Wanasiasa kifunzeni kutumia vyombo vya habari vizuri.

ARCHBISHOP

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
270
500
Wana Jf,Nimekuwa nikifatiria kwa ukaribu masuala ya kisiasa yanayoendelea kwa sasa, na nimegundua jambo kubwa linalo sababisha kudumaa kwa ushindani kisiasa, vyama vya upinzani vinakilaumu CCM na CCM kinavilaumu vyama vya upinzani, matokeo yake kipindi cha uchaguzi wananchi hawaelezwi mipango ya mandeleo, mkutano unaishia kusengenyana na kupigana majungu, siku ya uchaguzi ukimwuliza mpiga kura nini kinamsukuma kupiga kura, atakwambia aither amechoshwa na CCM au anaogopa vurugu za wapinzani anazoziona leo zisiingie Ikuru.Nimegundua nini?,Wanasiasa wa nchi hii hawana mipango madhubuti yakukabiriana na majanga au mtetemo wa kisiasa, wote ni watu wa matukio, na mbaya zaidi hawana muda wa kutafakari kabla yakuwaita wana habari na kutoa misimamo yao, wengi wanakuwa too defensive wakiwaza maslahi ya vyama vyao na siyo maslai ya wananchi.

CCM;
Pole pole ninavyomjua ni mtu makini sana na anauwezo mkubwa sana kichwani, rakini kuna wakati anajitoa akiri kwa maslahi ya chama, na kuna wakati anatoa matamko kwa jazba na mihemko ya kisiasa anasahau kuna mamilioni tunamsikiliza na tunapata muda mwingi wa kurudia hizo clip na kugundua madhaifu mengi. Humphrey pata mtu wakukusaidia Twitter na kwingineko hata kwenye press conference.

Wapinzani;
Katika kipindi hiki cha viongozi na wanachama kuhamia CCM ndicho kipindi tumeweza kuona na kupima uwezo wa kuhimili mikiki ya siasa ulivyo chini kwa wanasiasa wa upinzani,

Ni juzi nolimsikia Abdul Kambaya akimshamburia Mbunge wa Kinondoni kwa kujiuzuru ubunge na kwenda CCM, Kambaya aliongea mengi rakini kati ya hayo alidai yule mbunge aliwahi kujitoa kiutata kwenye mbio za udiwani na walitiria shaka uamuzi huo, kambaya akagombea mwenyewe, pia 2015 wakati anataka kuporwa ushindi, hakujihusisha wala kuwasiriana, mpaka Kambaya akaingia kwa nguvu kwenye chumba cha majumuisho, akasema kwa muda mrefu amekuwa si mtu wa kuaminika, sasa swali ni je, hawana utaratibu wa kuwachuja na kuondoa wagombea wenye kasoro? Kama wanao, kwanini walikuwa wakimng'ang'ania yeye? Wanataka tuamini nini?

Jambo lingine ni kuhusu barua iliyoandikwa kwenda kwa CAG na Mwanachama wa CHADEMA ndugu, Mackdeo Shilinde, barua yenyewe iko wazi. Kilichonishangaza nikusikia kiongozi wa Chadema akisema "kuna mtu anajiita mwanachama wa chadema" Kaandika barua kwa CAG, nilishtuka sana kuona wanamkana hadharani wakati huyu mtu alishagombea mpaka udiwani kata ya Azimio kama sijakosea na amekuwa mstari wa mbele kukitetea chama, leo kafuata utaratibu kupeleka duku duku lake mnamkana? Ujumbe gani mnatupa sisi wananchi?

Mwisho,Leo nimesikiriza press conference iliyoitishwa na Kubenea kuhusu kutuhumiwa kutaka kuhamia CCM, kwakweli sielewi alikuwa anajitetea au anamshamburia Raisi, anajisafisha kwa hofu ya kutengwa, au anataka kuikumbusha jamii kuwa bado yupo?. Utetezi na maelezo yake vilikuwa vyepesi sana, na sijui kama kulikuwa kuna urazima aitishe press, kama siyo kweli angeweza kaa kimya na bado maisha yangeendelea, zaidi angeandika barua kwa uongozi wake kukanusha.

Zitto:
Huyu siku izi amekuwa anakurupuka kwenye vyombo vya habari mpaka nashindwa kumwelewa hivyo sina cha kusema hapa. Anashindana na BBC kubreak news, mengine hana uhakika yeye anabandika tu!
<br /><br />Tafadhari wanasiasa tumieni media vizuri, sasa hivi tukisikia press conference hata hatushtuki kabisa maana ni hoja nyepesi sana zinaletwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom