Wanasheria wetu, mahakimu na majaji kumbukeni mliapa kwa Mungu kuwa mtatenda haki

Mpira wa kona

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
350
338
Hakika nimekuwa nafuatilia utendaji Kazi wa Majaji, Mahakimu Na Wanasheria wetu wa kila siku. Watu hao Kwa pamoja waliapa Kwa Mwenyezi Mungu kuwa Watatenda haki bila upendeleo Na uonevu. Naamini sasa kuwa kiapo hicho hakipo kwani tumekuwa tunashuhudia uonevu mkubwa wanaofanyiwa watu hata kama Sheria iko wazi.

Tumeshuhudia watu wananyimwa dhamana Kwa makusudi tumeona kesi za kulipa faini lakini mtu halipishwi lakini wanasheria na viongozi wa Mahakama wako kimya.Tunawasihi kumbukeni viapo vyenu tendeni haki Mungu atawaangamiza Siku moja.
 
Ni mara chache sana ambapo mahakama inakuwa inaamua kwa busara zake (court dicretion) ila mara nyingi maamuzi yote ni lazima yatoke kwa mujibu wa sheria (sheria ya bunge au maamuzi ya mahakama - precedent)..

Ingawa mahakama inapoamua kwa kutumia busara zake lazima iwe na sababu za maana kuback up huo uamuzi wake..

Tukirudi kwenye ishu yako, naamini kuwa mahakimu na majaji wanapotoa maamuzi huwa wanatoa au wanaeleza nini walichokitumia mpaka kufikia uamuzi huo wanaoutoa na haki ya rufaa huwa inaelezwa..ukiona kilichoamuliwa kimezidi kilichopaswa kuamuliwa au hujaridhishwa nacho basi unapinga maamuzi hayo katika mahakama ya juu zaidi.. Sheria inayoishi ni mapambano, kwa hiyo lazima mtu upambane vyema..

Mahakimu ni waamuzi na wafasiri wa sheria, wanaamua kutokana na hoja zilizoletwa mbele yao na namna walioleta walivyozitetea..sasa uamuzi wao usitafsiriwe kuwa ni wa uonevu..kama sheria imewekwa hivyo na ipo hai basi usimlaumi jaji au hakimu bali ilaumu sheria na bunge lililoipitisha sheria hiyo
 
Hakika nimekuwa nafuatilia utendaji Kazi wa Majaji, Mahakimu Na Wanasheria wetu wa kila siku. Watu hao Kwa pamoja waliapa Kwa Mwenyezi Mungu kuwa Watatenda haki bila upendeleo Na uonevu. Naamini sasa kuwa kiapo hicho hakipo kwani tumekuwa tunashuhudia uonevu mkubwa wanaofanyiwa watu hata kama Sheria iko wazi.

Tumeshuhudia watu wananyimwa dhamana Kwa makusudi tumeona kesi za kulipa faini lakini mtu halipishwi lakini wanasheria na viongozi wa Mahakama wako kimya.Tunawasihi kumbukeni viapo vyenu tendeni haki Mungu atawaangamiza Siku moja.
Mungu wao ni PESA tu!
 
Back
Top Bottom