Wanasiasa mjiheshimu sana

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,330
2,000
Huwa sipendi kuwaongelea maana najua fika mu waongo waongo sana, ila sasa ngoja haya nisije kufa nayo moyoni.

Kwanza kabisa nianze na huyu Mzee Lowassa please jiheshimu sana, usituone tuko kimya ukahisi tu wapuuzi sisi(watanzania million 6) tuliokupatia kura binafsi nilikupa kura yangu nikiwa ccm ulikohama, usijedhania nilikuwa nakupenda kuliko kijani mpk nikakupa kura yangu ungetaka kujua ungegombania urais ukiwa ccm uone km ungepata kura yangu.

Sikufanya hivyo kwa kukuamini, nilikuwa nimechoshwa na porojo za kikundi fulani ndani ya CCM kujiona ukoo wa kifalme. Binafsi nilitaka nikutumie kubomoa hicho kikundi ingawa ulikuwa mmoja wao.

Mzee Lowassa usivimbe kichwa nasema kwa dhati bila chuki, hivi kipi cha ziada unacho wewe mzee mpk binafsi najiuliza ni uzuzu wetu watanzania/wanaccm au kuna mazingara unatumia wewe mzee..? Huna mvuto wa kisiasa labda tungesema huwa una speech zinazosisimua HAPANA umezeeka na u kikongwe kusema tuweke tumaini kwako ni sawa na kupanda bua la mhindi afu utegemee kuvuna mhindi.

Kiufupi wewe mzee jiheshimu tafadhali sana, sisi si wajinga hivyo tadhali unakera sana, nimekuona mtu wa hovyo kabisa na malaya wa kiwango cha kahaba wa siasa.

Nirudi kwa WAPINZANI, nitawasema wafuatao MBOWE, MAARIM SEIF, ZITTO, LIPUMBA nikitaja wachache kwa umhimu wa upuuzi wao. Mh.MBOWE una shida gani wewe mzee binafsi unanikera sana u mtu usiye na maono wala plans zozote ila ubishi na king'ang'anizi unayeponza CHADEMA na UPINZANI nchini nasema haya sababu kubwa moja tu kwanini uandai vijana wa kuendesha Chama cha Demokrasia na Maendeleo, huwezi kumuweka mtu km prof. Baregu strategic man pembeni afu eti wewe ukae na uwe mwenyekiti upuuzi gani huu....? Yupo prof. Safari why don't you allow these stonemen to lead CHADEMA.....?? Ni wewe Mbowe umemkimbiza Zitto na Mkumbo na Mwita Waitara, pia vijana wengi sana wakina Katambi na wengine. Please nikuombe achia ngazi bakini km mshauri waamini vijana wakina HECHE, MNYIKA, LISSU, MWALIMU, MSIGWA, MDEE, ESTHER, MATIKO jamani wapisheni na wapo underground wengi mno wanaogopa mfumo wako hapo juu uliojaa sura za ukabila na ukanda.

Waliobaki narusha nyukilia iwamalize wote kwa mpigo, Maarim Seif, Lipumbav, Mbatia, Zitto, ebu acheni ujinga vunjeni hizo vyama zenu uchwara uundeni chama kimoja na toeni kipaumbele kwa vijana.

Yaani zaidi ya miaka 20 hamjaona kuichallenge CCM kinahitajika chama kimoja chenye nguvu na mshikamano wa hali ya juu..? Eboooo mnakera na kuboa sana nyie wazee na vijana wapuuzi wachache..! Badirikeni ishiiii..... Otherwise mnatuboa sana.

KUBWA LAO CCM, hakuna kitu kinakera kama chama changu CCM hizi kero zote zimeletwa na viongozi wake wakiongozwa na m/kiti wake mh. Dr. John P Magufuri na rais wa Tanzania na ndugu. Bashiru Ally katibu mkuu wa CCM pamoja na H. Polepole.

Jamani nyie watu jiheshimuni, mnatia aibu na kutuchefua siye watanzania wazalendo ebu fanyeni siasa kisayansi na kisasa tunaposema nchi yetu ni ya kidemokrasia please we need to see this democracy prevailing not otherwise.

Dr. Bashiru acha ukanjanja wako tendea haki demokrasia. Pingana ata m/kiti waki akikufukuza kazi sawa maana bora utunze na kulinda dhamira yako maana itakuhukumu siku si nyingi, mna double standard nyingi za kijnga, upendeleo wa kichama ni ujinga, CCM mikutano sawa wapinzani hakuna ni ujinga na upuuzi, visa vya kufungana na kuviziana kukamata huviioni ukakamea bila kujali nani anavifanya..? Haya mambo yakiota mizizi kuyang'oa si rahisi km mnavyodhani.

Mh. Rais ebu usitugeuze wapuuzi sisi watanzania ebu simamia haki acha double standard, ulikataza mikutano sasa mzee Lowassa ni nani nchii akafanye mikutano ya hadhara Monduli...?? Yapo mambo mengi mnajaribu kutushika mdomo tusiseme ila tunayajua na tutasema kila tutakapopata wasaa na nanafasi ya kusema. Mfano mh. Tundu Lissu anasemwa vubaya sawa ila nikuulize swali. "TUKIO LA KUSHAMBULIWA KWAKE LILIKUWA KUBWA NCHINI MWETU KWA MJIBU WA HISTORIA NA USTAARABU WETU KAMA NCHI , ZAIDI YA MWAKA MNALICHUKULIA POA UPO KIMYA UTADHANI ULIJUI UKIWA KAMA MKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NA RAIS WA NCHI...., LABDA MH. TUNDU LISSU AFANYEJE...?? ATA KINAFIKI UNASHINDWA KUJISEMESHA KAMA ULIPENDEZWA NA KUSHAMBULIWA KWAKE....? Juzi kati ulikiri kuwa watanzania sisi si wajinga tunaweza kuhoji na kuchambua mambo iwehe wewe pia unanyamaza kimya kwa mambo mabaya hivi..?? Yanaleta makovu ambayo si rahisi kupotea.

Mwishi ujinga wa kuhamisha wanachama ni siasa za kishamba sitaki kusema kama CCM tunawanunua hawa wapinzani iwe kwa vyeo au pesa ukumbuke ni rushwa ni adui wa haki na watanzania tunaona na hatupendezwi tukiwa CCM au upinzani nje vyama.

Nimalize kwa Kusema " HAKUNA CCM IMARA BILA UPINZANI IMARA, SASA KUUA UPINZANI NI SAWA KUIPELEKA CCM KITANDANI IKACHAPE USINGIZI.

"Politicians STOP fooling us(Tanzanians).

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
29,555
2,000
Ulikua upo mawazoni mwangu! hii thread i a ujumbe mzito sana..jana saa 2 TBC news zaidi ya dk 20 ilikua ni hbari za ccm..full kampeni...!niliumia kbs rohoni nilipomuona EL anaongea kwao Arusha huyu mzee huenda ana mental pbm..hv anajua watu walovyojitoa kuhusu yy?watu walikua hawalali wengine walinusurika kuvunja ndoa kisa Lowasa leo anakuja kutugeuka kishenzi shenzi tu ..nataman kupotea nchi hii mm..watu tuliweka rehani vibarua vyrtu na ndoa zetu kwaajili ya msenge huyu leo anaondoka km kitu cha kawaida!
Naamini machungu na machozi yetu Mungu atatulipia hapa hapa !huyu hachukui 3yrs Israel atamwita!shenzy
 

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,330
2,000
Lowassa ni mtu mpuuzi na CCM wanao muona kama shujaa..! Nadhani kuna cha kujifunza kwa hawa wanasiasasa uchwara na wapiga porojo wote kwa ccm na upinzani wote ni wapuuzi wanaangalia maslahi yao.
Ulikua upo mawazoni mwangu! hii thread i a ujumbe mzito sana..jana saa 2 TBC news zaidi ya dk 20 ilikua ni hbari za ccm..full kampeni...!niliumia kbs rohoni nilipomuona EL anaongea kwao Arusha huyu mzee huenda ana mental pbm..hv anajua watu walovyojitoa kuhusu yy?watu walikua hawalali wengine walinusurika kuvunja ndoa kisa Lowasa leo anakuja kutugeuka kishenzi shenzi tu ..nataman kupotea nchi hii mm..watu tuliweka rehani vibarua vyrtu na ndoa zetu kwaajili ya msenge huyu leo anaondoka km kitu cha kawaida!
Naamini machungu na machozi yetu Mungu atatulipia hapa hapa !huyu hachukui 3yrs Israel atamwita!shenzy

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom