Wanasiasa: Kuingiliwa kwa Wahasibu na Wakaguzi kulivyowahi kuangusha makampuni na kutikisa chumi za nchi

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,760
6,294
Wakuu.

Tanzania tumezidiwa na nguvu ya siasa. Siasa kutoka ku-control kila ueledi ni Laana ya ajabu.
Naweza kusema hivyo baada ya sakata la kutoelezeka kwa matumizi ya shilingi trillion 1.5 kama ripoti ya Ukaguzi ya CAG kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Katika ukurasa wa 34 wa ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 anasema,
"Kati ya Shilingi bilioni 25,307.48 zilizokusanywa, Shilingi bilioni 23,792.30 zilitolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi, matumizi mengine, matumizi ya maendeleo na fedha kwa ajili ya kulipa madeni yatokanayo na amana za Serikali pamoja na riba. Kielelezo cha hapo chini kinaonesha fedha za matumizi katika mwaka wa fedha 2016/17"


Kwa maelezo hayo ni kwamba kuna bakaa “baki” ya shilingi trillion 1.5 ambazo hazijulikani zimetumika wapi.
Katika ukaguzi kuna kitu kinaitwa “Audit Query” ambapo mkaguzi husema upungufu/udhaifu aliouona.

CAG (kama Mkaguzi) si polisi au mahakama kwamba atoe hitimisho kwamba fedha hizi zimeibwa.
Hata sharia ya kazi yake inasema madhaifu yaliyopo ktk ripoti yashughulikiwe na bunge, na hoja ikishindwa kufungwa huko basi inaweza kuamuliwa mahakamani. Kiufupi bunge hutoa maelekezo kwa serikali kwa sababu serikali ndiye mkaguliwa.

Hapa nitaeleza visa 10 vya namna Wakaguzi na Wahasibu walivyowahi kutumika kudanganya ripoti na baadae kuja kusababisha anguko la makampuni au uchumi wan chi kutikiswa.

1. WORLDCOM SCANDAL (2002)

Ni kampuni ya nini?
Mawasiliano

Nini kilitokea?
Kudanganya mtaji (assets) kwa zaidi ya dola billion 11, kulikopelekea wafanyakazi 30,000 kufukuzwa kazi na hasara kwa kampuni kiasi cha dola billion 180.

Wasuka dili/Wahusika wakuu
Mtendaji Mkuu (CEO) Bernie Ebbers

Dili ilisukwaje?
Alishusha matumizi kwa kuongeza mtaji badala ya gharama, na kupandisha mapato kwa mauzo feki.

Namna ilivyogundulika
Idara ya Mkaguzi wa ndani wa WORLDCOM aligundua ubadhirifu wa dola billion 3.8
Hapa ukaguzi zaidi ukaagizwa. Kampuni ilitangazwa Bankruptcy (mufilisi)


Adhabu
Mkuu wa Idara ya Fedha (CFO) alifukuzwa kazi, Mdhibiti (controller) aliachia ngazi, Kampuni ikashindwa kujiendesha na kutangazwa mufilisi.
Mkurugenzi Ebbers alifungwa miaka 25 jela kwa ubadhirifu uhujumu na kuwapa nyaraka bandia wakaguzi.



2. TYCO SCANDAL (2002)

Ni kampuni ya nini?
Kampuni ya Ulaya (iliyokuwa New Jersey) ya mifumo ya ulinzi

Nini kilitokea?
Mkurugenzi Mkuu (CEO) na Mkuu wa Idara ya fedha (CFO) waliiba dola million 150, na kudanganya kwa kuongeza mapato katika vitabu kwa dola million 500.

Wasuka dili/Wahusika wakuu
CEO Dennis Kozlowski na CFO Mstaafu Mark Swartz.

Dili ilisukwaje?
Walijilipa mikopo na marupurupu ya kiutendaji. Pia walijilipa kama wasambazaji wa bidhaa kwa kampuni.

Namna ilivyogundulika
Uchunguzi uliofanywa na Kamisheni ya dhamana ya Dhamana na Mitaji ya Marekani (SEC) iligundua kukiukwa kwa kanuni za kihasibu na mikopo mikubwa kwa Kozlowski.

Adhabu
Kozlowski na Swartz walifungwa miaka 25. Kampuni Tyco iliamriwa kulipa fidia kwa wawekezaji dola biliion 2.92

……………………………………List itaendelea hadi visa vyote kumi (10)……………………..

Hoja
Kwanza, ni uwendawazimu kumshamshulia Mkaguzi (CAG)

Pili, wote mnaona namna ambavyo namba hupikwa ili kuwapa wahusika matumaini hewa. Hapa ndio jukumu la Mkaguzi hutakiwa ili kung’amua ukweli wa hizo namba.

Rais, Mawaziri, Makatibu wakuu, na Wakurugenzi na maafisa wengine wa serikali ni wakaguliwa wa namna walivyotumia mali hizo za wananchi (kodi)
Katika sekta ya umma, CAG ndiye mlinzi/mhakiki wa mali za umma na thamani ya uwekezaji wa umma.
Kunapokuwa na mkanganyiko wowote ktk ukaguzi wa CAG, ni bunge ndio chombo cha kuhoji na sio Mawaziri/Rais ambao hawa ndio wakaguliwa.


Tukija kuendelea na makala hii utakuja kugundua namna ambavyo si afya kiuchumi kuchukia kazi ya Mkaguzi mfano CAG.

Kasomeni historia ya “Auditing” ambayo ilitokana na Principal-Agency business relationship”.
 
I read on paper concerns how politics affect public service and professionalism in Africa , sikumbuki mwandishi.
Hakika ni sawa na haya yanayotokea Tanzania.
Mfano:
1. Ukaguzi ni suala ambalo ni very professional na Kwa mujibu wa Sheria na taratibu zetu ni miongozo ya kujibu hoja za CAG zipo na sivyo ilivyofanyika Ikulu ya kuulizana hadharani, taratibu za kujibu hoja za CAG zifuatwe.
2. Anayofanya bashite hususani hili jipya aliloliibua la kupika tezi dume nyumba Kwa nyumba, Kwa mujibu wa ethic na professionalism za utabibu hilo halikubaliki.
 
Kwani accounting officer wa fedha za serikali ni nani? Katibu mkuu Hazina ambae ni mjomba wa Magufuli na pengine ndio maana povu linamtoka!!
Huyo mtoto wa Dada yake Jiwe anamrishwa tu atoe pesa hazina......

Kwa hiyo uchunguzi wa kina ukifanyika itajulikana ni nani yuko behind all these mess
 
Kwa hali yoyote ile hata kama tunampenda Mh. Raisi tunaomba au kushauri bunge lifuatilie vizuri kuondoa mashaka yoyote yaliyojitokeza.
Wakati tukijiandaa kumuunga mkono mheshimiwa sana ashinde vita ya kiuchumi lakini na yeye aangalie upande wake kwa wale aliowapa dhamana.
Ikishindikana kupatikana muafaka kwa hali ya kawaida basi tume huru ya kibunge ndio lituletee majibu sahihi na sio haya ya sasa ingawa yana akisi ukweli wa wapi fedha hizo zimetumika. Lakini hii haiondoi mashaka yote.
 
I read on paper concerns how politics affect public service and professionalism in Africa , sikumbuki mwandishi.
Hakika ni sawa na haya yanayotokea Tanzania.
Mfano:
1. Ukaguzi ni suala ambalo ni very professional na Kwa mujibu wa Sheria na taratibu zetu ni miongozo ya kujibu hoja za CAG zipo na sivyo ilivyofanyika Ikulu ya kuulizana hadharani, taratibu za kujibu hoja za CAG zifuatwe.
2. Anayofanya bashite hususani hili jipya aliloliibua la kupika tezi dume nyumba Kwa nyumba, Kwa mujibu wa ethic na professionalism za utabibu hilo halikubaliki.
Tunatengeneza nchi ya ajabu sana. Tuna kiongozi anayepemba kujitukuza na ana act ki-pomposity ya hali ya juu
 
Nafikiria CEO anayepaswa kufungwa kwenye sakata hili la 1.5T ni nani?
CEO na CFO. Wote wana kesi za kujibu. Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu wa Idara ya Fedha.

Nadhani unaelewa kiserikali nani ni nani.....
 
Kwa hali yoyote ile hata kama tunampenda Mh. Raisi tunaomba au kushauri bunge lifuatilie vizuri kuondoa mashaka yoyote yaliyojitokeza.
Wakati tukijiandaa kumuunga mkono mheshimiwa sana ashinde vita ya kiuchumi lakini na yeye aangalie upande wake kwa wale aliowapa dhamana.
Ikishindikana kupatikana muafaka kwa hali ya kawaida basi tume huru ya kibunge ndio lituletee majibu sahihi na sio haya ya sasa ingawa yana akisi ukweli wa wapi fedha hizo zimetumika. Lakini hii haiondoi mashaka yote.
Ni kweli. Hata wanaompenda mh Rais wamwambie atulize akili. Aache vyombo huru vifanye uchunguzi vitoe majibu.
 
Tanzania ilikuwa haijafikia Viwango vya kuwa Na CAG Kama Prof Assad!
Size yetu ni kina Ludovick Uttoh ambao report zao ziliangaIia Na Mazingira ya Kisiasa ya wakati husika
Pohamba mkuu una maanisha CAG huyu ni msumari zaidi. Penye kijiko anasema kijiko na sio beleshi/koleo.
 
Back
Top Bottom