Wanasiasa - Video hii ya North Mara na Barrick mmeiona?

Wanasiasa - Video hii ya North Mara na Barrick mmeiona?

Akili kumkichwa. Tuamue sasa, saa ya ukombozi ni sasa
Mkuu inasikitisha sana yani wenzetu wa Toronto Marekani wanatusaidia kuandamana maana huku tukiandamana tunaambulia kipigo na wengine kuuliwa na Polisi
 
Nakumbuka issue hii iliongolewa sana hata bungeni lakini magamba hayana jipya,Huu si wakati tena wa kujadili na dalili za watu kukata tamaa zinaonekana Tanzania nzima. Mara,majita anzisheni kuogopa huku tunazidi kutuangamia.Mh.Zitto ulikuwemo kwenye kamati za kurekebisha mikataba ,Je ni mingapi imerekebishwa.JK hivi kwa nini unakaa kimya wakati watu wanaangamia.

OOHHH kumbe tatizo ni sisi wenyewe hatutaki kuamka na kuyaona mambo jinsi yalivyo,Pamoja na DR. wa ukweli Slaa kuwaelimisha watanzania lakini bado watanzania wameendelea kuwa kondoo. Hali inatisha na wahanga ni wengi sana wanaoadhirika na uwekezaji sio hao tu wa tarime lakini tuna vijana wanaojua sheria wameingia bungeni na ni wapiganaji wazuri.

Chadema endeleeni kupambana ndani na nje ya bunge ipo siku moja Wadanganyika wataelewa kuwa wanadanganywa na mabadiliko yatakuwa lazima.CDM kazeni buti elimu kwa wingi mpaka kieleweke NA WOGA WOTE UISHE TUIKOMBOE NCHI YETU
 
duh!
Hii inatisha, hivi wanaharakati wetu wako wapi? Wapi deus kibamba,wapi mama ananilea nkya,wapi francis kiwanga and co?
Inaumiza sana, uchunguzi wa wabunge uchwara wa magamba hautatusaidia kitu, kama wanaparurana kwa posho ya 70k tzs je marushwa manene ya barick wanayaruka kweli? Inahitaji ujasiri wa kiungu kupambana na uharamia huu....

Kuna watu wengine wanasema eti hatuwezi kuwafanya kitu kwa kuwa tulisign mkataba, sidhani mkataba ulijumuisha ukatili huu??!
Kama nikiwa rais nitakuwa dictator for at least 3 yrs kuwashughulikia wenye nia ovu dhidi ya raia wangu...ntafunga watu wote wanaonyamazia hali hii, hakuna cha mahakama wa nini...kama kuna watumishi wa issues za mazingira wanashinda kwenye viyoyozi halafu mie niwaache kisa utawala wa sheria!..nyambaf.
Watumishi wa mazingira wote wapo dar na bado viwanda vinatiririsha majitaka kwenye makazi ya watu i.e. Tbl,ktm n.k kwa nini?? Kwa nini??
Agriiiiiiiiiiiiiiiiiii!ahuuuuuuuuuuuuuu! Napata hasira.


usiulize wote hao wako wapi, jiulize na wewe unaweza fanya nini kwa ajili ya kupinga ukatili huu?
 
Back
Top Bottom