Wanasiasa tuache unguchiro

Wanasiasa tuache unguchiro

Alloyce PR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2020
Posts
704
Reaction score
801
"Hebu tafakari:

Mwanasiasa anasimama mbele ya wafuasi wake na kuanza kuwaponda viongozi wa Serikali kuwa hawana akili au ni wajinga, akidai hawawezi kuleta maendeleo; wakati huo huo, huko anakotoka ameshindwa hata kuwahamasisha na kuwawezesha vijana wa chama chake walau kujiajiri. Katika mazingira kama hayo, ukiitwa 'nguchiro' una sababu gani ya kulalamika?

Ni muhimu kwa wanasiasa kutambua kuwa mjinga huvutiwa na matusi, kejeli, na kila aina ya maneno yaliyojaa upuuzi. Hata hivyo, mtu mjanja na mwerevu huvutwa na hoja zenye mashiko, wala si makelele yasiyo na tija kama ya nguchiro." — Alloyce, P.R.
 
Sema nchi hii Nyerere na Mwinyi walikurupukia mfumo wa vyama vingi tu watanzania walikuwa hawajawa tayari kuvipokea.

Sasa kama wewe ulichoonesha hapa ni ujinga mtupu. Sababu bado uelewi maana ya chama Cha upinzani ni nini.

Unataka kije kikusifie tu kisa unatawala huo sio upinzani huo ni ushirika wenza. Jifunze siasa kijana ni sayansi kama sayansi nyingine. Watch dog ndio sayansi ya upinzani kosea nikukosoe Ili nigain popularity. Huu sio uadui ni mfumo tu wa siasa. Shida vijana wa ccm kila kitu mnpanick
 
Utter nonsense!

Watawala ndio custodians wa resources zote za taifa hili. Hawana excuse yoyote kwa kushindwa kwao kuwaletea watu maendeleo.
 
Sema nchi hii Nyerere na Mwinyi walikurupukia mfumo wa vyama vingi tu watanzania walikuwa hawajawa tayari kuvipokea.

Sasa kama wewe ulichoonesha hapa ni ujinga mtupu. Sababu bado uelewi maana ya chama Cha upinzani ni nini.

Unataka kije kikusifie tu kisa unatawala huo sio upinzani huo ni ushirika wenza. Jifunze siasa kijana ni sayansi kama sayansi nyingine. Watch dog ndio sayansi ya upinzani kosea nikukosoe Ili nigain popularity. Huu sio uadui ni mfumo tu wa siasa. Shida vijana wa ccm kila kitu mnpanick
Huu ndio Unguchiro ninaosema, husomi, unakurupuka ku comment.

Kuna utofauti ya kujenga hoja na kejeli na matusi. Kama unashindwa kuelewa utofauti wa kujenga hoja na matusi basi hiyo siasa yako ni ile siasa ya wanawake kusutana kwenye vikao vyao.
 
Nenda Kenya hapo jirani yenu kila siku nchi inasonga kwa kejeli, matusi tena kutoka kwa viongozi na waliowai kuwa viongozi lakini halizuii nchi yao kwenda mbele.

Kwenye ulimwengu wa siasa kejeli, matusi nk ni kitu Cha kawaida sana usipandisne acidi bure.
Samia aliwahi sema huyu Simba kwenye cage kwa kuwa hatulii muiteni Tundu Lissu. Ko Lissu aibuke aseme Samia kanikeji au kanitukana?. Ommy Dimpozi mbele ya Samia aliwaisema dhambi zako abebeswhe Lissu ulisikia Lissu anammahind Ommy.

Jifunze, siasa bila vijembe, kejeli na matusi hainogi. Una mengi ya kujifunza kwenye ulimwengu huu kuhusu political arena approach ili usiwe unapandisha sukari ovyo sio kila kitu kinajengewa hoja vingine ni burudisha Kambi.
 
"Hebu tafakari:

Mwanasiasa anasimama mbele ya wafuasi wake na kuanza kuwaponda viongozi wa Serikali kuwa hawana akili au ni wajinga, akidai hawawezi kuleta maendeleo; wakati huo huo, huko anakotoka ameshindwa hata kuwahamasisha na kuwawezesha vijana wa chama chake walau kujiajiri. Katika mazingira kama hayo, ukiitwa 'nguchiro' una sababu gani ya kulalamika?

Ni muhimu kwa wanasiasa kutambua kuwa mjinga huvutiwa na matusi, kejeli, na kila aina ya maneno yaliyojaa upuuzi. Hata hivyo, mtu mjanja na mwerevu huvutwa na hoja zenye mashiko, wala si makelele yasiyo na tija kama ya nguchiro." — Alloyce, P.R.

View: https://youtube.com/shorts/qOANi7gjoqw?si=voZtSPxkW-59wog3
 
Kuna mambo machache ya kutafakari ili tusichanganye 'kunoga kwa siasa' na 'ufanisi wa siasa':

Burudani vs. Maendeleo. Ni kweli Kenya wana siasa za kejeli na 'matusi' ya kisiasa, lakini tujiulize; je, nchi inasonga mbele kwa sababu ya matusi hayo, au inasonga mbele licha ya matusi hayo? Mara nyingi, kelele hizi hufunika mijadala muhimu ya kimaendeleo na kuwafanya wananchi washangilie 'punchlines' badala ya kuhoji mikataba, deni la taifa, au huduma za kijamii.

Tofauti ya 'Kijembe' na 'Matusi'. Kuna utofauti mkubwa kati ya kumuita mpinzani 'Simba aliyefungiwa' (kejeli ya kisiasa/metaphor) na kutukana utu, familia, au maumbile ya mtu. Kejeli inaleta msisimko (spice), lakini matusi ya nguoni yanashusha hadhi ya uongozi na yanaweza kupandikiza chuki ya kudumu miongoni mwa wafuasi wa chini ambao hawana 'ngozi ngumu' kama viongozi wao.

Kenya hiyo hiyo unayoitolea mfano, siasa za kejeli na kashfa mara nyingi zimeishia kwenye mivutano ya kikabila na kijamii ambayo imekuwa ikigharimu nchi hiyo kila uchaguzi. Sisi Tanzania, siasa zetu mara zote zilikuwa zikijikita katika umoja na staha (National Civility) kabla ya Unguchiro kuanza.

Tukichanganya hoja vs. 'Kufurahisha Kambi' siasa itabadilika kuwa 'Comedy Show'. Mwanasiasa akitumia 90% ya muda wake kutoa burudani za kejeli, mwisho wa siku anashindwa kujenga hoja za kisayansi na kitakwimu zinazotatua changamoto za wananchi.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kama ni wendawazimu wasiojali wananchi wanaolipa kodi ili serikali iendelee kuwepo watukanwe tu, hawana maana yeyote ya kuwa hapo walipo. Mijitu milafi na imejaa kiburi ni takataka kwa kweli.
 
Yamkini hutembei hii Tanzania mkuu, kwa wanaotembea hii Tanzania, yapo mengi makubwa ambayo yanaonyesha kodi zinaenda wapi, na mikopo inaenda wapi.

Mara nyingi wanaoendeshwa kwa hisia ni wale ambao kwanza wamezaliwa kanyaga twende, wameishi kanyaga twende, anasikiliza usiasa zaidi na hajui usiasa ni nini.

Watu wa aina hiyo wapo wengi sana. Sawa na mtu tokea amezaliwa yupo porini, kazi kusubiri tarumbeta alafu anakwambia miaka 60+ ya Uhuru bado tunazungumzia Choo.

Ambapo, Kenya asilimia kubwa wanajisaidia vichakani kama Ngedere, hadi Mzee Ruto alipoingia anahamasisha masuala ya vyoo na Nyumba.

Usipojithamini na kujielewa kisha ukawa na akili ya kushikiliwa pasipo kujua, utaumia sana duniani hapa hadi unapowekwa kaburini.

Ukitaka kujua uhalisia wa hili, Mtafute Babu au Baba yako au Kaka yako au Mama yako au Dada yako mwenye umri sawa na Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) muulize akifa leo jamii yake itamkumbuka kwa kitu gani kama Hazina, akikujibu pasipo kuleta stori mpongeze.
 
Naomba sifa za huyo Nguchiro na tabia zake ili nipime mzani kabla sijachangia uzi.
 
Hasira na kuanzisha ugomvi (Aggression)

Kama vile nguchiro asivyoogopa kupigana na mnyama mkubwa, wanasiasa Nguchiro huwa wenye "hasira za kisiasa." Mara nyingi wanatafuta migogoro na vyombo vya dola au serikali hata pale ambapo mazungumzo yangeweza kusaidia, ni watu wanaopenda "fujo" ili wapate kiki.​

Uharibifu (Calculated Chaos)

Nguchiro anapovamia banda la kuku na kuua wengi bila kuwala wote, ni sawa na siasa za "ubomoaji." Wanasiasa Nguchiro hushambulia kila juhudi ya serikali (hata zile zenye tija) bila kutoa mbadala, hili hupelekea kutaka kuharibu sifa ya nchi au uongozi uliopo kwa manufaa ya kisiasa tu.​

"Ubinafsi" na ugomvi wa ndani

Nguchiro ni mchoyo wa chakula chake. hii inafanana na migogoro ya madaraka ndani ya vyama ambavyo vina Unguchiro. Mara nyingi huonekana wakigombea ruzuku, nafasi za uongozi, au umaarufu (ego), ambapo kiongozi mmoja hataki mwingine ang’are, hali inayopelekea vyama kupasuka au kudhoofika.​

Kelele bila matokeo (Noise vs. Action)

Kundi la nguchiro lina kelele nyingi sana. Ni sawa na Wanasiasa Nguchiro walivyo wenye "kelele nyingi za majukwaani" na kwenye mitandao ya kijamii, lakini matokeo yao ya kiutendaji au mabadiliko ya sera na mitazamo ni madogo ikilinganishwa na kelele wanazopiga.​

Ujanja na "Wizi" wa Mayai

Nguchiro ana mbinu za kipekee za kuiba mayai. Hii ni sawa na siasa za fursa (opportunism). Wanasiasa Nguchiro huvizia matatizo ya wananchi (kama vile kupanda kwa bei ya bidhaa au kero za kijamii) na kuyatumia kama "mtaji" wa kisiasa badala ya kutafuta suluhu ya kudumu ya matatizo hayo.​

Harufu na Alama (Identity Politics)

Nguchiro huashiria eneo lake kwa harufu kali. Vivyo hivyo, Wanasiasa Nguchiro hujenga "ukuta wa kiitikadi" au wa kikanda ambao unawatenga watu wengine. Wanatengeneza mazingira ambayo ukiwa nje ya "harufu" ya chama chao, huonekana kama adui, jambo linalogawa wananchi.​
 
"Hebu tafakari:

Mwanasiasa anasimama mbele ya wafuasi wake na kuanza kuwaponda viongozi wa Serikali kuwa hawana akili au ni wajinga, akidai hawawezi kuleta maendeleo; wakati huo huo, huko anakotoka ameshindwa hata kuwahamasisha na kuwawezesha vijana wa chama chake walau kujiajiri. Katika mazingira kama hayo, ukiitwa 'nguchiro' una sababu gani ya kulalamika?

Ni muhimu kwa wanasiasa kutambua kuwa mjinga huvutiwa na matusi, kejeli, na kila aina ya maneno yaliyojaa upuuzi. Hata hivyo, mtu mjanja na mwerevu huvutwa na hoja zenye mashiko, wala si makelele yasiyo na tija kama ya nguchiro." — Alloyce, P.R.
Screenshot_20260427-082911~2.png
 
Yamkini hutembei hii Tanzania mkuu, kwa wanaotembea hii Tanzania, yapo mengi makubwa ambayo yanaonyesha kodi zinaenda wapi, na mikopo inaenda wapi.😅😅😅😅😅 MATAKO YANA KUWASHA WEWE
 
Huu ndio Unguchiro ninaosema, husomi, unakurupuka ku comment.

Kuna utofauti ya kujenga hoja na kejeli na matusi. Kama unashindwa kuelewa utofauti wa kujenga hoja na matusi basi hiyo siasa yako ni ile siasa ya wanawake kusutana kwenye vikao vyao.
Ww utakuwa ni mjinga fulani, hoja zinaongelewa nyingi, lakini ubongo wako huwa unachakata kejeli chache kwenye hizo hoja. Kwenye siasa kejeli na kebehi ni sehemu ya kumtoa mshindani wako kwenye reli. Usitegemee wapinzani wa kweli watakusifia kwa lolote, labda uweke ushahidi siku ccm waliwasifia wapinzani.
 
Kwa bahati mbaya kwako unasoma na huelewi maana ya kilichoandikwa, hivyo inakupelekea moja kwa moja kuwa Nguchiro kwa sababu unaandika usichoelewa. Hiyo inanipa faida kuendelea na yenye maana kuliko reply yako hapa.
 
Yamkini hutembei hii Tanzania mkuu, kwa wanaotembea hii Tanzania, yapo mengi makubwa ambayo yanaonyesha kodi zinaenda wapi, na mikopo inaenda wapi.😅😅😅😅😅 MATAKO YANA KUWASHA WEWE
Bado unaonyesha wewe ni Nguchiro.
 
Kwa bahati mbaya kwako unasoma na huelewi maana ya kilichoandikwa, hivyo inakupelekea moja kwa moja kuwa Nguchiro kwa sababu unaandika usichoelewa. Hiyo inanipa faida kuendelea na yenye maana kuliko reply yako hapa.
Sasa mkuu, si utueleweshe ni wapi hatujakuelewa kuliko kurudia rudia tu kwamba hatuelewi na hatutoi hoja za maana?
 
Back
Top Bottom