Wanasiasa msiwatumie waTZ kwa manufaa yenu ya kisiasa

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,836
Nimekuwa na muda mrefu sana ninafuatilia mambo ya siasa na nimegundua ni mchezo mchafu sana.
Mchezo huu unahatarisha maisha si ya wanasiasa bali ya wananchi wasio na hatia.
Nimekua nikifikiria hivi hawa wanasiasa wanapata faida gani wanapozunguka huku na huku majukwaani wakinadi sera zao, hivi kweli ni wazalendo na wanachokiongea ndio hicho? Mwisho wa siku nimeona kuwa sio wazalendo na wala sio watu wanaojinadi kuwa ni wakombozi.

Kunavyama hapa nchini zaidi ya 5 kila mmoja lengo lake ni kutawala nchi. Huku nyuma ya pazia wako na ajenda yao ya siri na kuwahadaa watz kuwa wao ni wakombozi. Wakitumia shida na changamoto za maisha kama kigezo cha wao kupewa nafasi ya utawala.

Mambo ya muhimu ya maendeleo hawayapigii kampeni wanakaa kimya.

Mfano tu mmoja tunazoezi la sensa kitaifa, wanasiasa wamekaa kimya hakuna hata mmoja anaye ongelea hilo. Zaidi tu kueneza propaganda mbalimbali ambazo hazimsaidii mtanzania.


Haya ni maoni yangu kuwa wanasiasa wanataka kutumia watanzania kwa manufaa yao.
Naomba tu wawe wawazi kuhusu mali wanazo miliki. Na sisi watanzania tusipelekwe pelekwe na mtu yeyote tutumie akili zetu na kufikilia.
 
we hujamsikia pimda akinadi sensa au ulitaka nani aongelee sensa? Na ni kwanini ccm isaidiwe kutimiza wajibu wake?kama haiwezi ikae kushoto SAU ichukue nchi
 
mkuuu1 sasa ivi hii nchi haina siasa tena,watu wanapigania stahiki zao sasa! amsha akili iyo.
 
annael mawazo yako ni mazuri,lakini ujue siasa bila watu haipo!kwa hiyo siasa na watu ni vitu amabvyo havitengani,pia siasa unaumhimu wake,bila siasa hatuna watawala,mipango ya maendeleo inatoka na siasa,maendeleo ya nchi pia yanategemea siasa.
labda ungewashauri watu wafanye siasa safi zenye ustawi wa maendeleo na sio siasa za kifisadi
halafu pia ujue kuwa ,upende siasa,uchukie siasa,bado matatizo ya kisiasa yakitokea yatakuathili tu.
mie badala ya kuponda siasa,naomba watanzania wapime siasa safi zenye manufaa kwao,wawachague viongozi watakaoweza kuwawajibisha maana tunaona kwenye nchi za wenzetu haya mambo yanawezekana.
 
ambaf taja hao ni nani ni chama cha mabwepande hata marekani kuna siasa na watu sasa siasa bila watu ni siasa? Jpange naonautakuwa umekosa share some where. sanz yako
 
ambaf taja hao ni nani ni chama cha mabwepande hata marekani kuna siasa na watu sasa siasa bila watu ni siasa? Jpange naonautakuwa umekosa share some where. sanz yako
<div> <b> Poa</b></div>
 
Mleta mada unachekesha, wanasiasa na kuwatumia wananchi ni sawa kabisa, kama wasipowatumia wananchi wawatumi wanyama? Hata wananchi pia tunawatumia wanasiasa kututengenezea mfumo mzuri wa utawala ili tuishi ktk nchi yetu kwa amani, upendo na mshikamano. Pia kila chama lengo lake ni kushika hatamu siku moja. Maisha ya binadamu ni kutumiana. Mimi nakutumia hapa na wewe unanitumia pale. Kubali au kataa.
 
mbona we mwenyewe upo kisiasa? Mada yako ipo kisiasa' lazma systm ya nnchma ibadlshwe imeoza kabxa.
 
Back
Top Bottom