyingi zitaenda kugharamia uchaguzi,” aliongeza Profesa Lipumba.

  Alisema hata wabunge hawatapata muda wa kutosha kuijadili bajeti hayo, badala yake wataijadili kwa wiki tano na kuipitisha.

  Lipumba alisema ili tuweze kuwa na bajeti yenye tabasamu na inayotekelezeka kwa Watanzania, tulipaswa kuwa na mjadala wa wataalamu wa uchumi kuhusu mafanikio na matatizo ya Mkukuta wa awamu ya kwanza kabla ya kwenda kwa wa awamu ya pili.

  “Lakini ipunguze matumizi mabovu kwa kuwa zaidi ya asilimia 40 ya matumizi ya serikali ni mabovu. Serikali ya Norway ilitoa dola 60 milioni za Kimardekani katika mradi mmoja wa serikali, matokeo yake dola 30 milioni zilitumiwa kifisadi,” alisema Profesa Lipumba.

  Alitaka kufanyika kwa tathimini ya matumizi ya serikali ili kugundua matumizi mabovu kwa lengo la kuzifanya fedha hizo kuwatumikia Watanzania kiuchumi na kijamii.

  Naye katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samuel Ruhuza alisema wananchi wategemee machungu makubwa ya bajeti ya mwaka huu.

  “Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja thamani ya shilingi ya Kitanzania imeanguka kwa asilimia 30, hili ni anguko kubwa sana,” alisema Ruhuza.

  “Mwaka jana dola moja ya Kimarekani ilikuwa ni sawa na Sh1,200 za Kitanzania, lakini hivi sasa dola imepanda thamani kulinganisha na shilingi na kufikia Sh1,500 kwa dola moja,” aliongeza Ruhuza.

  Alisema bajeti yetu inakuwa kwa kujikongoja na sasa takwimu zinaonyesha kuwa inakuwa kwa asilimia 16 tu.

  “Pamoja na hayo serikali imeshindwa kubana matumizi, imekuwa na matumizi makubwa na mabovu, huku pato la taifa likizidi kuanguka,” alisema Ruhuza.

  Alisema kuongezeka kwa matumizi makubwa na mabovu ya serikali kumesababisha mfumuko wa ajabu wa bei za bidhaa muhimu na kufanya hali ya maisha kwa Watanzania kuzidi kuwa ngumu.

  “Hakuna cha maisha bora kwa kila Mtanzania wala bora maisha kinachoonekana hapa ni kuumia tu na wananchi wasitarajie nafuu yoyote,” alisema Ruhuza.

  Alisema pengo la kipato kati ya waliyonacho na wasiokuwanacho linazidi kukua na kibaya ni kwamba masikini anazidi kuwa masikini na tajiri anazidi kuwa tajiri.

  “Kitu kikubwa ambacho kinanitisha ni kwa serikali kukopa kama mtu wa kawaida katika benki ya Stanbic.

  Je hawa jamaa wakikiuka masharti, serikali itawezaje kuwawajibisha wakati yenyewe inafadhiliwa,” alisema Ruhuza.
  Alisema amefurahia kitendo cha wahisani kupunguza fungu la fedha katika misaada yao, kwa kuwa serikali itatia akili na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.

  Wanasiasa wabashiri bajeti ya kiinimacho
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  kazi kweli kwenye hii Serikali Ufisadi,Wizi, na Rushwa ndio unazidi siku hata siku kazi kwetu sisi watu wa hali ya chini na walala hoi tutazidi kuumia na Matajiri ndio wanazidi kutajiri Ee Mwenyeezi Mungu tuokowe sisi Masikini Ameen.
   
Loading...