Wanasiasa na hatima ya nchi yetu!

Ruhinda

Member
Aug 29, 2011
24
0
Wakuu wangu wana JF salaam....,

Kila nikikaa na kuwaangalia au kuwasikiliza wanasiasa katika nchi yetu, siasa zao wanazopiga na hali ya nchi yetu ilipofikia huwa najiuliza kama kweli wana macho na masikio ya kuonea na kusikilia. Lakini pia huwa najiuliza kama huwa wanajua vitu vya msingi ambavyo wananchi wao wanavihitaji kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.

Leo ushabiki wa kisiasa ndio kipaumbele kwa wanasiasa wetu, hata kama wanajua chama fulani ni janga lakini kwa kuwa wao wanapata chochote kupitia hicho basi watendelea kukipigia debe bila kuangalia maslahi mapana ya Taifa. Matokeo yake hukwepa hoja nzito kama za ufisadi na kuanza kushambuliana wao kwa wao kwa hoja nyepesi nyepesi zisizokuwa na tija. Na sisi humu hujikuta tumeangukia kwenye hoja zao na kuanza kuchangia na kuwapa kiburi kana kwamba walichokileta kina tija.

Wakati nchi yetu inaliwa na mafisadi kwa kutorosha nyara ughaibuni, wakati mafisadi wakikwapua hela zetu na kuzipeleka kuzificha ughaibuni. wakati hali ya kiuchumi ya watanzania inazidi kua mbaya, wanasiasa ambao tungetarajia waje hapa JF na hoja mbadala za kuikomboa nchi yetu wanakuja na kujadili vitu kama "KADI ZA VYAMA"!

Ndg, wana JF mi napendekeza kwamba mtu yeyote ambaye ni mwanasiasa akija hapa na hoja zake nyepesi nyepesi zisizo na tija kulingana na hali ya nchi yetu, tusizichangie badala yake tumchape maswali mazito yenye kuhitaji majibu mazito kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu, ndio kusema tuhamishe hoja yake na kumpa hoja nyingine.

Hoja ya kipuuzi, ushabiki wa kisiasa usio na tija, tuupuuze. Hatima ya nchi yetu iko mikononi mwetu kama wananchi na si mikononi mwa wanasiasa vipofu wanaotanguliza itikadi za vyama vyao na wala si maslahi mapana ya ustawi wa nchi yetu.

Wenu,

Ruhinda
 
Kitanga

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
366
250

Tumefika hapo kwa kutokuwa makini katika kujua malengo halisi ya vyama vya siasa na wanasiasa wenyewe. Kila mtu Tanzania ni mwanasiasa na hata kama hajui itikadi ya chama chake bado atataka kuaminisha watu kuwa yeye ni mzuri na sera za chama chake ndo nzuri. Mfano, hivi karibuni tumeona tatizo ya fedha katika siasa na jinsi tunavyopatiwa viongozi wa rushwa. Hawa watu wakiingia madarakani ni kutafuta namna ya kulipa fadhila na kurudisha pesa walizotumia kupata vyeo. Lakini tungekuwa makini kwa kuwatosa hawa watu, tungepata viongozi safi na wenye mapenzi mema Watanzania na nchi.
 
Mtanzania1

JF-Expert Member
Dec 30, 2010
1,168
1,250
Mkuu kazi yao ni siasa...wanatetea matumbo yao.....wapate wanachama wengi.....wapate ada..washike dola...wadhibiti kodi na rasilimali zetu...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom